Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)


Bado ni wezi tu! Mimi nimejiunga na chekatime, hela wamekata na huduma sijapata! Na eti wakasema nitajulishwa kwa sms hakuna cha sms wala nini na hela yangu inaniuma sana!
 
Ni wazi vodacom ni wezi wa siku nyingi huiba salio na kusingizia kuwa umetumia simu vibaya mara umemuachia mtu au ameisahau mtu akachota salio mara ulijiunga na kitu gani sijui ndicho kinatumia pesa yako kwa kifupi vodacom haifai . Mimi nimeshaachana nayo napeta tu na TIGO na AIRTELL
 

Habari,tutumie namba ya simu PM tafadhali.
 

Habari,tutumie namba ya simu PM kwa mawasiliano zaidi.
 
Hawa voda ni MATAPELI walinidanganya kwa sms nijiunge dk 60 kwa Sh 200 nilipojiunga nilipipiga simu ya kwanza na ya pili hazikua na majibu, mara ya tatu nilijibiwa kuwa sina salio .

Nikaamua kuishiana nao kimya kimya sasa nipo kwenye mitandao wanayojua kusoma hali ya soko.
 
Hahahahahah me sina ham nao kubadili line naona zengwe basi wanantia mawazo ila ikifika january ntachukua maamuz magumu insha'allah!
Voda si wezi bali wanyang'anyi
 
Nilikuwa natumia voda kwa net. cha kushangaza nanunua bando na pesa inakatwa afu service sipati. hao customer care kuwapata ni mziki mnene nikaamua kujiweka mbali nao.

mmmh mkuu umezungumzia mambo ya net nikakumbuka, hawa jamaa wamekuwa wezi kuliko hata tanesco, nimefikisha sii chini ya mara 4 nanunua bando 100mb, lkn hata dakika 2 haimalizi net inakata ukiangalia salio hola, SASA sijui ndo fedha za kampeni zinasakwa? na kwa vile ule mpango wao wa kulipia kila mwezi umeingia zwengwe ndo kabisaaaa tuaibiwa kwa nguvu.
 
Voda ni wezi sana mimi waliniibia nikawapigia wakaniambia wamegundua kuna tatizo ni wapigie baada ya masaa matatu ,nilivyowapigia wakaniambia siruhusiwi kupiga huduma kwa wateja mpaka January 15 nilichofanya nikanunua line ya airtel nikacopy majina cjui hata nilikoitupa line ya Voda. I hate this Voda for sure.
 
mh.....hapa bado sijaelewa huu uwizi. kama ndivyo kwa kweli inabidi wapelekwe mahakamani
 
ni kweli hata mimi imenitokea mara kadhaa na juhudi za kuongea na customer care hazikuzaa matunda sasa nimeachana nao.

kama mimi mkuu. Imenitokea mara mbili lakini castomer care kimeo.
 

Pole sana, kama ungekuwa na line ya baba lao ungeongeza shs 3000 tu halafu ungepiga simu mwezi mzima kwa 10,000 internet ya kumwaga na sms zisizohesbika

Hawa akina dogo (voda na tigo) wezi wanataka kula bila jasho, wasamehe bure bado wanakua they have to eat excessively so that they grow big
 
Hili jambo lilinitoke hata mimi majuzi tuu, kila nikitaka kujiunga kifurusha ina kataa lakini salio lina katwa hadi likaisha. nili kerwa sana siku hiyo lakini niliwapigia tuka yamaliza na customer care.

Vodacom ni wasikivu sana.
 
Habari,tutumie namba ya simu PM kwa mawasiliano zaidi.
Mkuu naona kama kawaida yenu mnaomba namba, kama fb vile! Hapa ni JF ni muhimu utoe ufafanuzi wa kutosha mnaana haya matatizo ni kwa watumiaji karibia wote, sasa wewe unaposema pm namba unawasaidiaje wale wasioingia JF!!
 
Mkuu naona kama kawaida yenu mnaomba namba, kama fb vile! Hapa ni JF ni muhimu utoe ufafanuzi wa kutosha mnaana haya matatizo ni kwa watumiaji karibia wote, sasa wewe unaposema pm namba unawasaidiaje wale wasioingia JF!!

umemkimbiza customer care wa watu....teh teh teh..
 
Mtandao wao mbaya sana saiv,mimi nilikua najiunga na Cheka za 500 cha kushangaza,data zinakaa muda mfupi wananiletea ujumbe eti zimeisha bila hata kuzitumia.

Niliwapigia nikapewa majibu hovyo hovyo kabsa,nilipowapigia tena eti nikaambiwa huduma ya bure nimefungiwa mpaka january!

Nilichokifanya nikopy majina kwenye simu na kuivunja iyo line,staki tena Voda nimesharudi nyumban Airtel coz nilihamiaga voda mwaka 2010 bada ya kukuta wanafunzi wengi chuon wanavoda na tiGO bt saiv nimeshamaliza chuo na Airtel ndo mpango mzima.
Voda ni wezi tu!
 
Hiyo iko wazi kbs kuwa vodacom wana matatizo makubwa sana hata ya usikivu wakati unaongea. Hili la wizi limekithili kwani unawekewa wimbo na kukatwa bila ya wewe kuomba wimbo husika. Huu sio mtandao kabisa jamani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…