Habari ndugu mteja,tunaimani tumeelewana kama tulivyozungumza kwa njia ya simu asubuhi ya leo hii,pole sana.
Hata kifuta machozi hapewi, mpeni dk. 60.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Habari ndugu mteja,tunaimani tumeelewana kama tulivyozungumza kwa njia ya simu asubuhi ya leo hii,pole sana.
Kuna wizi mkubwa kwa fedha za salio za wateja unaoendelea sasa hivi katika mtandao wa Vodacom.
Kwa vile hili si jungu bali ukweli nimisha report wizi huo katika kitengo cha malalamiko TCRA kwa hatua zaidi.
Nimeweka salio la Tsha 10,000 mchana wa leo kwa Mpesa ref Y23SY687 na baada ya muda mfupi nikakuta salio langu la maongezi ni sifuri.
Nikanunua vocha na kutumiwa tshs 10,000 na hela yote imekatwa tena.
Wateja wa Vodacom jihadharini, kuna mwizi kaingia mtandaoni Vodacom
UPDATE
=====
VODACOM wamefanya ustaarabu wa kunipigia baada ya kuona detail ya transaction hapo juu, na kuiona kwenye mtandao wa Jamiiforums.
Kimsingi wameapologise kwa mtafaruku uliotokea lakini wamenieleza nifike ofisini kwao kuona aian ya simu ninyotumia isije ikawa data apps ziko wazi.
Na kweli baada ya maongezi ya kuchunguza, mobile data setting ilikuwa ON, na mimeizima sasa.
Hata hivyo ni vema nitaenda kupata maelezo ya kuyeyuka kwa salio langu , karibu 20,000, kwa siku moja.
Wanabodi mtajulishwa inawezekana kuna wenye tatizo kama langu.
Unajiunga ktk promosheni zao, wanakuambia piga namba fulani kisha aidha ujiunge na cheka time au internate masaa 24, unaambiwa subiri ujumbe mfupi utajibiwa. Unasubiri weee! Hakuna kitu, ukiangalia salio limekatwa! Na hakuna huduma hiyo wala nini! Ni kwa nini hamtuhurumii wateja wenu?
Vodacom wamekithiri ktk wizi...
1. Nilijiunga na kifushi cha Cheka, 7000 kwa wiki... Kesho yake kuangalia kifurushi kimekwisha.... Wakati sikutumia sana.
2. Ktk bango lao la kutoa na kutuma pesa kwa Mpesa wameandika kuwa, kutuma fedha kwa wateja wasiosajiliwa kutoka 400,000 mpaka 499,999 wanatoza 7000... Wiki iliyopita nilituma 490,000 wakanikata 7800.. Ikiwa ni ziada ya 800.
3. Kutuma pesa kwa wateja wasiosajiliwa, kutoka 20,000 mpaka 49,999 wanatoza 1,600... Nilituma 20,000 wakanitoza 1,800... Ikiwa ni ziada ya 200.
.
Voda si wezi bali wanyang'anyi
Nilikuwa natumia voda kwa net. cha kushangaza nanunua bando na pesa inakatwa afu service sipati. hao customer care kuwapata ni mziki mnene nikaamua kujiweka mbali nao.
ni kweli hata mimi imenitokea mara kadhaa na juhudi za kuongea na customer care hazikuzaa matunda sasa nimeachana nao.
Vodacom wamekithiri ktk wizi...
1. Nilijiunga na kifushi cha Cheka, 7000 kwa wiki... Kesho yake kuangalia kifurushi kimekwisha.... Wakati sikutumia sana.
2. Ktk bango lao la kutoa na kutuma pesa kwa Mpesa wameandika kuwa, kutuma fedha kwa wateja wasiosajiliwa kutoka 400,000 mpaka 499,999 wanatoza 7000... Wiki iliyopita nilituma 490,000 wakanikata 7800.. Ikiwa ni ziada ya 800.
3. Kutuma pesa kwa wateja wasiosajiliwa, kutoka 20,000 mpaka 49,999 wanatoza 1,600... Nilituma 20,000 wakanitoza 1,800... Ikiwa ni ziada ya 200.
.
Mkuu naona kama kawaida yenu mnaomba namba, kama fb vile! Hapa ni JF ni muhimu utoe ufafanuzi wa kutosha mnaana haya matatizo ni kwa watumiaji karibia wote, sasa wewe unaposema pm namba unawasaidiaje wale wasioingia JF!!Habari,tutumie namba ya simu PM kwa mawasiliano zaidi.
Mkuu naona kama kawaida yenu mnaomba namba, kama fb vile! Hapa ni JF ni muhimu utoe ufafanuzi wa kutosha mnaana haya matatizo ni kwa watumiaji karibia wote, sasa wewe unaposema pm namba unawasaidiaje wale wasioingia JF!!
Pole mkuu,kama wanaiba hivyo dawa ni kusitisha matumizi ya huduma za Vodacom.
Tangu leo nitatumia sim card yangu ya mitandao mingine si Vodacom.