Vodacom Tanzania
Official Account
- Aug 12, 2013
- 324
- 126
- Thread starter
-
- #1,821
Naitwa kilua nawapenda sana vodacom na pia mimi niwakala wenu ila kitendo cha kunikata pesa ninapojazafloat kinatuumiza sana hasa ukizingatia kuwa hamtoi mitaji bali mitaji tunayoikopa ktk vikundi ndio hiyo hiyo inayoleta faida vodacom bila nyinyi kuchangia chochote leo hii tena mnazichota bila sababu yoyote badala ya kutusaidia kama wapinzani wenu wanavyotoa gawio mbali ya kamisheni nyinyi ni kinyume iinahuzunisha
Mimi nipo tunduru- marumba! netwrk inazingua sana wakat mnara wa voda upo aiseeee! ni mateso uktaka kuwasliana hadi ujiposition mbali na makazi ya watu
Poleni sana tonyz na tunaomba radhi kwa usumbufu unaojitokeza, tafadhali tunaomba namba ya simu PM kwa msaada zaidi.Tupo Kibaigwa Dodoma internet iko slow mno had inaboa mbona mnazidiwa na tigo tuboresheen huduma.
Karibu sana Beatrice, jitahidi kutembelea hapa https://www.vodacom.co.tz/careers ndipo nafasi za kazi hutangazwa.Naombeni kazi
Mbona page not found??
Nashukuru kwa majibu yako.
Fungulia kupitia Kompyuta ndugu mteja.
Mtandao wenu hapa Kinyerezi upo chini sana, kupiga simu ni kwa shida, internet ndio kabisa huwezi kufanya chochote. Njoni mshuhudie wenyewe kwani nimekuwa natoa taarifa hizi mpaka nimechoka sasa imebidi niwahame. Ukiwa Kinyerezi mwisho ukielekea kaskazini mashariki kilometa 1 tu unapoteza mawasiliano. Kwanini msijenge mnara eneo hili? Kitu gani kinawashinda, mbona tigo, airtel wote wana minara eneo hili. Chukueni hatua, mnapoteza sana wateja eneo hili
Habari Bedo, hii inatokea pindi unapokuwa umefungua huduma za Intaneti kisha ukaweka salio, unachotakiwa kufanya ni kuzima huduma za Intaneti ongeza salio na nunua kifurushi kisha fungua huduma. Ahsante
Habari mkuu, intaneti bila mpaka inamaanisha kuwa utapata intaneti kwa muda wote uliolipia, mfano ulinunua kifurushi cha siku 30 ni kwamba hata ukimaliza kifurushi cha ukubwa kamili ndani ya siku 20 utaweza kupata Intaneti kwa siku 10 zilizobaki. Ahsante
Acha uongo hayo yote nimefanya na bado tatizo liko palepale usitufanye sis wajinga then acha tabia ya kujibu maswali kwa kukariri ni hatari sana hiii tabia mnaboa sana
Habari Service, katika utatuzi wa tatizo kuna hatua za awali za kufanya mojawapo ni kumshauri mteja au kuhakiki kwamba mteja anapata uelewa na kifaa anachotumia hatua zinazofuata ni kuangalia tatizo katika mifumo yetu. Unaweza kututumia PM ukitufahamisha tatizo lako na usisahau kuweka namba ya simu.achaeni tabia ya kujibu maswali kwa kukariri hii tabia inaumiza sana mambo hayo yote nimeyafanya lakin bado tatizo huwa pale pale hebu jaribu kufanya alternative ya hii jambo
Habari Daud, endapo kutatokea tatizo mteja hurudishiwa salio lake.