Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Naitwa kilua nawapenda sana vodacom na pia mimi niwakala wenu ila kitendo cha kunikata pesa ninapojazafloat kinatuumiza sana hasa ukizingatia kuwa hamtoi mitaji bali mitaji tunayoikopa ktk vikundi ndio hiyo hiyo inayoleta faida vodacom bila nyinyi kuchangia chochote leo hii tena mnazichota bila sababu yoyote badala ya kutusaidia kama wapinzani wenu wanavyotoa gawio mbali ya kamisheni nyinyi ni kinyume iinahuzunisha

Ahsante kwa mrejesho BUGE na tumelifikisha suala hili idara husika.
 
Mimi nipo tunduru- marumba! netwrk inazingua sana wakat mnara wa voda upo aiseeee! ni mateso uktaka kuwasliana hadi ujiposition mbali na makazi ya watu

Tunaomba radhi kwa usumbufu ndugu mteja, mafundi wetu wanajitahidi kutatua hali yoyote inayojitokeza ili kuwapa waeja wetu huduma bora. Unaweza kututumia namba ya simu PM kwa msaada zaidi.
 
Tupo Kibaigwa Dodoma internet iko slow mno had inaboa mbona mnazidiwa na tigo tuboresheen huduma.
Poleni sana tonyz na tunaomba radhi kwa usumbufu unaojitokeza, tafadhali tunaomba namba ya simu PM kwa msaada zaidi.
 
Mtandao wenu hapa Kinyerezi upo chini sana, kupiga simu ni kwa shida, internet ndio kabisa huwezi kufanya chochote. Njoni mshuhudie wenyewe kwani nimekuwa natoa taarifa hizi mpaka nimechoka sasa imebidi niwahame. Ukiwa Kinyerezi mwisho ukielekea kaskazini mashariki kilometa 1 tu unapoteza mawasiliano. Kwanini msijenge mnara eneo hili? Kitu gani kinawashinda, mbona tigo, airtel wote wana minara eneo hili. Chukueni hatua, mnapoteza sana wateja eneo hili

Acha uongo hayo yote nimefanya na bado tatizo liko palepale usitufanye sis wajinga then acha tabia ya kujibu maswali kwa kukariri ni hatari sana hiii tabia mnaboa sana
 
Habari Bedo, hii inatokea pindi unapokuwa umefungua huduma za Intaneti kisha ukaweka salio, unachotakiwa kufanya ni kuzima huduma za Intaneti ongeza salio na nunua kifurushi kisha fungua huduma. Ahsante

achaeni tabia ya kujibu maswali kwa kukariri hii tabia inaumiza sana mambo hayo yote nimeyafanya lakin bado tatizo huwa pale pale hebu jaribu kufanya alternative ya hii jambo
 
Habari mkuu, intaneti bila mpaka inamaanisha kuwa utapata intaneti kwa muda wote uliolipia, mfano ulinunua kifurushi cha siku 30 ni kwamba hata ukimaliza kifurushi cha ukubwa kamili ndani ya siku 20 utaweza kupata Intaneti kwa siku 10 zilizobaki. Ahsante

Andikeni kuwa unapewa 20g siyo bila kikomo by way what is unlimited bundle ?kama hiyo ndio maana yenu ....huu ni udanganyifu kwa Wateja....
 
Acha uongo hayo yote nimefanya na bado tatizo liko palepale usitufanye sis wajinga then acha tabia ya kujibu maswali kwa kukariri ni hatari sana hiii tabia mnaboa sana

achaeni tabia ya kujibu maswali kwa kukariri hii tabia inaumiza sana mambo hayo yote nimeyafanya lakin bado tatizo huwa pale pale hebu jaribu kufanya alternative ya hii jambo
Habari Service, katika utatuzi wa tatizo kuna hatua za awali za kufanya mojawapo ni kumshauri mteja au kuhakiki kwamba mteja anapata uelewa na kifaa anachotumia hatua zinazofuata ni kuangalia tatizo katika mifumo yetu. Unaweza kututumia PM ukitufahamisha tatizo lako na usisahau kuweka namba ya simu.
 
Internet yenu inasumbua sana, maeneo ya tegeta na mbezi beach karibu na bot flats
 
Habari Daud, endapo kutatokea tatizo mteja hurudishiwa salio lake.

Hilo swali niliwauliza ili kujua uongo wenu uko wapi, maana nimeshawai kufanyiwa hivyo nikaongea na wahudumu wenu na wakathibitisha lakn haikurundi hata senti 5. hongereni kwa kufungua uzi wa kujifurahisha. lakn hakuna lolote.
 
Vodacom mnatakiwa kuboresha huduma ya internet Mtwara ..mko nyuma sana! Hasa kwenye simu!
 
Aisee nina note4 nikiweka gsm/wcdma auto connect then nikapigiwa simu mi nawasikia wao hawanisikii na ndio naeza pata internet yenye speed other wise niweke gsm only and simu zinaenda poa ila net inagoma.....tunafanyaje?
 
huduma ya pesa kampuni za simu ziapata faida kubwa sana na hasa ukizingatia mfumo wa kodi wa mdogo kulip zaidi(%ge basis), (vibarua?) mawakala wenu mnawapa kamisheni kidogo sana na ukizingatia walivojazana kila kona! na bado mwisho wa mwezi 10% hukatwa kama kodi! akiweka float anakatwa! kuweni na ubinadamu!
 
Mtujuze sekunde/muda tunaotumiaunaobaki mara tu tumalizapo kuongea.maana huwa na salio langu lililobaki linarambwa kwa kukosa huduma hii
 
Back
Top Bottom