Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Nieona hii katika ukurasa wa habari mchanganyiko.

Hakuna kitu kama hicho!!!

Ile hela ambayo naamini wameichota toka talk time account yangu(elfu ishirini) wala haijarudishwa hadi leo hii , licha ya bla bla nyingi zisizo na msingi toka kwa staff wao.
Tatizo lao wanafikiri wote ni ma-laymen wa mitandao, hivyo kuibiwa at will.

Hapo unawekewa offer kama za hapo juu ambazo ni kama mwanga kwa kumbi kumbi ili muwe wengi wawachote kwa urahisi!
Kuna mtoa mada anasema Voda wameamka sasa, haelezi nani kawaamsha .

Inaelekea tu ni marketing gimmicks za Voda yenyewe baada ya kukabiliwa na bad press ya matukio ya wizi yanayolalamikiwa na wengi.
 
Yameshanikuta hayo mpaka nikasitisha kutumia mtandao huo toka tar 6.01.2014 jana nikaweka vocha ya buku na kujiunga cheka asubuhi nikatumiwa sms kuwa cheka ya mitandao mingine imekwisha wakati sikupiga simu yeyote ile
 
wamepunguza dakika voda kwennda mitandao mingne ila voda kwenye voda kawaida
 
Jana 28 Jan 2014 saa 6:43 mchana nilweka vocha ya sh 500 ktk line yangu ya Voda kwa lengo la kujiunga na Kifurushi chao kipya cha CHEKA BOMBASTIC

Dakika tano baadae nilipotaka kujiunga nilijibiwa kwa sms kuwa salio langu halitoshi

Nilipouliza salo nilijibiwa salio ni Tsh. 477.91

Saa 7:15 nilipiga simu. Kuongea na mhudumu akanijibu ni kweli na kwamba sidaiwi chochote na kwamba baada ya saa tatu marekebisho yatafanyika

Hadi leo saa 7:15 mchana sijatumia line hiyo naangalia salio ni Tsh 439.57
Hii ndiyo staili mpya ya kuibia wateja. Kama si wizi ni nini?
 
Habari chameleon,tafadhali tutumie namba ya simu PM kwa msaada zaidi ndugu mteja,pole.
 
Last edited by a moderator:
kama unatumia smart phone inawezekana simu ilikuwa inachek updates za software kama net app ilikuwa on. so ndo hicho kiasi kilichotumika.
 
Kaka mbona kawaida hiyo Hapo ....kifurushi /package etc ikikata unatakiwa kufunga data connection lazivyo hela yote itakwisha kwasababu hizo appln zilizo on km watsup etc zinakula hela ya ndani ukitumia net au uki open appln kama jamii forum, ni kawaida tuu mkuu sema kuavoid hii ki2 muwe mnaweka package ya mwezi hizi za kila Siku matokea yake pack inakata hujui afu unaendelea tumia internet ndo inapelekea hela yako inatumika
 
Kama wewe ni mtumiaji wa laini ya TIGO jaribu kufanya utafiti huu;

Weka vocha angalau ya Tsh 500 then rekodi salio lako, hakikisha hupigi wala kutuma msg n aukifanya hivyo hakikisha unarekodi salio lako.

Asubuhi ukiamka angalia salio lako kama ni lile lile uliloacha kabla.

Ukipata jibu rudi utujuze.
 
hamia airtel

kwel bwana mie nilishatoka vodacom mapema anasubil nin. Na kuniua kabisa juz nimetoka zangu mbez mwisho nimeenda mliman city kurenew no ya voda iliyopotea kama miez mitano iliyopika pamoja na kuwaonyesha vitambulisho vyangu kazaa et wanataka nikalete passport size, bas hapo ndio ukawa mwisho wangu na hawa jamaa voda.
 
Habari chameleon,tafadhali tutumie namba ya simu PM kwa msaada zaidi ndugu mteja,pole.

Ivi mnakuaga wapi mpaka mnaruhusu UJINGA kama huu?? Mnajua ni watu wangapi mnawapoteza kwa huduma mbaya na KUPANDISHA GHARAMA bila mpangilio?

Kueni makini na huduma zenu bwana au kama mnajiandaa na 2015 mtuambie kabisa na sisi tujue!!! Mnakera sana..
 
Last edited by a moderator:
Ofa Maalumu kwa ajili yako!Ongeza salio la Tsh18000 hadi Jumamosi01/02/2014 na upate Tsh20000 kwa siku 2. Kwa maelezo zaidi ya Ofa Maalumu piga*149*01#
 
Pole sana mkuu, watu wengi wanalalamika kukatwa pesa zao bila kujua, mimi natumia simu isiyo na internet lakini pesa yangu inakatwa bila sababu.

Hata wazazi wangu kijijini wanalalamika. Hawa jamaa kwa wizi wa kijanja hivi lazima watakuwa wanapata si chini ya milioni 100 kwa siku
 
Kama wewe ni mtumiaji wa laini ya TIGO jaribu kufanya utafiti huu;
Weka vocha angalau ya Tsh 500 then rekodi salio lako, hakikisha hupigi wala kutuma msg n aukifanya hivyo hakikisha unarekodi salio lako. Asubuhi ukiamka angalia salio lako kama ni lile lile uliloacha kabla.

Ukipata jibu rudi utujuze.

Ninachotaka ni kujulishwa tu kuwa makato ni ya nini
 
Ofa Maalumu kwa ajili yako!Ongeza salio la Tsh18000 hadi Jumamosi01/02/2014 na upate Tsh20000 kwa siku 2. Kwa maelezo zaidi ya Ofa Maalumu piga*149*01#

Wajinga ndio waliwao If I can spend 18000 airtime in a week why gamble with my money in the pit hole?
Usijaribu kunitoa relini nimeuliza makato niya nini?
 
Habari chameleon,tafadhali tutumie namba ya simu PM kwa msaada zaidi ndugu mteja,pole.

Hivi mnasubiri hadi mtu aje JF" ndiyo mshughulikie tatizo lake, mnajua wangapi hawapo katika hii mitandao ya jamii?

Hii sio "individual case", kila kona watu wanalalamika na uwizi wa aina hii!! Inakera sana mtu anaweka vocha kwa "plan" halafu anakuta imepungua!!
 
Habari chameleon,tafadhali tutumie namba ya simu PM kwa msaada zaidi ndugu mteja,pole.
Asante kwa majibu yenu

Namba yangu itawafaa nini iwapo nimeongea na mhudumu wenu kupitia Na. 100 akashindwa? Na si mnasema simu zote za malalamiko zinarokodiwa? Why dont you go through your records for that matter?

Ninachotaka sio kurudishiwa fedha bali sababu za deductions hizo na muwe fair kwa wateja wote.
Otherways I can't sunbmit my No.here for security reasons
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom