Vodacom Tanzania yadaiwa kutowalipa mawakala wake wa huduma ya kifedha(M-Pesa) kamisheni zao

Hii ni nzuri lakini ni risk hasa ktk mfumo wa sasa wa kucancel miamala[emoji3]
Huo ujinga sifanyi.
Mteja akitaka kutoa elfu 10 makato ni 1400
Natuma 11000 kwenye simu yangu yeye atakatwa 310.
Napata 1,000 iliyosimama.

Habari ya mwisho wa mwezi sina.

Ila hii ni riski
 
Nikweli ila hii unafanya pamoja na biashara nyingine...mteja anakuja anatoa hela ananunua na bidhaa hapo hapo
Miloni 3 ukifanya hata biashara ya mkaa unakunja faida zaidi ya hiyo laki 4 anayolipwa wakala[emoji3]
 
Pamoja na mleta mada kuwa ameshapata malipo yake,naomba kumsaidia ili siku nyingine asije kulalamika. Commission huwa zinalipwa kuanzia tarehe 1-5. Hii ni kwa mitandao yote. Kwa hiyo unaweza kuwasiliana na wakala wako mkuu baada ya tarehe 5 km utakuwa hujapata. Na kwa wale wanaovunjwa moyo kufungua hii biashara msidanganywe,hakuna biashara rahisi na nzuri kufanya km hii ya miamala ya pesa. Kikwazo pekee kwenye hii biashara ni majambazi tu.

Kuna mtu hapo amesema alifanya miamala ya thamani ya milioni 33 na akapata laki 4 na 20. Lkn hajasema mtaji wake ulikuwa bei gani. Unaweza kufanya hata miamala ya thamani ya bilioni 1 Kwa mtaji wa laki 5 na ukapata milioni na nusu kwa mwezi. Hizo ni pesa za wateja wanaokuja ku-depost na ku-withdraw. Nimefanya hiyo biashara tangu mwaka 2011 hadi leo. Pesa zako muda wote zipo Salama,na ni pesa ambayo ukitaka ikusaidie inakusaidia hapohapo. Maana muda wote ama itakuwa kwenye simu au unayo cash. Na wakala ukitaka kutoa pesa zako hukatwi. Hiyo nyumba iliyopo kwenye avatar yangu,nimejenga kwa hiyo biashara. Na nilimvua mtu kwa milioni 14 nikaivunja nikajenga hiyo. Wale mnaotaka kufungua msikatishwe tamaa,karibuni tufanye biashara.
 
Huo ujinga sifanyi.
Mteja akitaka kutoa elfu 10 makato ni 1400
Natuma 11000 kwenye simu yangu yeye atakatwa 310.
Napata 1,000 iliyosimama.

Habari ya mwisho wa mwezi sina.

Ila hii ni riski
Nashukuru kujua tupo wengi....!!mimi nna wateja wangu nnaowajua ndo hua nawafanyia hvyo....!!na sifanyagi kwa mtu nisiyemjua

Sina namba ya wakala ila natoa pesa mitandao yote
 
Katika biashara za kulipwa commission faida huwa inapataikana katika kuwa na 'volume' kubwa. Lakini pamoja na hayo kuna haja ya mawakala kuwa na umoja wenu utakaoweza kuwa na sauti moja ya kusaidia ku'negotiate' na makampuni za simu, kiukweli 'risk' zote za biashara, mtaji na kazi yenyewe ya kufanya hiyo miamala mnaifanya ninyi hivyo kamisheni inapaswa kuwa kubwa kidogo angalau hata 30%. Mkiwa na umoja wenu inawapa sauti yenye nguvu kushinikiza makampuni yaongeze kamisheni, hakuna asiejua na hata ukiangalia taarifa za fedha za kampuni za simu biashara ya pesa ndio inayowapatia faida na inayokuwa pamoja na ya 'data'. Mnaweza kufanya tafiti kuona kenya wanalipaje maana wao ndio wanaongoza duniani kwenye hii nyanja. Lakini yote kwa yote ni lazima uwe na miamala mingi sana ili uone faida. Kama mtumiaji wa huduma hizo ninapokatwa basi nategemea yule anaenihudumia nae anafaidika ili kukuza uchumi wetu.
 
Huu upuuzi wa Mawakala wakuu ndio tatizo. Wakala mkuu anapata zaidi ya Wakala anayepigwa jua. Biashara ya kijinga sana hii
 
Nimesomesha wadogo zangu, nimejenga nyumba, sasa naanza ujenzi dar es salaam kwa kazi hii, nina shamba heka ishirini kwa kazi hii kikubwa hakikisha kila mteja aliyefika kwako kapata huduma siyo kujibu tu mteja sina salio,
Kuna kingine zaidi ya usemacho. Au we wakala mkuu. Ama umemix na business zingne otherwise ni uongo mtakatifu. Wakala?
 
Acha kuingiza watu mkenge kwa maslahi yako. Hiyo ni biashara ya kitumwa kabisa. Unaweza niambia kazi ya wakala mkuu kwa wakala mdogo ni ipi ? Na kwa mini kamisheni yake nikubwa kuliko ya wakala mdogo ambae ndie anatafuta wateja na kurisk pesa zake?
 
Acha kuingiza watu mkenge kwa maslahi yako. Hiyo ni biashara ya kitumwa kabisa. Unaweza niambia kazi ya wakala mkuu kwa wakala mdogo ni ipi ? Na kwa mini kamisheni yake nikubwa kuliko ya wakala mdogo ambae ndie anatafuta wateja na kurisk pesa zake?
Tatizo wewe unakuwa na wivu bila hata kujua kile anachopata unayemuonea wivu. Wakala mkuu anapata 20% ya commission yako wewe. Yaani wewe ukipata laki 1 baada ya kodi ya zuio,wakala mkuu anapata elf 20. Kwa hiyo wakala mkuu anapata km nyie mawakala wake pia mnapata. Msipende kulalamika sana,hii biashara unaweza kuwa na mtaji wa milioni 1 km upo eneo lenye mzunguko Mkubwa wa watu,hiyo milioni inaweza kukuletea zaidi ya milioni kwa mwezi. Hizi biashara zinategemea mzunguko yaani uwe na wateja wa kufanya. Mm nna wastani wa kufanya miamala 90 mpaka 120 kwa siku kwenye tigo. Voda nafanya miamala 25 hadi 40 kwa siku. Airtel 15 hadi 35. Comission,tigo napata laki 9 hadi 1ml. Voda laki 2 na Airtel laki 1 na 20. Mtaji wangu ni milioni moja na nusu. Hebu niambie biashara nyingine ambayo unaweza kupata hiyo faida kwa huo mtaji.
 
Kwahiyo wataka kutuambia kuwa waliosema kwamba commission inayolipwa ni ndogo ni waongo? au sio mawakala? Mfano mtu kaja kaweka sh laki mbili je wakala anapewa commission sh ngapi? Na ikitokea mtu katoa sh laki mbili pia je commission anapewa sh ngapi wakala?
 
Jambo la busara ni kwa mawakala kwa umoja wao wakawa na chama chao chenye nguvu waweze ku negotiate commissions na makampuni ya simu. Vinginevyo, tunafanya kazi kama vibarua wasio na thamani..
 
Hawa wanatetea ni wakala wakuu wanakula bila jasho
 
Nashukuru kujua tupo wengi....!!mimi nna wateja wangu nnaowajua ndo hua nawafanyia hvyo....!!na sifanyagi kwa mtu nisiyemjua

Sina namba ya wakala ila natoa pesa mitandao yote
Yap huwa nafanya hivyo pia mtu nisiyemjua huwa ninanunua vocha moja kwa moja kupitia VODAFASTA OFFICIAL inakuja kwangu kama vocha so hawezi rudisha hii ina 8% zaidi faida
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…