Vodacom Tanzania yapata CEO Mpya, Hisham Hendi raia wa Misri

Hapa hatuongelei kulipa kodi, tunaongela mtu kushika nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji/Mkuregenzi Mkuu (Executive Director) wa kampuni nafasi ambayo binafsi naamini wapo watanzania wenye uwezo wa kushika. Unaposema hakuna Mtanzania mwenye uwezo wa kuongoza kampuni kama Vodacom sisi tueleweje, wakati kuna watanzania wameshawahi kuwa hadi washauri kwenye Benki ya Dunia. Mimi hili sintakubaliana nalo mpaka naingia kaburini.
 

Post tunayoongelea na inayolalamikiwa hapa ni Managing Director ambayo ni Executive Director. Board Chairman ni Non-Executive Director. Kumbuka Pius Msekwa amekuwa Chairman kipindi fulani. Huyu ni Spika wa Bunge wakati huo na ndiyo anapanga policy kama unazozisema.

The Company Act unayotaja haitofautishi kati ya Executive Director na non-Executive director. Inasema tu Directors wawe kuanzia wawili.

Mfumo wa Executive Director na Non Executive Directos ni practice ya kampuni na zinafanya hivyo kampuni zote hapo nchini.

Bahati nzuri umewataja Laurent Mafuru na Deo Mwanyika. Hebu malizia useme sasa hivi wako wapi na waliondokaje huko unakowataja? Ndiyo mantiki ya ninayoyasema humu.
 
Mkuu siyo kila mtanzania ni mbabaishaji. Ubabaishaji uko kwenye utumishi wa umma kwasababu mbalimbali na siasa, kubebana kukiwemo. Lakini kwenye sekta binafsi sidhani kama kuna ubabaishaji kwasababu watu wanaoajiriwa huko wengi wao ni wale wenye uwezo mkubwa sana.

Leo hii mwanasheria wa kampuni la Bakhersa uwezo wake ni lazima uwe mkubwa kuliko yule wa Serikali. Sasa mnaposema kuwa watanzania wote ni wababaishaji mimi sikubaliani kabisa kwasababu nawafahamu Watanzania ambao hawasikiki lakini wana uwezo mkubwa sana kiutendaji.
 

Lakini mkuu hili la Ali Mafuruki kusema kwamba hakuna Mtanzania mwenye uwezo wa kuongoza kampuni kama Vodacom nadhani ni matusi kwa watanzania. Jamani mbona kuna watanzania wana uwezo mkubwa sana kwenye Private Sector na binafsi nawafahamu ?? Hii kauli imeniumiza sana.
 

Kaka Malcom,

Inaelekea unatakiw akusaidia taarifa kadhaa ambazo haunazo. Ni kweli ubabaishaji uko serikalini zaidi. Watzania ni walewale wanaofanya kazi serikalini na private sector.

Tofauti ni kwamba private sekta menejiment inafuatilia kw aukaribu. Hiyvo ninachoweza kusema ni kwamba watanzania wa private sekta wanasukumwa haraka kama kondoo machungani.

Lakini serikalini mchunga kondoo anaishia kuparamia maembe huku kondoo wanajichunga wenyewe. Lakini uvivu ni uleule. Kampuni zinazoanguka nyingi ni zile ambazo zinalegea katika usimamizi na ndiyo hizi zinatangazwa kila siku kufilisika.
 
Labda hii ndiyo iwe sababu, lakini kusema kwamba hakuna Mtanzania mwenye uwezo wa kuongoz kampuni kama Vodacom ni matusi makubwa kwa watanzania. Halikubaliki hata kidogo....
 
Msipende kukimbilia hoja ya kutukanwa pale mnapoambiwa ukweli. Mafuruki alisema wanapata shida kumpata mtanzania wanapotafuta Managing director wa kampuni yoyote hapo nchini.

Sasa, kama kweli watanzania mpo mnaoweza mbona hatujawasikia mkiomba nafasi hiyo. Tueleze mchkato ulikuwa vipi na mmeomba wangapi.

Malalamiko yenu huku mitandaoni msidhani yatawasiaidia. Nimesema na ninarudia. Acheni uvivu. Acheni fitina. Acheni porojo. Acheni majungu. Acheni kuchukia wachapakazi. Acheni kuchukia wabunifu. Acheni kujilimbikizia mali. Acheni kukimbilia 10% kwenye tender.

Labda hii ndiyo iwe sababu, lakini kusema kwamba hakuna Mtanzania mwenye uwezo wa kuongoz kampuni kama Vodacom ni matusi makubwa kwa watanzania. Halikubaliki hata kidogo....
 
Mimi nakubali kabisa kwamba siasa inavuruga utendaji wa nchi na mimi mwenyewe nishawahi kuwa muhanga kwasababu nimeshawahi kupata bahati ya kufanya kazi kwenye hizi Board na nimekaa na baadhi ya viongozi wakubwa tu. Kuna matatizo sana ya ubabaishaji na mimi nakubali kabisa.

Ambacho mimi napinga ndugu yangu ni hii kauli ya Ali Mafuruki kusema hakuna Mtanzania mwenye uwezo wa kuwa Managing Director wa kampuni kama Vodacom. Napinga kwasababu nawafahamu watanzani wengi kwenye Private Sector ambao wako makini sana Ali Mafuruki mwenyewe akiwemo.

Hii kauli haina tofauti na ile ya Raisi Magufuli kututukana watanzania kusema anaomba wataalamu wa ICT kutoka Rwanda. Kuna kauli ambazo mtu unaweza kuzungumza ukafurahi lakini zinawajeruhi watu mioyo yao kama watanzania.
 
Si umeona issue ya museveni na M net wale maboss wa kinyarwanda wako Uganda but wanapeleka data kwao,Museveni kawatimua na bifu ya mpaka inajumlisha na hilo Na ndo hayo ya kufukuzwa wanyarwanda wa MTN uganda
 

Mkuu mbona unanichukulia kama mimi ndiyo naomba hii kazi ?? Mimi nimeridhika na kazi nayofanya. Binafsi miaka ya nyuma nilikuwa ninafikiri hivi hivi na kudharau sana watanzania waliosoma sehemu kama UDSM na MZUMBE, lakini nikaja kufahamu kwamba hii dhambi ya kitukana na kukashifu watanzania wote kisa makosa ya watu wachache inawajeruhi watu wengi sana.

Mkuu kama kufanya kazi nje, nikwambie kwamba siyo wewe peke yako umefanya. Lakini hili la kuwatukana watanzania waliosoma kwamba hawana uwezo au wezi mimi sikubaliani nalo kabisa. Kuna watanzania ni waadilifu sana na wana uwezo.

NB: Kama unadhani kwamba watanzania wote walioko hapa nchini ni wajinga basi sawa, its well and good. Lakini kwangu binafsi nadhani siyo uungwana sana kusema hakuna mtanzania anayeweza kuongoza kampuni kama Vodacom.
 
Sasa kama hzo kampuni za watanzania hazipo huo u-CEO watanzania wanaushikia wapi???

Kama hakuna watanzania wenye kampuni kubwa means hakuna watanzania wanaopata exposure ya kuwa CEO kwenye makampuni makubwa.

Kama unabisha basi wataje watanzania wenye uwezo huo mkubwa unaosema wanaweza kuwa CEO kwenye makampuni makubwa. Taja angalau wa3 kwenye Tele industry

Swala la kulipa kodi limekuja sababu nafikiri ni kigezo sahihi cha kupima uadilifu na uongozi imara wa kampuni.
 
Huyo mtu ni msanii balaa,inaonekana jiwe kamdhibiti kwani mara nyingi analialia
 
Mkuu haujui kuwa misri wametoa pesa za ule mradi mkubwa wa umeme?
 
Ni engineer alikuwa german,kafika hapo ni msaada wa Benja
 
Hivi huyu ana PhD ?
Au ni Engineer wa Telecom?
Sisi tumezoea hivyo banaa!
CC barafu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenye kampuni ninayotafutia riziki zile nafasi za juu zipo ngozi yetu hii yani wana roho mbaya hata shetani ana afadhali,ile sheria ya mh raisi zile nafasi wapewe wazawa kwa kweli iondolewe sio wabunifu na hawajali muwajibikaji no motisha,walioanzisha usemi ngozi kota mbaya hawajakosea,safi Vodacom kwa kutambua hilo ili msonge mbele.

mvujajasho nguli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…