Vodacom Tanzania yapata CEO Mpya, Hisham Hendi raia wa Misri

Vodacom Tanzania yapata CEO Mpya, Hisham Hendi raia wa Misri

Huu mjadala nafikiri unapaswa kujadiliwa kwa mapana na bila hisia. Hiyo ndio njia pekee itakayopelekea kujua hasa chanzo cha tatizo ni nini hasa??

Mara zote zikitoka list ya walipa kodi wakubwa Tanzania huwa kuna majina mengi ya waarabu na wahindi. Je hii inamaanisha wahhindi na waarabu ndio walipa kodi tuu??
Au inamaanisha wahindi na waarabu ndio wako vizuri kwenye usimamizi wa biashara/kampuni??

Tukiwatoa Mzee Mengi na Mzee Massawe ni watanzania gani wengine wanamiliki kampuni kubwa zinazofanya operation karibu sehemu kubwa ya Tanzania?? Kama wapo namba za revenues za kampuni hizo zikoje??

Na je kuna mtanzania anaemiliki kampuni nje ya nchi ambayo revenues zake ni zaidi ya 50m us $??
Hapa hatuongelei kulipa kodi, tunaongela mtu kushika nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji/Mkuregenzi Mkuu (Executive Director) wa kampuni nafasi ambayo binafsi naamini wapo watanzania wenye uwezo wa kushika. Unaposema hakuna Mtanzania mwenye uwezo wa kuongoza kampuni kama Vodacom sisi tueleweje, wakati kuna watanzania wameshawahi kuwa hadi washauri kwenye Benki ya Dunia. Mimi hili sintakubaliana nalo mpaka naingia kaburini.
 
Kisheria Board of Directors ndiyo inahusika kutunga sera zote za uendeshaji wa kampuni kama ambavyo washika hisa wanataka: Kiingereza naweza kusema hivi "The Board of Directors is a Principal Policy Organ of the Company" .

Executive Director ni mtendaji wa kila siku wa shughuli za kampuni akitekeleza sera zote na maelekezo (Policies and Directives) ambazo zimetolewa na Board of Directors. Kikubwa zaidi ni kwamba The Executive Director anawajibika kwa Board of Directors.

Haya siyasemi mimi bali The Companies Act of Tanzania ambayo ni sheria iliyotungwa na bunge ndiyo inasema hivi. Wewe utasemaje naongea siasa ??

Kwenye Organogram ya kampuni yoyote ile The Chairman of the Board yuko juu kuliko The Executive Director. Sasa nauliza huyo Ali Mafuruki anayesema hakuna watanzania wenye uwezo yeye alifikaje hapo juu na kuwa Chairman of the Board.

Halafu kuna watanzania wameongoza makampuni mengi tu zaidi ya Vodacom. Wapo wakina Deo Mwanyika wameongoza makampuni mazito kama BARRICK na ACACIA, wakina Laurent Mafuru ni Certified Bankers wamefanya kazi kwenye mabenki makubwa Uingereza.

Kuna watanzania wengi ambao siwezi kuwataja lakini wanaongoza makampuni makubwa ndani na nje ya nchi. Watafute....

Post tunayoongelea na inayolalamikiwa hapa ni Managing Director ambayo ni Executive Director. Board Chairman ni Non-Executive Director. Kumbuka Pius Msekwa amekuwa Chairman kipindi fulani. Huyu ni Spika wa Bunge wakati huo na ndiyo anapanga policy kama unazozisema.

The Company Act unayotaja haitofautishi kati ya Executive Director na non-Executive director. Inasema tu Directors wawe kuanzia wawili.

Mfumo wa Executive Director na Non Executive Directos ni practice ya kampuni na zinafanya hivyo kampuni zote hapo nchini.

Bahati nzuri umewataja Laurent Mafuru na Deo Mwanyika. Hebu malizia useme sasa hivi wako wapi na waliondokaje huko unakowataja? Ndiyo mantiki ya ninayoyasema humu.
 
Watanzania Hatuko serious na kazi hatuko smart visingizio kibao kazini mala nimefiwa mala mama anaumwa mala mtoto wangu kafukuzwa ada yote hayo ni matatizo ambayo yanatufanya tuendelee kuwa chini..

Stupidity ya kuwekeza akili zetu nyingi kwenye mambo ya siasa Mapenzi na kufatiliana maisha ndio shida inapokuja tunakosa sifa kwenye mambo mengi ya kibishara ..

Tuwe wakweli Makampuni yanataka watu ambao sio tu wamesoma sana shule no ila wako mentally fit.

Sio unamwajiri mtu kila siku yuko busy kusuruhisha matatizo ya ndoa yake ..

Kampuni kama Vodacom haiwezi kuchukua mtu kama uyo awe mtendaji mkuu.

Tutaendelea kuwa na wahindi warabu na wazungu kibao maana wako na nidhamu ya kazi.
Mkuu siyo kila mtanzania ni mbabaishaji. Ubabaishaji uko kwenye utumishi wa umma kwasababu mbalimbali na siasa, kubebana kukiwemo. Lakini kwenye sekta binafsi sidhani kama kuna ubabaishaji kwasababu watu wanaoajiriwa huko wengi wao ni wale wenye uwezo mkubwa sana.

Leo hii mwanasheria wa kampuni la Bakhersa uwezo wake ni lazima uwe mkubwa kuliko yule wa Serikali. Sasa mnaposema kuwa watanzania wote ni wababaishaji mimi sikubaliani kabisa kwasababu nawafahamu Watanzania ambao hawasikiki lakini wana uwezo mkubwa sana kiutendaji.
 
Issue sio kwamba kampuni ni yetu au sio yetu bali ni kampuni inayofanya kazi Tanzania! Bila kujali inamilikiwa na nani, huwezi kupuuza ajira walizonazo Watanzania kutoka Vodacom! Huwezi kupuuza kodi inayolipwa na Vodacom!!! Huwezi kupuuza biashara kadhaa zinazotokana na uwepo wa Vodacom! Lakini kubwa zaidi, huwezi kupuuza kwamba Vodacom ipo listed Dar es salaam Stock Exchange na kwahiyo kuna maelfu ya Watanzania wenye hisa zao Vodacom kupitia 25% ya hisa ambazo ziliingizwa sokoni!

Lakini pamoja na hayo, Rostam Aziz alikuwa anamiliki zaidi ya 25% ya hisa za Vodacom ambazo iliripotiwa aliziuza au yupo njiani kuziuza baada ya kukubaliwa na mamlaka! You never know, labda mnunuzi au wanunuzi wa hizo 25+% ya hisa za Rostam ni pamoja na Watanzania!!!

So, kampuni kama hiyo huwezi kusema awe Mkenya au Mzulu, it doesn't matter kwa sababu Vodacom ni ya SA!!!

Lakini mkuu hili la Ali Mafuruki kusema kwamba hakuna Mtanzania mwenye uwezo wa kuongoza kampuni kama Vodacom nadhani ni matusi kwa watanzania. Jamani mbona kuna watanzania wana uwezo mkubwa sana kwenye Private Sector na binafsi nawafahamu ?? Hii kauli imeniumiza sana.
 
Mkuu siyo kila mtanzania ni mbabaishaji. Ubabaishaji uko kwenye utumishi wa umma kwasababu mbalimbali na siasa, kubebana kukiwemo. Lakini kwenye sekta binafsi sidhani kama kuna ubabaishaji kwasababu watu wanaoajiriwa huko wengi wao ni wale wenye uwezo mkubwa sana.

Leo hii mwanasheria wa kampuni la Bakhersa uwezo wake ni lazima uwe mkubwa kuliko yule wa Serikali. Sasa mnaposema kuwa watanzania wote ni wababaishaji mimi sikubaliani kabisa kwasababu nawafahamu Watanzania ambao hawasikiki lakini wana uwezo mkubwa sana kiutendaji.

Kaka Malcom,

Inaelekea unatakiw akusaidia taarifa kadhaa ambazo haunazo. Ni kweli ubabaishaji uko serikalini zaidi. Watzania ni walewale wanaofanya kazi serikalini na private sector.

Tofauti ni kwamba private sekta menejiment inafuatilia kw aukaribu. Hiyvo ninachoweza kusema ni kwamba watanzania wa private sekta wanasukumwa haraka kama kondoo machungani.

Lakini serikalini mchunga kondoo anaishia kuparamia maembe huku kondoo wanajichunga wenyewe. Lakini uvivu ni uleule. Kampuni zinazoanguka nyingi ni zile ambazo zinalegea katika usimamizi na ndiyo hizi zinatangazwa kila siku kufilisika.
 
Sabab ya kuwa kuna watanzania wanaweza kuwa MDs wa kampuni kubwa kama Vodacom na nyinginezo ilkuwa n sabab tu ya kumkataa Mkenya.....hawa jamaa(wakenya) wapo vzur sana kweny Economic Espionage....amini kwamba yule mama alkuwa anakuja kuiua Vodacom na kuireplace Safaricom Tanzania

Taasisi zote za kibiashara za Tanzania zilizowahi kuingia ubia na Kenyan Firms ziliishia pabaya, anza na General Tyre vs Yana Tyre, SBL vs EABL, njoo kwa Precision ilivyokuwa inang'aa mpaka CCM wakataka kuipa hadhi ya Shirika la ndege la Taufa kwa ATCL kuinunua Hisa za Precision.....

Sasa hiv kuna kampuni ya chai kule mufindi na Njombe iliyokuwa ikijulikan kama Rift Valley Tea Company(ina kampuni tanzu 5 za chai) imenunuliwa na wakenya DL Group lkn wanachofanya n dhahir kabisa wana plan ya kuua zile plabtations ili kuimarisha viplot vyao vya chai Kenya. Hawajafanya investment yyte zaid ya kuuza properties walizozikuta na kukata miti kwa wingi mno kuuza magogo ...miti waliyoikuta imepandwa ili kuendeleza uoto wa kieneo kwa ustawi wa chai na vyanzo vya maji.

Yule mama angepewa Vodacom, tungekuwa tunaongea mengine muda huu!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Labda hii ndiyo iwe sababu, lakini kusema kwamba hakuna Mtanzania mwenye uwezo wa kuongoz kampuni kama Vodacom ni matusi makubwa kwa watanzania. Halikubaliki hata kidogo....
 
Msipende kukimbilia hoja ya kutukanwa pale mnapoambiwa ukweli. Mafuruki alisema wanapata shida kumpata mtanzania wanapotafuta Managing director wa kampuni yoyote hapo nchini.

Sasa, kama kweli watanzania mpo mnaoweza mbona hatujawasikia mkiomba nafasi hiyo. Tueleze mchkato ulikuwa vipi na mmeomba wangapi.

Malalamiko yenu huku mitandaoni msidhani yatawasiaidia. Nimesema na ninarudia. Acheni uvivu. Acheni fitina. Acheni porojo. Acheni majungu. Acheni kuchukia wachapakazi. Acheni kuchukia wabunifu. Acheni kujilimbikizia mali. Acheni kukimbilia 10% kwenye tender.

Labda hii ndiyo iwe sababu, lakini kusema kwamba hakuna Mtanzania mwenye uwezo wa kuongoz kampuni kama Vodacom ni matusi makubwa kwa watanzania. Halikubaliki hata kidogo....
Lakini mkuu hili la Ali Mafuruki kusema kwamba hakuna Mtanzania mwenye uwezo wa kuongoza kampuni kama Vodacom nadhani ni matusi kwa watanzania. Jamani mbona kuna watanzania wana uwezo mkubwa sana kwenye Private Sector na binafsi nawafahamu ?? Hii kauli imeniumiza sana.
 
Kaka Malcom,

Inaelekea unatakiw akusaidia taarifa kadhaa ambazo haunazo. Ni kweli ubabaishaji uko serikalini zaidi. Watzania ni walewale wanaofanya kazi serikalini na private sector.

Tofauti ni kwamba private sekta menejiment inafuatilia kw aukaribu. Hiyvo ninachoweza kusema ni kwamba watanzania wa private sekta wanasukumwa haraka kama kondoo machungani.

Lakini serikalini mchunga kondoo anaishia kuparamia maembe huku kondoo wanajichunga wenyewe. Lakini uvivu ni uleule. Kampuni zinazoanguka nyingi ni zile ambazo zinalegea katika usimamizi na ndiyo hizi zinatangazwa kila siku kufilisika.
Mimi nakubali kabisa kwamba siasa inavuruga utendaji wa nchi na mimi mwenyewe nishawahi kuwa muhanga kwasababu nimeshawahi kupata bahati ya kufanya kazi kwenye hizi Board na nimekaa na baadhi ya viongozi wakubwa tu. Kuna matatizo sana ya ubabaishaji na mimi nakubali kabisa.

Ambacho mimi napinga ndugu yangu ni hii kauli ya Ali Mafuruki kusema hakuna Mtanzania mwenye uwezo wa kuwa Managing Director wa kampuni kama Vodacom. Napinga kwasababu nawafahamu watanzani wengi kwenye Private Sector ambao wako makini sana Ali Mafuruki mwenyewe akiwemo.

Hii kauli haina tofauti na ile ya Raisi Magufuli kututukana watanzania kusema anaomba wataalamu wa ICT kutoka Rwanda. Kuna kauli ambazo mtu unaweza kuzungumza ukafurahi lakini zinawajeruhi watu mioyo yao kama watanzania.
 
Suala LA Dada wa Kenya,na msuguano wa Kenya na TZ,ni kubwa kuliko unavyolifahamu,
Kwanza hatuna Vita ya kiuchumi kati yetu na Misri,tuna vita ya kiuchumi kati yetu na Kenya,unajua kilichotokea kwenye kiwanda cha General Tyre?watu waliingia pale kijasusi,wakashika uongozi,wakahujumu kiwanda,kikafa,mitambo ikahamishiwa Kenya,sasa HV ni Yana,sio General tyre tena,
Ukiruhusu kampuni kubwa kama Vodacom,iwe na CEO kutoka nchi,ambayo,MNA ugomvi nayo wa kiuchumi,ikihujumiwa uchumi wa nchi utayumba balaa,
Hivi vitu ni vikubwa sana.Kuna CEO wa Huawei,mchina,kashikwa kule CANADA,na USA inataka apelekwe USA,akashitakiwe kwa wizi wa tekinolojia,China na USA ni wapinzani kwenye uchumi,ukilala umeliwa.
Uwezi kusikia USA,imegombana na India,wakati wahandisi na madakitari kibao kutoka India wanafsnya kazi kwenye vitengo nyeti pale USA.
Hatuna shida na Zambia,watu wake wamejaa Tazara,hatuna shida na SA,wala Uganda,lakini Kenya,tuna shida nao sana,wakipata nafasi,wanaweza kuifanya nchi hii soko LA bidhaa zao.
Unakumbuka ishu ya vifaranga?
Nashukuru Maghufuri kwenye vita ya kiuchumi,ameiwezea sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Si umeona issue ya museveni na M net wale maboss wa kinyarwanda wako Uganda but wanapeleka data kwao,Museveni kawatimua na bifu ya mpaka inajumlisha na hilo
Suala LA Dada wa Kenya,na msuguano wa Kenya na TZ,ni kubwa kuliko unavyolifahamu,
Kwanza hatuna Vita ya kiuchumi kati yetu na Misri,tuna vita ya kiuchumi kati yetu na Kenya,unajua kilichotokea kwenye kiwanda cha General Tyre?watu waliingia pale kijasusi,wakashika uongozi,wakahujumu kiwanda,kikafa,mitambo ikahamishiwa Kenya,sasa HV ni Yana,sio General tyre tena,
Ukiruhusu kampuni kubwa kama Vodacom,iwe na CEO kutoka nchi,ambayo,MNA ugomvi nayo wa kiuchumi,ikihujumiwa uchumi wa nchi utayumba balaa,
Hivi vitu ni vikubwa sana.Kuna CEO wa Huawei,mchina,kashikwa kule CANADA,na USA inataka apelekwe USA,akashitakiwe kwa wizi wa tekinolojia,China na USA ni wapinzani kwenye uchumi,ukilala umeliwa.
Uwezi kusikia USA,imegombana na India,wakati wahandisi na madakitari kibao kutoka India wanafsnya kazi kwenye vitengo nyeti pale USA.
Hatuna shida na Zambia,watu wake wamejaa Tazara,hatuna shida na SA,wala Uganda,lakini Kenya,tuna shida nao sana,wakipata nafasi,wanaweza kuifanya nchi hii soko LA bidhaa zao.
Unakumbuka ishu ya vifaranga?
Nashukuru Maghufuri kwenye vita ya kiuchumi,ameiwezea sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Na ndo hayo ya kufukuzwa wanyarwanda wa MTN uganda
 
Msipende kukimbilia hoja ya kutukanwa pale mnapoambiwa ukweli. Mafuruki alisema wanapata shida kumpata mtanzania wanapotafuta Managing director wa kampuni yoyote hapo nchini.

Sasa, kama kweli watanzania mpo mnaoweza mbona hatujawasikia mkiomba nafasi hiyo. Tueleze mchkato ulikuwa vipi na mmeomba wangapi.

Malalamiko yenu huku mitandaoni msidhani yatawasiaidia. Nimesema na ninarudia. Acheni uvivu. Acheni fitina. Acheni porojo. Acheni majungu. Acheni kuchukia wachapakazi. Acheni kuchukia wabunifu. Acheni kujilimbikizia mali. Acheni kukimbilia 10% kwenye tender.

Mkuu mbona unanichukulia kama mimi ndiyo naomba hii kazi ?? Mimi nimeridhika na kazi nayofanya. Binafsi miaka ya nyuma nilikuwa ninafikiri hivi hivi na kudharau sana watanzania waliosoma sehemu kama UDSM na MZUMBE, lakini nikaja kufahamu kwamba hii dhambi ya kitukana na kukashifu watanzania wote kisa makosa ya watu wachache inawajeruhi watu wengi sana.

Mkuu kama kufanya kazi nje, nikwambie kwamba siyo wewe peke yako umefanya. Lakini hili la kuwatukana watanzania waliosoma kwamba hawana uwezo au wezi mimi sikubaliani nalo kabisa. Kuna watanzania ni waadilifu sana na wana uwezo.

NB: Kama unadhani kwamba watanzania wote walioko hapa nchini ni wajinga basi sawa, its well and good. Lakini kwangu binafsi nadhani siyo uungwana sana kusema hakuna mtanzania anayeweza kuongoza kampuni kama Vodacom.
 
Hapa hatuongelei kulipa kodi, tunaongela mtu kushika nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji/Mkuregenzi Mkuu (Executive Director) wa kampuni nafasi ambayo binafsi naamini wapo watanzania wenye uwezo wa kushika. Unaposema hakuna Mtanzania mwenye uwezo wa kuongoza kampuni kama Vodacom sisi tueleweje, wakati kuna watanzania wameshawahi kuwa hadi washauri kwenye Benki ya Dunia. Mimi hili sintakubaliana nalo mpaka naingia kaburini.
Sasa kama hzo kampuni za watanzania hazipo huo u-CEO watanzania wanaushikia wapi???

Kama hakuna watanzania wenye kampuni kubwa means hakuna watanzania wanaopata exposure ya kuwa CEO kwenye makampuni makubwa.

Kama unabisha basi wataje watanzania wenye uwezo huo mkubwa unaosema wanaweza kuwa CEO kwenye makampuni makubwa. Taja angalau wa3 kwenye Tele industry

Swala la kulipa kodi limekuja sababu nafikiri ni kigezo sahihi cha kupima uadilifu na uongozi imara wa kampuni.
 
Ali Mafuruki mwenyewe alisema hakuna mtanzania anayeweza kuongoza kampuni kama VODACOM. Katika hili tumuunge mkono. Kuna watanzania wamo VODACOM tangu imeanzishwa yaani wana miaka 19 sasa ndani ya VODACOM.

Hawa wana kazi ya kutueleza VODACOM waliitumia vipi kukuza ujuzi wao kuiongoza. Je walipanda (ku-grow) kimaisha au walipnada kiujuzi.
Huyo mtu ni msanii balaa,inaonekana jiwe kamdhibiti kwani mara nyingi analialia
 
Mimi ni Mtanzania ninayependa kuangalia mambo objectively. Siyo bendera kufuata upepo. Nakubaliana na wewe. Huu ni ujinga uliokithiri. Syvia wa Kenya alibaguliwa kwa sababu ya ngozi yake. Ni bora angebaguliwa na Wazungu. Hili la kubaguliwa na Weusi wenzie linasikitisha sana. Kama kweli walimaanisha kuwa kuna Watanzania wenye uwezo wa kuongoza Vodacom kwa nini wametuletea raia wa Misri? Aliyempa kibali Mmisri hakukumbuka kuwa alimnyima kibali Mkenya? Umoja wetu wa EAC uko wapi?
Mkuu haujui kuwa misri wametoa pesa za ule mradi mkubwa wa umeme?
 
Kama Ali Mafuruki alisema hivyo basi ni mtu mwenye kiburi sana na mwenye roho ya majivuno. Yeye awe mwenyekiti wa Board ya Vodacom halafu asema hakuna watanzania wanaoweza kuongoza kampuni kama Vodacom kweli: Yeye anajitoa kwenye orodha ya watanzania ??

Hivi ni mtu wa wapi huyu Ali Mafuruki, maana kuna siku nilimsikiliza kwenye TED Talks nikajua anaongea kwa kutaka kurekebisha kumbe ni uzandiki na kiburi.

This is too bad and disappointing....

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni engineer alikuwa german,kafika hapo ni msaada wa Benja
 
View attachment 1054930
Waafrika alieturoga alituweza sana.

Mwaka jana Vodacom ikateua raia mwanamama mmoja kutoka Kenya kuja kua mkurugenzi wake, maneno yakawa maneno kua kwani tumekosa mtanzania wa kushika hizo nafasi na mambo kede kede, serikali ikamnyima kibali cha kazi. Dada wa watu akaendelea na maisha yake huko kwao Kenya.

Sasa Vodacom wameteua mwarabu kutoka Misri kua mkurugenzi wake, zile kelele za mwaka jana hazisikiki tena, maana yake hatutaki waafrika wenzetu ila tunataka watu wenye ngozi nyeupe. Kwanza tunaweza kumnyima mkenya kibali cha kufanya kazi Tanzania ila tukampa mwarabu wa Misri, sijui akili za wapi hizi.

Kwa hiyo ikifika kwa ngozi nyeupe hadithi za wazawa zinakufa, ila ikiwa ni mweusi mwenzetu hadithi za wazawa wapewe fursa ndio zinaibuka.

Binafsi hua sikubaliani na hoja ya uzawa, kwenye ulimwengu ulioendelea watu wenye uwezo binafsi wanataftwa kutoka kila mahali wakafanye mabadiliko na kuongoza taasisi za nchi nyingine. Uingereza ilimkodi Gavana wa benki ya Canada ili awe Gavana wao awasaidie kurekebisha uchumi, mkuu wa Google ni mhindi na mifano iko mingi.

Hoja yangu ni kwamba, kwa nini mkenya tulimkatalia kwa hoja ya uzawa alafu tumekubali mwarabu wa Misri?
Hivi huyu ana PhD ?
Au ni Engineer wa Telecom?
Sisi tumezoea hivyo banaa!
CC barafu

Kwenye kampuni ninayotafutia riziki zile nafasi za juu zipo ngozi yetu hii yani wana roho mbaya hata shetani ana afadhali,ile sheria ya mh raisi zile nafasi wapewe wazawa kwa kweli iondolewe sio wabunifu na hawajali muwajibikaji no motisha,walioanzisha usemi ngozi kota mbaya hawajakosea,safi Vodacom kwa kutambua hilo ili msonge mbele.

mvujajasho nguli
 
Back
Top Bottom