Vodacom Tanzania yapata CEO Mpya, Hisham Hendi raia wa Misri

Vodacom Tanzania yapata CEO Mpya, Hisham Hendi raia wa Misri

Hapa hatuongelei kulipa kodi, tunaongela mtu kushika nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji/Mkuregenzi Mkuu (Executive Director) wa kampuni nafasi ambayo binafsi naamini wapo watanzania wenye uwezo wa kushika. Unaposema hakuna Mtanzania mwenye uwezo wa kuongoza kampuni kama Vodacom sisi tueleweje, wakati kuna watanzania wameshawahi kuwa hadi washauri kwenye Benki ya Dunia. Mimi hili sintakubaliana nalo mpaka naingia kaburini.
Nimekuelewa sana Kiongozi lakini maelezo yangu hayakutokana na hoja ya kutokuwa na Mtanzania mwenye sifa. Hoja yangu ilikuwa inajibu hoja ya huyo mdau aliyesema hata kama CEO angekuwa Mtanzania haina maana yoyote katika mazingira ambayo Vodacom yenyewe sio mali ya Tanzania. Ni kutokana na hoja yake hiyo ndo maana nikamweleza hata kama Vodacom TZ ni subsidiary ya Vodacom Group SA lakini umuhimu wake kwa Tanzania ni mkubwa sana na hivyo kuonesha ni namna nafasi za juu kwa kampuni kama hiyo inapaswa kwenda kwa mtu mwenye maslahi na Tanzania (kwa maana Mtanzania), na kama ni mgeni basi asiwe ni mgeni ambae nchi yake ina mgongano wa maslahi ya kiuchumi na Tanzania. Na ingawaje sijaona waliposema hakuna Mtanzania mwenye sifa lakini suala la kumteua mgeni linaashiria hivyo. Kwa maana nyingine, nakubaliana na wewe kwamba suala la kusema hakuna Mtanzania ni tusi kwa nchi yetu.

Lakini kuna hoja hapa inaongelewa sana na watu kwamba yule Mkenya angekuja kuiua Vodocom! Nakubaliana na wale wanaosema Kenya ni mshindani wake na wale wanaweza kufanya lolote kutuhujumu! Hata hivyo, kwa yule dada siamini hata kidogo kwamba eti angekuja kuihujumu Vodacom kwa sababu yule dada alitoka SafariCom,.Nasema sio rahisi kwa sababu Vodacom Tanzania na Safaricom ni wajukuu wa babu na bibi mmoja; Vodafone UK. Sitaki kuamini kwamba Safaricom wanaweza kuleta mtu wa kuiua Vodacom halafu awaache airtel, tigo na halotel wakila kuku kwa mrija! Niliunga mkono suala la yule dada kuwekewa figisu figisu kwa sababu tu naamini wapo Watanzania ambao wangeweza kushika hiyo nafasi lakini sio kwa hoja ya hofu ya hujuma! Kama ni hujuma basi labda hujuma ya kuua mitandao mingine lakini sio Vodacom!

Lakini tukija kwenye suala la huyo Muarabu nadhani serikali imeshindwa kufanya figisu figisu kwa sababu unlike yule dada wa Kenya, huyo Mwarabu alikuwa pale Vodacom na kwahiyo zile figisu za work permit zisingewezekana kwa huyo jamaa! Kwahiyo serikali wakita kuendeleza zile figisu za awali basi ni kumnyima kibali jamaa mara kibali chake cha sasa kitakapoisha! Lakini swali linalofuata, je kule juu kuna Watanzania wanaoandaliwa kuchukua top positions? Nadhani hapa ndipo tunapofeli! Kama tunasema haiwezekani ceo atoke nje lakini hatujali ikiwa chini ya ceo kuna Watanzania wenye sifa, basi siku ceo mmoja akitoka tutajikuta ni kweli hakuna mtanzania mwenye sifa kwa sababu hawakuwa groomed earlier! Na sidhani kama tunaweza kuwalazimisha wachukue ceo nje ya Vodacom wakati kuna watu ndani ya Vodacom wenye sifa hata kama ni wageni! Yule dada wa Kenya walimleta kwa sababu ni "Vodacom mwenzao"!!
 
Post tunayoongelea na inayolalamikiwa hapa ni Managing Director ambayo ni Executive Director. Board Chairman ni Non-Executive Director. Kumbuka Pius Msekwa amekuwa Chairman kipindi fulani. Huyu ni Spika wa Bunge wakati huo na ndiyo anapanga policy kama unazozisema.

The Company Act unayotaja haitofautishi kati ya Executive Director na non-Executive director. Inasema tu Directors wawe kuanzia wawili.

Mfumo wa Executive Director na Non Executive Directos ni practice ya kampuni na zinafanya hivyo kampuni zote hapo nchini.

Bahati nzuri umewataja Laurent Mafuru na Deo Mwanyika. Hebu malizia useme sasa hivi wako wapi na waliondokaje huko unakowataja? Ndiyo mantiki ya ninayoyasema humu.

Mkuu mimi hapa wala sitaki kubishana nataka tuwekane sana na kufukia makubaliano ya kiungwana. Nafasi ya Director kwenye Companies Act imetajwa kabisa na imesema dhahiri kwamba Director anaweza kuitwa jina lolote kutokana na nafasi yake aliyonayo.

Kwenye Interpretation Section kule juu wamesema hivi "A director includes any person occupying a position of a director by whatever name called"

Tofauti kidogo na ulichosema hapo juu, Companies Act imesema dhahiri kabisa na kutenganisha kazi za Board Members na zile za Director hadi kufikia hatua ya kusema kwamba atawajibika kwa Board huku akiwa ndiyo mtendaji mkuu wa shughuli za kila siku za kampuni.

NB 1: Hayo mengine ya Vodacom yako kwenye Memorandum na Articles of Association na wala hayanihusu. Lakini nitakachokikataa mpaka naingia kaburini ni kutaka kusema nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi siyo mtu mzito kwenye kampuni kisa tu yeye siyo mtendaji kama alivyo Mkurugenzi.

NB 2: Kama Mkurugenzi anawajibika kwenye Board ambayo inaongozwa na Mwenyekiti, huyu Mafuruki atasemaje hakuna Mtanzania mwenye uwezo wa kuongoza hiyo kampuni ?

NB 3: Halafu kitu kingine ambacho sikuelewi ni kutaka kusema kwamba Chairman of the Board hana umuhimu na ni nafasi ambayo inaweza ikajazwa tu kirahisi.

NB 4: Kuondolewa kwa Laurent Mafuru na Deo Mwanyika kisiasa na watawala wa nchi hii hakumaanishi kwamba hakuna watanzania ambao hawana uwezo wa kuongoza kampuni kama Vodacom.
 
Mufuruki ni Mhaya na mhaya na majivuno+dharau ndio mahala pake, haiwezekan kwenye Watanzania zaidi ya mili. 50 eti hakuna Mtanzania mwenye uwezo wa kuongoza Vodacom, kina Mwanyika wasingekubalika kushika zile nafasi ACCASIA au nao sio Watz

Sent using Jamii Forums mobile app
Ww unalinganisha accasia na vodacom. Two difference companies zinazofanya kazi za tofauti kabisa.
Halaf usiwapangie vodacom wamuajri nani maana si kampun ya serikal ni binafsi. Na wananchi wana 25% ya hisa tu ambazo kisheria haziwapi nguv ya kufanya maamuz ndani ya vodacom.

Kampuni kubwa inatafuta Top ambae ana experience na telecom companies. Ndio maana viongoz wake wengi huko nyuma walishaongoza kwenye baadhi ya kampuni za simu. So wanajua nn cha kufanya wenye telecom industry.

Kama wako watanzania ambao wanadhani wana uwezo. Kwann hawaja apply.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata kama nafasi za Board Memebrs na Directors zingetangazwa au zilitangazwa hawa wapiiga kelele wasingeweza kuomba wanajijua hawafai, wanafaa kutumwatumwa na si kuongoza kampuni.

Tatizo la taifa kuwa YESMAN kwa kila kitu ni hili. Unatumika kumridhisha bosi wako matokeo yake unajiondolea uwezo wa kuwa creative.

Endeleeni kuongozwa na vitoto vilivyoanza kazi juzi vikitokea Uingereza, MIsri, Uganda nk.
Siasa zinaharibia watu cv. Wakishaona ulishafanya maamamuzi ya kijinga kwenye cheo fulani. Hata interview hawakuiti

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kisheria Board of Directors ndiyo inahusika kutunga sera zote za uendeshaji wa kampuni kama ambavyo washika hisa wanataka: Kiingereza naweza kusema hivi "The Board of Directors is a Principal Policy Organ of the Company" .

Executive Director ni mtendaji wa kila siku wa shughuli za kampuni akitekeleza sera zote na maelekezo (Policies and Directives) ambazo zimetolewa na Board of Directors. Kikubwa zaidi ni kwamba The Executive Director anawajibika kwa Board of Directors.

Haya siyasemi mimi bali The Companies Act of Tanzania ambayo ni sheria iliyotungwa na bunge ndiyo inasema hivi. Wewe utasemaje naongea siasa ??

Kwenye Organogram ya kampuni yoyote ile The Chairman of the Board yuko juu kuliko The Executive Director. Sasa nauliza huyo Ali Mafuruki anayesema hakuna watanzania wenye uwezo yeye alifikaje hapo juu na kuwa Chairman of the Board.

Halafu kuna watanzania wameongoza makampuni mengi tu zaidi ya Vodacom. Wapo wakina Deo Mwanyika wameongoza makampuni mazito kama BARRICK na ACACIA, wakina Laurent Mafuru ni Certified Bankers wamefanya kazi kwenye mabenki makubwa Uingereza.

Kuna watanzania wengi ambao siwezi kuwataja lakini wanaongoza makampuni makubwa ndani na nje ya nchi. Watafute....
Kaka nikurekebishe kidogo. Hao ulio wataja kuwa wameongoza ACACIA..BANKS.. wanauzoefu na telecom companies ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama Ali Mafuruki alisema hivyo basi ni mtu mwenye kiburi sana na mwenye roho ya majivuno. Yeye awe mwenyekiti wa Board ya Vodacom halafu asema hakuna watanzania wanaoweza kuongoza kampuni kama Vodacom kweli: Yeye anajitoa kwenye orodha ya watanzania ??

Hivi ni mtu wa wapi huyu Ali Mafuruki, maana kuna siku nilimsikiliza kwenye TED Talks nikajua anaongea kwa kutaka kurekebisha kumbe ni uzandiki na kiburi.

This is too bad and disappointing....

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni MTU wa kwenu kagera Mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenye TED talks alizungumza vizuri hasa kwenye AFRICAN RISING , alipinga kwa hoja na Mimi nilimuelewa na anatumika sana kwenye hyo presentation yake kwenye mijadala mingi nje ya afrika na ndan
Kama Ali Mafuruki alisema hivyo basi ni mtu mwenye kiburi sana na mwenye roho ya majivuno. Yeye awe mwenyekiti wa Board ya Vodacom halafu asema hakuna watanzania wanaoweza kuongoza kampuni kama Vodacom kweli: Yeye anajitoa kwenye orodha ya watanzania ??

Hivi ni mtu wa wapi huyu Ali Mafuruki, maana kuna siku nilimsikiliza kwenye TED Talks nikajua anaongea kwa kutaka kurekebisha kumbe ni uzandiki na kiburi.

This is too bad and disappointing....

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa kama hzo kampuni za watanzania hazipo huo u-CEO watanzania wanaushikia wapi???

Kama hakuna watanzania wenye kampuni kubwa means hakuna watanzania wanaopata exposure ya kuwa CEO kwenye makampuni makubwa.

Kama unabisha basi wataje watanzania wenye uwezo huo mkubwa unaosema wanaweza kuwa CEO kwenye makampuni makubwa. Taja angalau wa3 kwenye Tele industry

Swala la kulipa kodi limekuja sababu nafikiri ni kigezo sahihi cha kupima uadilifu na uongozi imara wa kampuni.

Mkuu mimi sitabishana na wewe, pia sitataka kutaja majina ya watu ambao hawafahamiki mbele ya hadhara. Lakini ntakupa mfano mmoja mzuri tu wa hukohuko Vodacom. Kulikuwa na watanzania kama wakina Kevin Twisa ambao nadhani ni vijana wenye uwezo mzuri sana kwenye mambo ya Telecom.

Unaposema kwamba watanzania hawana uwezo kisa hawamiliki makampuni binafsi au ukwasi mkubwa mimi hili sitalikubali hadi naingia kaburini.

Uwe na siku njema mkuu, ahsante.
 
Nimekuelewa sana Kiongozi lakini maelezo yangu hayakutokana na hoja ya kutokuwa na Mtanzania mwenye sifa. Hoja yangu ilikuwa inajibu hoja ya huyo mdau aliyesema hata kama CEO angekuwa Mtanzania haina maana yoyote katika mazingira ambayo Vodacom yenyewe sio mali ya Tanzania. Ni kutokana na hoja yake hiyo ndo maana nikamweleza hata kama Vodacom TZ ni subsidiary ya Vodacom Group SA lakini umuhimu wake kwa Tanzania ni mkubwa sana na hivyo kuonesha ni namna nafasi za juu kwa kampuni kama hiyo inapaswa kwenda kwa mtu mwenye maslahi na Tanzania (kwa maana Mtanzania), na kama ni mgeni basi asiwe ni mgeni ambae nchi yake ina mgongano wa maslahi ya kiuchumi na Tanzania. Na ingawaje sijaona waliposema hakuna Mtanzania mwenye sifa lakini suala la kumteua mgeni linaashiria hivyo. Kwa maana nyingine, nakubaliana na wewe kwamba suala la kusema hakuna Mtanzania ni tusi kwa nchi yetu.

Lakini kuna hoja hapa inaongelewa sana na watu kwamba yule Mkenya angekuja kuiua Vodocom! Nakubaliana na wale wanaosema Kenya ni mshindani wake na wale wanaweza kufanya lolote kutuhujumu! Hata hivyo, kwa yule dada siamini hata kidogo kwamba eti angekuja kuihujumu Vodacom kwa sababu yule dada alitoka SafariCom,.Nasema sio rahisi kwa sababu Vodacom Tanzania na Safaricom ni wajukuu wa babu na bibi mmoja; Vodafone UK. Sitaki kuamini kwamba Safaricom wanaweza kuleta mtu wa kuiua Vodacom halafu awaache airtel, tigo na halotel wakila kuku kwa mrija! Niliunga mkono suala la yule dada kuwekewa figisu figisu kwa sababu tu naamini wapo Watanzania ambao wangeweza kushika hiyo nafasi lakini sio kwa hoja ya hofu ya hujuma! Kama ni hujuma basi labda hujuma ya kuua mitandao mingine lakini sio Vodacom!

Lakini tukija kwenye suala la huyo Muarabu nadhani serikali imeshindwa kufanya figisu figisu kwa sababu unlike yule dada wa Kenya, huyo Mwarabu alikuwa pale Vodacom na kwahiyo zile figisu za work permit zisingewezekana kwa huyo jamaa! Kwahiyo serikali wakita kuendeleza zile figisu za awali basi ni kumnyima kibali jamaa mara kibali chake cha sasa kitakapoisha! Lakini swali linalofuata, je kule juu kuna Watanzania wanaoandaliwa kuchukua top positions? Nadhani hapa ndipo tunapofeli! Kama tunasema haiwezekani ceo atoke nje lakini hatujali ikiwa chini ya ceo kuna Watanzania wenye sifa, basi siku ceo mmoja akitoka tutajikuta ni kweli hakuna mtanzania mwenye sifa kwa sababu hawakuwa groomed earlier! Na sidhani kama tunaweza kuwalazimisha wachukue ceo nje ya Vodacom wakati kuna watu ndani ya Vodacom wenye sifa hata kama ni wageni! Yule dada wa Kenya walimleta kwa sababu ni "Vodacom mwenzao"!!
Tuko pamoja sana mkuu.
 
Mkuu mimi sitabishana na wewe, pia sitataka kutaja majina ya watu ambao hawafahamiki mbele ya hadhara. Lakini ntakupa mfano mmoja mzuri tu wa hukohuko Vodacom. Kulikuwa na watanzania kama wakina Kevin Twisa ambao nadhani ni vijana wenye uwezo mzuri sana kwenye mambo ya Telecom.

Unaposema kwamba watanzania hawana uwezo kisa hawamiliki makampuni binafsi au ukwasi mkubwa mimi hili sitalikubali hadi naingia kaburini.

Uwe na siku njema mkuu, ahsante.

Kevin Twisa alifukuzwa VODACOM kwa utoro kazini. Ndiyo walewale wazembe kazini ambao kw ajicho lako unawaona ni potential leaders. Sijui alikufurahisha nini.
 
Lakini swali linalofuata, je kule juu kuna Watanzania wanaoandaliwa kuchukua top positions? Nadhani hapa ndipo tunapofeli! Kama tunasema haiwezekani ceo atoke nje lakini hatujali ikiwa chini ya ceo kuna Watanzania wenye sifa, basi siku ceo mmoja akitoka tutajikuta ni kweli hakuna mtanzania mwenye sifa kwa sababu hawakuwa groomed earlier! Na sidhani kama tunaweza kuwalazimisha wachukue ceo nje ya Vodacom wakati kuna watu ndani ya Vodacom wenye sifa hata kama ni wageni! Yule dada wa Kenya walimleta kwa sababu ni "Vodacom mwenzao"!!

VODACOM imeingia mwaka 2000 hivyo kuna watu wako pale kwa hiyo miaka 19. Wamewekeza unyenyekevu na siyo kuonyesha aggresivenes ya kuwa CEO.

Kuwa CEO kunatakiwa uwe aggresive, ni mapambano ya kudumua bila kujali litakalokutokea na siyo kuonyesha utumwa wa kutaka kujua bosi wako anapenda timu gani kati ya Manchester na Barcelona. Au anakula chakula gani anachokipenda.
 
Kaka nikurekebishe kidogo. Hao ulio wataja kuwa wameongoza ACACIA..BANKS.. wanauzoefu na telecom companies ?

Sent using Jamii Forums mobile app
Nakuelewa vizuri ndugu yangu, nimetoa mfano huo kuonyesha kwamba kuna watanzania wenye uwezo wa kuongoza haya makampuni makubwa. Kama wako watanzania wanaongoza makampuni makubwa ya madini, sembuse Vodacom ?

Mkuu myplusbee kaelezea vizuri sana kwamba watanzania wenye utaalamu kwenye Telecom Industry wapo.

Kusema hakuna watanzania wenye utaalamu wakati yeye ni Mwenyekiti wa hiyo Board ni dharau na kiburi kwa watanzania. Ina maana Managers wote wa huko Vodacom hawana kabisa uwezo wa kuwa CEO au Managers wote wa idara ndani ya Vodacom ni wageni ? Ina maana Vodacom hakuna succession plan ?

NB: Kuna mdau nikamwabia kuna watanzania walikuwepo huko Vodacom kama Managers mfano Kevin Twisa, ambao uwezo wao ni mkubwa. Sasa unaposema hakuna watanzania wenye uwezo wa kuongoza kampuni kama Vodacom tumweleweje huyu Mafuruki ?
 
Ila Wamisri ndio wa kuwashobokea! For the record; mimi nathamini competence. Haijalishi ni nani alie nayo.

All in all. Tunajadili wakenya wamisri yaani extrnal. Kikubw ani kwamba watanzania hawafai. Wanafaa kwa majungu. Tena nilisahau. Na kwa ngono.
 
Kwenye kampuni ninayotafutia riziki zile nafasi za juu zipo ngozi yetu hii yani wana roho mbaya hata shetani ana afadhali,ile sheria ya mh raisi zile nafasi wapewe wazawa kwa kweli iondolewe sio wabunifu na hawajali muwajibikaji no motisha,walioanzisha usemi ngozi kota mbaya hawajakosea,safi Vodacom kwa kutambua hilo ili msonge mbele.

mvujajasho nguli

Ninashangaa sana mtu anapopigia debe watanzania wenzake wakati kuna ujinga kama huu usiofichika.
 
Hongera kwa bwana mdogo Hisham Hendi. Ila huo ndio utakuwa mwisho wa career yake after three years.
Voda com dont believe that an MD will still perform after three yrs. So he shouldnt expect a contract renewal after three yrs.
Historically, the recent past two Vodacom MDs are on retirement leave.
Huwezi toka Voda ukaenda tena uswahilini kuajiriwa kama sijui meneja wa nini! Huu ndio mwisho wa career. Akitoka hapo akawe mkulima tu.
Kina Ian wako wapi?
 
Kevin Twisa alifukuzwa VODACOM kwa utoro kazini. Ndiyo walewale wazembe kazini ambao kw ajicho lako unawaona ni potential leaders. Sijui alikufurahisha nini.
Hapana kosa la Kevin lilikuwa ni kubwa zaidi ya utoro kazini, jingine kabisa. Sema kwasababu sipendi kuzungumza maisha ya watu hadharani, sitapenda kuzungumza makosa ya Kevin Twisa kwasababu sikuwepo hata anapofukuzwa na kama nikifanya hivyo yatakuwa ni majungu.

Narudia tena, kukuambia mkuu. Unapoangalia makosa ya watu wachache na kujumuisha jamii nzima ya watanzania huo siyo uungwana. Mimi hizi tabia za kuponda watanzania wenzangu kisa nafanya kazi na wazungu au nimebahatika kufika sehemu ambazo wengi hawajafika nilishaziacha kwasababu hazina faida zaidi ya kujichumia laana bure.

Kama kuna makosa yamefanyika ntajaribu kuwa Objective na ntamkosoa mtu binafsi bila kukashifu jamii nzima ya Watanzania. Uwe na siku njema mkuu, ahsante sana.
 
Sasa kama hzo kampuni za watanzania hazipo huo u-CEO watanzania wanaushikia wapi???

Kama hakuna watanzania wenye kampuni kubwa means hakuna watanzania wanaopata exposure ya kuwa CEO kwenye makampuni makubwa.

Kama unabisha basi wataje watanzania wenye uwezo huo mkubwa unaosema wanaweza kuwa CEO kwenye makampuni makubwa. Taja angalau wa3 kwenye Tele industry

Swala la kulipa kodi limekuja sababu nafikiri ni kigezo sahihi cha kupima uadilifu na uongozi imara wa kampuni.

Kaka,

Kumbe unawajua watzanania wlaivyo wazembe. Hata hao walioondoka kwenye hizi kampuni utadhani wamepata exposure lakini angalia shughuli wanazoenda kufanya mtaani, ni hizi nimeziorodhesha,

01: Kufuga kuku (Broiler)
02: Kufuga kuku wa mayai
03: Kufuga nguruwe
04: Kuanzisha shule za msingi
05: Kuanzisha bakery ya mikate
06: Kuuza Keki
07: Kuanzisha shule za sekondari
08: Kuanzisha maduka ya MPESA
09: Kuanzisha majengo, tena mengine yako uswahilini
10: Kufanya biashara ya kuagiza nguo toka Uganda
11: Kufanya biashara ya kuagiza msurufu toka Dubai
12: Kujenga baa za pombe
13: Kununua mabasi ya usafiri
14: Kusafirisha mazao
15: Kununua magari ya kukodisha
16: Kununua magari ya texi
17: Kutengeneza bustani za mbogamboga
 
Back
Top Bottom