Nimekuelewa sana Kiongozi lakini maelezo yangu hayakutokana na hoja ya kutokuwa na Mtanzania mwenye sifa. Hoja yangu ilikuwa inajibu hoja ya huyo mdau aliyesema hata kama CEO angekuwa Mtanzania haina maana yoyote katika mazingira ambayo Vodacom yenyewe sio mali ya Tanzania. Ni kutokana na hoja yake hiyo ndo maana nikamweleza hata kama Vodacom TZ ni subsidiary ya Vodacom Group SA lakini umuhimu wake kwa Tanzania ni mkubwa sana na hivyo kuonesha ni namna nafasi za juu kwa kampuni kama hiyo inapaswa kwenda kwa mtu mwenye maslahi na Tanzania (kwa maana Mtanzania), na kama ni mgeni basi asiwe ni mgeni ambae nchi yake ina mgongano wa maslahi ya kiuchumi na Tanzania. Na ingawaje sijaona waliposema hakuna Mtanzania mwenye sifa lakini suala la kumteua mgeni linaashiria hivyo. Kwa maana nyingine, nakubaliana na wewe kwamba suala la kusema hakuna Mtanzania ni tusi kwa nchi yetu.Hapa hatuongelei kulipa kodi, tunaongela mtu kushika nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji/Mkuregenzi Mkuu (Executive Director) wa kampuni nafasi ambayo binafsi naamini wapo watanzania wenye uwezo wa kushika. Unaposema hakuna Mtanzania mwenye uwezo wa kuongoza kampuni kama Vodacom sisi tueleweje, wakati kuna watanzania wameshawahi kuwa hadi washauri kwenye Benki ya Dunia. Mimi hili sintakubaliana nalo mpaka naingia kaburini.
Lakini kuna hoja hapa inaongelewa sana na watu kwamba yule Mkenya angekuja kuiua Vodocom! Nakubaliana na wale wanaosema Kenya ni mshindani wake na wale wanaweza kufanya lolote kutuhujumu! Hata hivyo, kwa yule dada siamini hata kidogo kwamba eti angekuja kuihujumu Vodacom kwa sababu yule dada alitoka SafariCom,.Nasema sio rahisi kwa sababu Vodacom Tanzania na Safaricom ni wajukuu wa babu na bibi mmoja; Vodafone UK. Sitaki kuamini kwamba Safaricom wanaweza kuleta mtu wa kuiua Vodacom halafu awaache airtel, tigo na halotel wakila kuku kwa mrija! Niliunga mkono suala la yule dada kuwekewa figisu figisu kwa sababu tu naamini wapo Watanzania ambao wangeweza kushika hiyo nafasi lakini sio kwa hoja ya hofu ya hujuma! Kama ni hujuma basi labda hujuma ya kuua mitandao mingine lakini sio Vodacom!
Lakini tukija kwenye suala la huyo Muarabu nadhani serikali imeshindwa kufanya figisu figisu kwa sababu unlike yule dada wa Kenya, huyo Mwarabu alikuwa pale Vodacom na kwahiyo zile figisu za work permit zisingewezekana kwa huyo jamaa! Kwahiyo serikali wakita kuendeleza zile figisu za awali basi ni kumnyima kibali jamaa mara kibali chake cha sasa kitakapoisha! Lakini swali linalofuata, je kule juu kuna Watanzania wanaoandaliwa kuchukua top positions? Nadhani hapa ndipo tunapofeli! Kama tunasema haiwezekani ceo atoke nje lakini hatujali ikiwa chini ya ceo kuna Watanzania wenye sifa, basi siku ceo mmoja akitoka tutajikuta ni kweli hakuna mtanzania mwenye sifa kwa sababu hawakuwa groomed earlier! Na sidhani kama tunaweza kuwalazimisha wachukue ceo nje ya Vodacom wakati kuna watu ndani ya Vodacom wenye sifa hata kama ni wageni! Yule dada wa Kenya walimleta kwa sababu ni "Vodacom mwenzao"!!