Vodacom Tanzania yapata CEO Mpya, Hisham Hendi raia wa Misri

Nimekuelewa sana Kiongozi lakini maelezo yangu hayakutokana na hoja ya kutokuwa na Mtanzania mwenye sifa. Hoja yangu ilikuwa inajibu hoja ya huyo mdau aliyesema hata kama CEO angekuwa Mtanzania haina maana yoyote katika mazingira ambayo Vodacom yenyewe sio mali ya Tanzania. Ni kutokana na hoja yake hiyo ndo maana nikamweleza hata kama Vodacom TZ ni subsidiary ya Vodacom Group SA lakini umuhimu wake kwa Tanzania ni mkubwa sana na hivyo kuonesha ni namna nafasi za juu kwa kampuni kama hiyo inapaswa kwenda kwa mtu mwenye maslahi na Tanzania (kwa maana Mtanzania), na kama ni mgeni basi asiwe ni mgeni ambae nchi yake ina mgongano wa maslahi ya kiuchumi na Tanzania. Na ingawaje sijaona waliposema hakuna Mtanzania mwenye sifa lakini suala la kumteua mgeni linaashiria hivyo. Kwa maana nyingine, nakubaliana na wewe kwamba suala la kusema hakuna Mtanzania ni tusi kwa nchi yetu.

Lakini kuna hoja hapa inaongelewa sana na watu kwamba yule Mkenya angekuja kuiua Vodocom! Nakubaliana na wale wanaosema Kenya ni mshindani wake na wale wanaweza kufanya lolote kutuhujumu! Hata hivyo, kwa yule dada siamini hata kidogo kwamba eti angekuja kuihujumu Vodacom kwa sababu yule dada alitoka SafariCom,.Nasema sio rahisi kwa sababu Vodacom Tanzania na Safaricom ni wajukuu wa babu na bibi mmoja; Vodafone UK. Sitaki kuamini kwamba Safaricom wanaweza kuleta mtu wa kuiua Vodacom halafu awaache airtel, tigo na halotel wakila kuku kwa mrija! Niliunga mkono suala la yule dada kuwekewa figisu figisu kwa sababu tu naamini wapo Watanzania ambao wangeweza kushika hiyo nafasi lakini sio kwa hoja ya hofu ya hujuma! Kama ni hujuma basi labda hujuma ya kuua mitandao mingine lakini sio Vodacom!

Lakini tukija kwenye suala la huyo Muarabu nadhani serikali imeshindwa kufanya figisu figisu kwa sababu unlike yule dada wa Kenya, huyo Mwarabu alikuwa pale Vodacom na kwahiyo zile figisu za work permit zisingewezekana kwa huyo jamaa! Kwahiyo serikali wakita kuendeleza zile figisu za awali basi ni kumnyima kibali jamaa mara kibali chake cha sasa kitakapoisha! Lakini swali linalofuata, je kule juu kuna Watanzania wanaoandaliwa kuchukua top positions? Nadhani hapa ndipo tunapofeli! Kama tunasema haiwezekani ceo atoke nje lakini hatujali ikiwa chini ya ceo kuna Watanzania wenye sifa, basi siku ceo mmoja akitoka tutajikuta ni kweli hakuna mtanzania mwenye sifa kwa sababu hawakuwa groomed earlier! Na sidhani kama tunaweza kuwalazimisha wachukue ceo nje ya Vodacom wakati kuna watu ndani ya Vodacom wenye sifa hata kama ni wageni! Yule dada wa Kenya walimleta kwa sababu ni "Vodacom mwenzao"!!
 

Mkuu mimi hapa wala sitaki kubishana nataka tuwekane sana na kufukia makubaliano ya kiungwana. Nafasi ya Director kwenye Companies Act imetajwa kabisa na imesema dhahiri kwamba Director anaweza kuitwa jina lolote kutokana na nafasi yake aliyonayo.

Kwenye Interpretation Section kule juu wamesema hivi "A director includes any person occupying a position of a director by whatever name called"

Tofauti kidogo na ulichosema hapo juu, Companies Act imesema dhahiri kabisa na kutenganisha kazi za Board Members na zile za Director hadi kufikia hatua ya kusema kwamba atawajibika kwa Board huku akiwa ndiyo mtendaji mkuu wa shughuli za kila siku za kampuni.

NB 1: Hayo mengine ya Vodacom yako kwenye Memorandum na Articles of Association na wala hayanihusu. Lakini nitakachokikataa mpaka naingia kaburini ni kutaka kusema nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi siyo mtu mzito kwenye kampuni kisa tu yeye siyo mtendaji kama alivyo Mkurugenzi.

NB 2: Kama Mkurugenzi anawajibika kwenye Board ambayo inaongozwa na Mwenyekiti, huyu Mafuruki atasemaje hakuna Mtanzania mwenye uwezo wa kuongoza hiyo kampuni ?

NB 3: Halafu kitu kingine ambacho sikuelewi ni kutaka kusema kwamba Chairman of the Board hana umuhimu na ni nafasi ambayo inaweza ikajazwa tu kirahisi.

NB 4: Kuondolewa kwa Laurent Mafuru na Deo Mwanyika kisiasa na watawala wa nchi hii hakumaanishi kwamba hakuna watanzania ambao hawana uwezo wa kuongoza kampuni kama Vodacom.
 
Ww unalinganisha accasia na vodacom. Two difference companies zinazofanya kazi za tofauti kabisa.
Halaf usiwapangie vodacom wamuajri nani maana si kampun ya serikal ni binafsi. Na wananchi wana 25% ya hisa tu ambazo kisheria haziwapi nguv ya kufanya maamuz ndani ya vodacom.

Kampuni kubwa inatafuta Top ambae ana experience na telecom companies. Ndio maana viongoz wake wengi huko nyuma walishaongoza kwenye baadhi ya kampuni za simu. So wanajua nn cha kufanya wenye telecom industry.

Kama wako watanzania ambao wanadhani wana uwezo. Kwann hawaja apply.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siasa zinaharibia watu cv. Wakishaona ulishafanya maamamuzi ya kijinga kwenye cheo fulani. Hata interview hawakuiti

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kaka nikurekebishe kidogo. Hao ulio wataja kuwa wameongoza ACACIA..BANKS.. wanauzoefu na telecom companies ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni MTU wa kwenu kagera Mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenye TED talks alizungumza vizuri hasa kwenye AFRICAN RISING , alipinga kwa hoja na Mimi nilimuelewa na anatumika sana kwenye hyo presentation yake kwenye mijadala mingi nje ya afrika na ndan
Sent using Jamii Forums mobile app
 

Mkuu mimi sitabishana na wewe, pia sitataka kutaja majina ya watu ambao hawafahamiki mbele ya hadhara. Lakini ntakupa mfano mmoja mzuri tu wa hukohuko Vodacom. Kulikuwa na watanzania kama wakina Kevin Twisa ambao nadhani ni vijana wenye uwezo mzuri sana kwenye mambo ya Telecom.

Unaposema kwamba watanzania hawana uwezo kisa hawamiliki makampuni binafsi au ukwasi mkubwa mimi hili sitalikubali hadi naingia kaburini.

Uwe na siku njema mkuu, ahsante.
 
Tuko pamoja sana mkuu.
 

Kevin Twisa alifukuzwa VODACOM kwa utoro kazini. Ndiyo walewale wazembe kazini ambao kw ajicho lako unawaona ni potential leaders. Sijui alikufurahisha nini.
 

VODACOM imeingia mwaka 2000 hivyo kuna watu wako pale kwa hiyo miaka 19. Wamewekeza unyenyekevu na siyo kuonyesha aggresivenes ya kuwa CEO.

Kuwa CEO kunatakiwa uwe aggresive, ni mapambano ya kudumua bila kujali litakalokutokea na siyo kuonyesha utumwa wa kutaka kujua bosi wako anapenda timu gani kati ya Manchester na Barcelona. Au anakula chakula gani anachokipenda.
 
Kaka nikurekebishe kidogo. Hao ulio wataja kuwa wameongoza ACACIA..BANKS.. wanauzoefu na telecom companies ?

Sent using Jamii Forums mobile app
Nakuelewa vizuri ndugu yangu, nimetoa mfano huo kuonyesha kwamba kuna watanzania wenye uwezo wa kuongoza haya makampuni makubwa. Kama wako watanzania wanaongoza makampuni makubwa ya madini, sembuse Vodacom ?

Mkuu myplusbee kaelezea vizuri sana kwamba watanzania wenye utaalamu kwenye Telecom Industry wapo.

Kusema hakuna watanzania wenye utaalamu wakati yeye ni Mwenyekiti wa hiyo Board ni dharau na kiburi kwa watanzania. Ina maana Managers wote wa huko Vodacom hawana kabisa uwezo wa kuwa CEO au Managers wote wa idara ndani ya Vodacom ni wageni ? Ina maana Vodacom hakuna succession plan ?

NB: Kuna mdau nikamwabia kuna watanzania walikuwepo huko Vodacom kama Managers mfano Kevin Twisa, ambao uwezo wao ni mkubwa. Sasa unaposema hakuna watanzania wenye uwezo wa kuongoza kampuni kama Vodacom tumweleweje huyu Mafuruki ?
 
Ila Wamisri ndio wa kuwashobokea! For the record; mimi nathamini competence. Haijalishi ni nani alie nayo.

All in all. Tunajadili wakenya wamisri yaani extrnal. Kikubw ani kwamba watanzania hawafai. Wanafaa kwa majungu. Tena nilisahau. Na kwa ngono.
 

Ninashangaa sana mtu anapopigia debe watanzania wenzake wakati kuna ujinga kama huu usiofichika.
 
Kina Ian wako wapi?
 
Kevin Twisa alifukuzwa VODACOM kwa utoro kazini. Ndiyo walewale wazembe kazini ambao kw ajicho lako unawaona ni potential leaders. Sijui alikufurahisha nini.
Hapana kosa la Kevin lilikuwa ni kubwa zaidi ya utoro kazini, jingine kabisa. Sema kwasababu sipendi kuzungumza maisha ya watu hadharani, sitapenda kuzungumza makosa ya Kevin Twisa kwasababu sikuwepo hata anapofukuzwa na kama nikifanya hivyo yatakuwa ni majungu.

Narudia tena, kukuambia mkuu. Unapoangalia makosa ya watu wachache na kujumuisha jamii nzima ya watanzania huo siyo uungwana. Mimi hizi tabia za kuponda watanzania wenzangu kisa nafanya kazi na wazungu au nimebahatika kufika sehemu ambazo wengi hawajafika nilishaziacha kwasababu hazina faida zaidi ya kujichumia laana bure.

Kama kuna makosa yamefanyika ntajaribu kuwa Objective na ntamkosoa mtu binafsi bila kukashifu jamii nzima ya Watanzania. Uwe na siku njema mkuu, ahsante sana.
 

Kaka,

Kumbe unawajua watzanania wlaivyo wazembe. Hata hao walioondoka kwenye hizi kampuni utadhani wamepata exposure lakini angalia shughuli wanazoenda kufanya mtaani, ni hizi nimeziorodhesha,

01: Kufuga kuku (Broiler)
02: Kufuga kuku wa mayai
03: Kufuga nguruwe
04: Kuanzisha shule za msingi
05: Kuanzisha bakery ya mikate
06: Kuuza Keki
07: Kuanzisha shule za sekondari
08: Kuanzisha maduka ya MPESA
09: Kuanzisha majengo, tena mengine yako uswahilini
10: Kufanya biashara ya kuagiza nguo toka Uganda
11: Kufanya biashara ya kuagiza msurufu toka Dubai
12: Kujenga baa za pombe
13: Kununua mabasi ya usafiri
14: Kusafirisha mazao
15: Kununua magari ya kukodisha
16: Kununua magari ya texi
17: Kutengeneza bustani za mbogamboga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…