Vodacom, tiGO wapandisha tena bei za vifurushi vya Internet. Nape unafanya kazi gani?

Vodacom, tiGO wapandisha tena bei za vifurushi vya Internet. Nape unafanya kazi gani?

Mzee suala la mawasiliano huwa haliachwi bila kuwa na regulator na huyo huwa ni chombo cha serikali kitakachosimamia sheria na bei zake. Hiyo sio biashara ya vitumbua
Nini maana ya kuwa na regulator anaepanga bei badala ya kuwa na ushindani sokoni?

Bei ni ileile kwa makampuni yote. Sasa mantiki ya kuwa na makampuni manne wanaotoa huduma ileile ipo wapi?

Kunatakiwa kuwe na biashara huria, regulator aweke mkono kwenye mambo ya usalama, ila kwenye bei aachie makampuni yashindane yenyewe. Ikiwezekana bei zishuke kumlinda mwananchi.

Hakuna mantiki ya kuwa na regulator ambae anaumiza wananchi.

Hopeless kabisa.
 
Sipendagi hii tabia ya viongozi ku compare hali ya nchi yetu na nchi nyingine ......bas tu

Hii inakuwa dalili ya kushindwa kuongoza
Kama nchi nyingine wanaumia, ndio iwe sababu ya sisi kuumia pia??
Afu wanafananishaga kwenye matatizo tu hawasemagi kama wenzetu wanafurahia maisha kiasi gani, mishahara ya wafanyakazi ipoje, huduma za kijamii zikoje wao wanahangaikaga tu na kulinganisha matatizo
 
The types of complaint Ofcom deals with
  • Complaints about phone or internet services. ...
  • Complaints about unwanted calls and messages. ...
  • Complaints about TV, radio or on-demand services. ...
  • Complaints about postal services. ...
  • Complaints about wireless interference. ...
  • Complaints about video-sharing platforms (VSP)
Nataka uweke Ofcom wapi wamesema wana regulate bei?
Kusoma hujui? Ngoja ninukuu "....ofcom regulate prices, imposes charge controls....."
 
Nini maana ya kuwa na regulator anaepanga bei badala ya kuwa na ushindani sokoni?

Bei ni ileile kwa makampuni yote. Sasa mantiki ya kuwa na makampuni manne wanaotoa huduma ileile ipo wapi?

Kunatakiwa kuwe na biashara huria, regulator aweke mkono kwenye mambo ya usalama, ila kwenye bei aachie makampuni yashindane yenyewe. Ikiwezekana bei zishuke kumlinda mwananchi.

Hakuna mantiki ya kuwa na regulator ambae anaumiza wananchi.

Hopeless kabisa.
Bei iliyo regulated haipo fixed. Gharama ni Kati ya sh 1 Hadi sh 9. Kama Kuna kampuni itauza mb 1 kwa sh 1 ni sawa tu, Kama itauza kwa sh 9 ni sawa pia. Ubaya ni kuwa haya makampuni yote huuza kwa kufanana Ila bado wapo kwenye bei ambayo omepangwa na mamlaka.

Wanacholalamika watu ni labda mamlaka ipunguze bei kwa ukomo, badala ya sh 9 labda Sasa iwe sh 2
 
Kama hicho ofa maaalum wameona tunafaid hizo dakika. Mwanzo ilikua 2000 unapata dk 100 na gb 1.kwa wik
Wakaona hapana.wakafuta dk 100 zikawa 30 na mb 1000.na kitu najiuliza kwanin kwenye vifurush vingine wanasema gb 1 ila hicho cha ofa wanaandika mb 1000 badala ya kusema gb.ni nini malengo?

No sawa sawa na kumwambia mtu nakupa laki kumi.kwa nin usiseme nakupa mil.1? Au inakua mb 1000 ila pale kunakua na boshen flan mana kinaenda sio poa ghafla mteja umefika 75%ya matumizi.

Ila mungu sio athuman japo wanatudhulum kwa kila hali mara salio limekatwa kwa kujiunga na game mara sijui mb zimeliwa na auto update anawakomesha hela hazina baraka
1000MB siyo sawa na 1GB.
1024MB=1GB.
Hii ni sayansi tu mkuu.
 
Hata Tigo Leo imepanda
Airtel pia.
Hali mbaya sana nchini kwetu.
Maji na Umeme ni shida, bei za vitu zinapanda kila kukicha.
Mh.Samia ajitafakari juu ya usimamizi wake dhidi ya viongozi aliowapa dhamana kuongoza wizara na idara mbalimbali.

Aweso, Nape na Makamba ni sifuri kabisa. Hakuna viongozi hapo.
Waziri wa kilimo pia ni janga, mbolea imekuwa kama cocaine au heroin au crystal meth.
 
Ni kosa kubwa sana kumuachia Rostam kutawala telecom industry. Wacha tuone haya mambo yanaishia wapi.
Yani buku unapata 350mb kweli!
 
Kusoma hujui? Ngoja ninukuu "....ofcom regulate prices, imposes charge controls....."
Sijui kusoma hiyo sheria 2006 ilifutwa service customer wanaamua acha kupitia habari zimepitwa ni free market wateja ndio wanaamua bei kwa huduma bora
 
Kusoma hujui? Ngoja ninukuu "....ofcom regulate prices, imposes charge controls....."
1.19 The ending of retail price control after more than twenty years is a major alteration in the regulatory regime. The March Consultation outlined that Ofcom was considering a public information campaign to raise consumer awareness of the change. This UK wide campaign will commence forthwith and will help consumers to understand that from 1 August 2006 consumer choice rather than regulation will be the key determinant of the price and quality of services that customers receive. Annexes 1 and 2 set out the details of this information campaign.

Mwenye kujuwa kusoma hii nayo ngumu kujuwa? tuliza mzuka soma vizuri
 
Bwana yule alituchelewesha sana.

Acheni kulalamika wakati sheria ilitungwa na Magu

Alisikika chawa mmoja asiyejua yupo upande wa mama au upinzani
 
Badala ya kuendelea kumlalamikia Nape inabidi kuchukua hatua wenyewe tunaweza kuhamasishana kila siku kutoweka vocha Kwa siku. Maisha yetu lazima tutumie simu ila tukiamua jumamosi hatununui vocha isipokuwa wale wenye matatizo lazima watashika adabu ila kuendelea kulalamika bila kuchukua hatua wataendelea kutunyanyasa
 
Ongezea Jenister, Jafo nk... Kifupi vimeo wapo wengi kila mahala na kilichowaweka ni connections hakuna kingine.

Bahati mbaya hatuna utaratibu wa kitalaam wa kupata watu wazuri zaidi ya connection na ukada wa chama.
Sahivi ni udini umetawala, Tanga imetoa mawaziri 4 na Pwani 3 na wakati Arusha nzima hakuna wala Dar
 
Back
Top Bottom