Vodacom wameanza wizi wa hela za M-PESA

Vodacom wameanza wizi wa hela za M-PESA

G-Funk

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2022
Posts
2,398
Reaction score
5,554
Juzi asubuhi nilikwenda kwa wakala kutoa pesa kabla ya kuanza mihangaiko ya siku nikawa nimebakiza salio katika simu takribani Tshs.15,000+,,,, Cha ajabu jioni wakati natoka mishe mishe nikawa nataka nijiunge kifurushi cha kuongea na simu nikafanikiwa kujiunga kilikuwa cha Tsh.500. Ujumbe uliorudi MPESA kuja kwangu ulisoma kuwa salio lililobaki ni Tsh.10,000.

Hii inaashiria wameniibia sh.5000 nzima pasipo na sababu ya msingi.

Hili swala ni above and beyond halivumiliki napataje haki yangu kama mteja wakuu. Hawa jamaa naona mazoea yamezidi wanakwapua hela kwenye account za MPESA na kujikausha. Imenikera mno!!!

STATEMENTS HIZO TOKA VODA.
Screenshot_2022-06-02-07-47-44.png
 
5,000 kubwa sana, wairudishe.
Mkuu sms ninazo kwa ajili ya ushahidi wanioneshe nadaiwa kivipi? Huo ni uhuni kama ulivyo uhuni mwengine. Unatoaje hela kwenye account ya mtu bila consent?
 
😀 mkuu itakuwa umejiunga kifurushi cha 5,000
hamna kitu cha namna hio mkuu kifurushi ni chajero na breakdown ni hio! Voda naitumia sababu napokelea hela toka nje ya nchi ila kwa style hii ntatafuta mbadala tu! Huu ushenzi itafikia wakati tutaenda kuwavunjia computer zao vodashops! ili nao wasikie uchungu maana kama ndio style yao wanakukata na kukubambikia deni sintokubali!
 
Mimi siwez kuamini mara ukope songesha,nipige tafu mara nn walikata na ukiendelea kulia lia wanakukata.
mkuu songesha nafanyaga ila sijawahi chukua zaidi ya buku na ukiweka salio mpesa tu wanakata hela yao chap. So huwa sifugi madeni kabisa sasa hilo deni ambalo wao wanasema ni lipi?
 
naiamini sana hii kampuni huwa sio wezi kuna mahali tatizo lipo na wewe upande wa pesa.hukuangalia salio kabla hujatoa namaanisha hukuwa unajua salio lililopo kabla hujatoa pesa .
Mzee mi sio kichaa kabisa, nimetoa kiasi A na nilikuwa na lengo kile kitachobakia nikifanyie swala flani so nilikuwa najua kabisa kuna kiasi gani katika simu. Kilichotokea ni sawa na wewe unajua gari yako ni nyeupe unarudi jioni unaikuta ya bluu
 
Mzee mi sio kichaa kabisa, nimetoa kiasi A na nilikuwa na lengo kile kitachobakia nikifanyie swala flani so nilikuwa najua kabisa kuna kiasi gani katika simu. Kilichotokea ni sawa na wewe unajua gari yako ni nyeupe unarudi jioni unaikuta ya bluu
Piga simu customer care wakuangalizie zilivyoingia na kutoka kwa miamala mitano ya mwisho
 
Mkuu sijawahi kukopa wanioneshe hio list ya mkopo wao kama nahusika vipi sababu sijawahi kopa hela kwao na sidaiwi nao
Angalia statement ya akaunti yako ya M Pesa mkuu.... Sidhani kama wanaweza kukuibia.
 
si uwapeleke mahakamani ili wakulipe mpunga wa kueleweka?
 
Haaahaaaa hakuna kampuni yenye usalama upande wa peas kama Vodacom mpesa ltd..piga simu customer care utapata majibu mazuri na kujua peas ilikokwenda
 
kifurushi cha kuongea na simu nikafanikiwa kujiunga kilikuwa cha Tsh.500. Ujumbe uliorudi MPESA kuja kwangu ulisoma kuwa salio lililobaki ni Tsh.10,000.

Hii inaashiria wameniibia sh.5000 nzima pasipo na sababu ya msingi.
Huenda wakati wa kununua kifurushi cha 500 ulibonyeza 0 mara 3 bila kuhakiki au 0 ya 3 ilichelewa kurespond mfumo ukasoma 5000
 
Back
Top Bottom