Voices From Within: Je, wajua yuko Peponi, Mbinguni, Kwa Baba yake? Why kumshutumu, kumsakama na kumsimanga? Aachwe apumzike kwa amani

Maneno ya Mungu yanasema wafu watafufuliwa siku ya mwisho,..!
Mkuu Mshana Jr , japo ni kweli siku ya mwisho kutakuwa na ufufuko wa miili, kwanza huo ufufuko sio wa miili hii ya nyama, ni wa miili ya roho!, spiritual bodies, hii miili ya nyama, physical body, roho ikiisha acha mwili, that is the end of it!. Mwili huu unageuka mavumbi na haina shughuli nyingine yoyote!.

Watakao fufuliwa siku ya mwisho ni wale waliokufa kwenye kama!. Hawa wanaokufa sasa wanahukumiwa, wa peponi wanakwenda peponi na kuanza kula raha, wa motoni nao wanakwenda motoni na kupata mateso ya jehanam ya ziwa la moto wa milele.

Mbinguni, ahera, peponi na motoni ni kwenye ulimwengu wa roho, kule hakuna distance and time, siku moja ni kama miaka elfu moja, na miaka elfu moja ni kama siku moja!. Hivyo anayeungua motoni miaka elfu iliyopita na sawa na anaye ingia leo!.
Hivyo JPM wetu yuko peponi akila good time!.
P
 
JPM huyu aliyezuia tusikusanyike Makanisani kumuombea Tundu Lissu afya njema ,baada ya jaribio la kuuaea kama mnyama!
JPM Huyu huyu ambaye hakutia hata pole baada ya jirani yake Mawazo Nelson kuuawa kinyama Kwa mapanga kule Chato!
Kama ndivyo,basi the so Called Pepo it is a Relative Term/Phenomenal
 
Mungu ni pendo!. Hata dhambi zako ziwe nyeusi kama masizi, ukitubu, Mungu anakusamehe!. Zile siku za mwisho, JPM, changed for the better, mimi nilikuwa nasema humu from time to time,
  1. Magufuli is getting better and better, he is changing for the better. Hongera sana!
  2. Tusilalamike tuu, kulaumu na kulaani kila kitu, kwenye mazuri tupongeze! Rais Magufuli is changing for the better!.
  3. Tusikalie kumlaumu tu Rais Magufuli na Serikali yake wanapofanya mabaya, kwenye mazuri pia tupongeze!
  4. https://www.jamiiforums.com/threads/voices-from-within-jpm-ni-rais-msikivu-na-mwenye-huruma-1818712/
  5. Rais Magufuli, so far, is the best president this country has ever had. Msikivu, ana upendo na huruma. Atabarikiwa sana. Tanzania itabarikiwa!
  6. "Mimi ni Mwenzenu Hapa, Sijabadilika ni Yule Yule "KaJoni" - Ni Maneno Simple, Humble and Down to Earth Yenye Maana Kubwa
  7. Baadhi ya matendo yake ya ukatili yalikuja kufidiwa na matendo mema ya huruma na upendo kama kule kugawa mabulungutu, kutetea masikini, wamachinga etc
  8. hivyo ile siku yake ya mwisho kabla Mungu hajaichukua roho yake, alitubu dhambi zake zote, akasamehewa na ndio maana saa hizi yuko peponi, mbinguni kwa baba yake.
  9. Hata hili la katiba mpya, Mungu asinge mchukua, saa hizi tungekuwa kwenye mchakato Trends, Visions: Watanzania msitatizwe na kauli zake kuhusu Katiba, baada ya Nyerere, ni Magufuli ndiye ataacha legacy kubwa ikiwemo Katiba Mpya!.
P
 
Unanyambwa wewe, wewe ni nani umpamgie Mungu, lofa mmoja.
 
Unanyambwa wewe, wewe ni nani umpamgie Mungu, lofa mmoja.
Kwanza asante kwa hilo neno, ubarikiwe sana!. Pili Mungu hapangiwi bali huzungumza na sisi kupitia ndoto, maoni, revelations na Voices from within.
P
 
Mbinguni, ahera, peponi na motoni ni kwenye ulimwengu wa roho, kule hakuna distance and time, siku moja ni kama miaka elfu moja, na miaka elfu moja ni kama siku moja!.[emoji817][emoji818]
 
Magufuli aliye kula lambilambi za tetemeko!
 
Soma, sauti ya ndani inasema na Pascal.
Kumbuka siku sauti hiyo itakapo kusemesha nawe utatuambia.
 
Aliua, kuteka, kupora na kutesa watu bila sababu zozote za maana.
Mungu muweza wa yote akapindua meza.
Laana ya kijana wa makambako aliyepigwa na polisi, Tiss na jeshi kwa amri yake itamuandama popote alipo.
Mungu hasamehi waovu
Huyu alikuwa muovu
Imeandikwa"Hata kama dhambi zako zitakuwa nyekundu kama damu, lakini wewe ukazitubu hizo dhambi, hakika utakuwa mweupe kama theluji"
 
Imeandikwa"Hata kama dhambi zako zitakuwa nyekundu kama damu, lakini wewe ukazitubu hizo dhambi, hakika utakuwa mweupe kama theluji"
Alitubu wapi? [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] Bora hata mara mia Mzee Ben alitubu kwa kuandika kwenye Kitabu pia mbele ya watu wakati wa uzinduzi wa Kitabu! Ila Jiwe hadi anakata Roho wapambe wake hawakuamini kama jamaa anadanja! [emoji13] [emoji13] [emoji13]
 
Ni kweli, pia urais ni taasisi, tumemuacha yeye ila taasisi ya awamu yake bado ina la kujibu na jina lake litatumika tu likibeba hiyo awamu ya taasisi
 
Aliua, kuteka, kupora na kutesa watu bila sababu zozote za maana.
Mungu muweza wa yote akapindua meza.
Laana ya kijana wa makambako aliyepigwa na polisi, Tiss na jeshi kwa amri yake itamuandama popote alipo.
Mungu hasamehi waovu
Huyu alikuwa muovu
Rais gani hajaua?
Unapopewa madaraka makubwa kama ya Urais utaua tu!
Unaweza ukaua directly au indirectly. Vinginevyo kataa tu hayo madaraka.
 
Mayala nakuhakikishia hiyo sauti ni ya shetani tena lucifer mwenyewe!
Labda ile 'mbingu' nyingine na sio hii tunayoijua nwanaokwenda kule
 
Wewe umejuaje yuko peponi?ulipanda huko kuona?Mbona lipo kuzimu huko linaungua? Sukuma gang mtateseka sana kama vipi kazikwe naye
 
Alitubu wapi? [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] hadi anakata Roho wapambe wake hawakuamini kama jamaa anadanja! [emoji13] [emoji13] [emoji13]
Mkuu Alfred Daud Pigangoma , much respect for being verified!.
  1. Mungu ni nani na yuko wapi- Mungu ni Sprint ambaye ndie pekee Alfa na Omega hukaa kila mahali, Omnipresence
  2. Binadamu ni nani, ni kiumbe Mungu alichokiumba kwa udogo na kukipulizia pumzi ya uhai yenye Umungu ndani yake kwa lengo moja tuu kumtii. Hivyo Mungu yuko yuko ndani yetu na sisi tuko ndani yake.
  3. Mkataba wa uhai na kifo ni mkataba baina ya wawili tuu!. Wewe na Mungu wako. Hakuna yoyote mwingine mwenye uwezo wa kuumba na hakuna yeyote mwenye uwezo wa kuutoa uhai isipokuwa YEYE!.
  4. Amri za Mungu ni mkataba baina ya wawili tuu wewe na Mungu wako. Ukivunja amri yoyote ya Mungu anayeandika ni dhambi au sio dhambi ni mmoja tuu YEYE !.
  5. Unaweza kuvunja amri ya 5 kwa kuua na ukaandikiwa baraka na unaweza kuua ukaandikiwa dhambi anayejua nani ni mdhambi na nani ni Mtakatifu ni YEYE tuu ndio maana tunafundishwa tusihukumu ili tusihukumiwe!.
  6. Kama ilivyo kutenda dhambi ni baina yako na Mungu wako, vivyo hivyo kutubu dhambi zako ni baina yako na Mungu wako.
  7. Hakuna ajuaye mtu yoyote kabla ya kifo alizungumza nini na Mungu wake hivyo hakuna ajuaye.
  8. Tunaokolewa kwa neema na sio kwa matendo.
  9. Kwa vile Mungu yuko ndani yetu huongea nasi kwa vision kutokewa, kwa ndoto za maono na kwa kusema na wewe kwa sauti ya ndani, Voices from within, wengi hawajui kuisikiliza sauti Mungu iliyo ndani yake iitwayo consciousness.
  10. Mimi nimeisikia sauti hii kuwa JPM alitubu dhambi zake zote na akasamehewa sasa yuko peponi mbinguni kwa Baba yake yuko na Baba yake.
P
 
Na anatarajia kugombea uongozi wa maraika!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…