Voices From Within: Sultan Jamshid bin Abdullah Al Said atafurahi zaidi kama atarudi Zanzibar. Rais Samia, Rais Mwinyi, sameheni, utabarikiwa sana!

Nendeni kwanza kwenye kaburi la Karume mkaombe hiyo ruhusa.

Kuna clip ya Karume huwa naiskia redioni akikataa uwepo wa masultani Zanzibar, kwa ile sauti yake na kumaanisha kwake, akifufuka leo kwa mfano akasoma hili bandiko hapa, naona anaweza kuondoka na mtu..

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Asili ya mababu zake ni Oman,iweje hao waomani wamkatae ndugu Yao?halafu sisi weusi ambao ndio tulioumia na madhila ya huo usultan tumpokee aje afie kwetu! Kwa wema Gani na mapenzi Gani tuliyonayo juu yake na mababu zake???!
 
Asili ya mababu zake ni Oman,iweje hao waomani wamkatae ndugu Yao?halafu sisi weusi ambao ndio tulioumia na madhila ya huo usultan tumpokee aje afie kwetu! Kwa wema Gani na mapenzi Gani tuliyonayo juu yake na mababu zake???!
Sio tu asili ya mababu zake ni Oman. Hata utawala wa Oman ni ndugu zake, ni ukoo mmoja. Babu yao alipofariki, yake na mdogo wake wakagawana nchi. Baba yake akachukua Zanzibar, mwingine akachukua Oman. Kipindi hicho Oman hakuna kitu, Zanzibar ndio ilikuwa fresh. Waliogopa asije akawapindua
 
Unaandika tu uharo mradi umekujaa
 
Kwanini familia ya Okello ndiyo isirudi kuishi Zanzibar na kutunzwa na serikali ya Zanzibar!!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu, najua wewe ni jasiri! Unahofia nini kuweka kika kitu wazi?

Kwa sasa kuna uhuru wa kusema mkuu!
Funguka ueleweke mpaka kwa "watoto".
 
Historia ya sultan huyu na maisha yake baada ya mapinduzi na kuhamia uhamishoni ni ya majonzi na majuto.Ni vema akakaribishwa zanzibar kama Bado yu hai huenda nafsi yake ikapata faraja na inawezekana akataman kufia Zanzibar
Akaribishwe tu!
Uhasama haulipi.
 
Hakufanya yeye. Alikuwa kiongozi halali wa Zanzibar. Aachwe arudi "nyumbani" na apate stahiki za kiongozi mkuu mstaafu!
 
Muwe mnaachaga upofu kuwa masultani ndo walileta ushoga?
Na yule anaetangazia ulimwengu akiwa Italy tusemeje! Historia huwa mnasomea chooni ama!!

Kiufupi ulimwengu ukiamua kufunika ukweli huwa unaweza japo kwa kuchukua muda.sote tunafahamu ukweli wa mapinduzi ijapo unafichwa lakini utafichwa kwa wale wasiofatilia ukweli ama kukaa na wazee.

Jamshid bado laana itamtafuna ya kukubali kuingizwa mkenge na waingereza na kusaliti taratibu na miiko..
Kakubali mpaka kuteketeza misahafu baharini kisa ulafi wa madaraka kisa wazungu huyu Karma itamtafuna mpaka .
 
Kwanini utawala wa Oman ulimkatalia ndugu yao asirudi Iman
Alisaliti miiko ya ukoo na kufuata wanachotaka waingereza..
Mapinduzi ooh eti mapinduzi lengo la mapinduzi jingine kabisa na ulimwengu ulivodanganywa.
 
UNATUTEGA EEEH MZEE WA KULE KWENYE MAGARI YA TINTED EEEH....!!!
UMESHASOMEKA......!!!
 
Historia ya sultan huyu na maisha yake baada ya mapinduzi na kuhamia uhamishoni ni ya majonzi na majuto.Ni vema akakaribishwa zanzibar kama Bado yu hai huenda nafsi yake ikapata faraja na inawezekana akataman kufia Zanzibar
Hata arudi Zanzibar huyu Karma itamtafuna hata aje huyuu bado si aliona waingereza watamsaidia unakubali mpaka Qur an zinatupwa bahari na kutuaminisha Eti mapinduzi ooh mapinduzi.
 
Oman ambako ndiyo chimbuko lake na ambao ndiyo ndugu zake walipaswa kuwa wa kwanza kumsaidia, uliwahi kujiuliza ni kwanini walimkataa Mwarabu mwenzao wakati anapinduliwa na Waswahili? Kwanini walimkataa hata kwa kumpa hifadhi tu badala yake Waingereza ndiyo wakawa na huruma naye na kumpatia Msaada?
Kwani Oman waliendelea kumuwekea ngumu asikanyage nchini mwao? Aliwakosea nini? Hata wale waswahili waliompindua walirudisha mioyo na kumwambia kama atataka yipo huru kurjea Zanzibar lakini Oman waliendelea kumkataa, hadi amefikisha umri wa kuvalishwa pampus na kusahau jina lake ndiyo wamekubali kumruhusu aende kuishi mchini mwao.
Au ndiyo ile ugomvi wa madaraka baada ya Sultan aliyekuwa akizitawala Zanzibar na Oman kuamua kuhamishia Makao yake Zanzibar na kuendelea kuitawala Oman kutokea Zanzibar huku Zanzibar ikianza kupaa kimaendeleo na kuifikia na kuizidi Oman kwa nyakati zole, ambapo baada ya kufa warithi wakagawana mbao kwa yule aliyepewa Zanzibar kugoma kuwa chini ya aliyerithishwa Oman na wa Oman kugoma kuwa chini ya Zanzibar na hivyo kila upande ukajiendea kivyake.
Huo ugomvi wa warithi ndiyo ilikuwa sababu nini mkuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…