Wanabodi,
Baada ya kuisoma hii story hapa chini, nimeisikia sauti ya ndani, the voices from within ikiniambia huyu Sultan Jamshid bin Abdullah Al Said, ambaye alizaliwa tarehe 16 Septemba 1929 na kuwa Sultan wa Zanzibar baada ya kifo cha babake , Abdullah Bin Khalifa mwezi Julai 1963, akiwa na umri wa miaka 95, sauti hiyo imeniambia huyu Sultani anatamani sana kurejea Zanzibar, kuja kukamilisha ..., na kuwa atafurahi sana, na atakuwa na amani sana, iwapo kama ata... akiwa Zanzibar mahali alipozaliwa!.
Natoa wito kwa Rais Samia, na rais Mwinyi, kumfanyia application ya zile 4R za Rais Samia kwa kumsamehe, kumjengea mazingira wezeshi arejee Zanzibar, ili ... akiwa Zanzibar.
Hili likifanyika, Rais Samia na rais Mwinyi, mtabarikiwa sana for healing machungu ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, na Zanzibar itabarikiwa sana!.
The story ni C&P from BBC Swahili.
Jamshid bin Abdullah Al Said: Fahamu aliko Sultani wa mwisho wa Zanzibar
29 Septemba 2020
Imeboreshwa 12 Januari 2021
CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Maelezo ya picha,
Jamshid bin Abdullah Al Said
Rejea za Mwandishi kuhusu Zanzibar
Ombi kwa Rais Samia ni kufuatia Ombi hili
Watanzania tumshukuru Mungu kupata mtu mwenye moyo wa kusamehe. Je, tumuombe asamehe tu bila kuombwa msamaha au akomae naye? ambapo Rais Samia alimsamehe mtu bila kuombwa msamaha. Hivyo anaweza kabisa kumsamehe Sultan Jamshid bila hitaji la Sultan huyo kuomba msamaha.
NB. Kuna gaps nimeziacha, ili ujumbe huu uwafikie wale tuu wenye uwezo to read in between the lines!.
Nawatakia Mapumziko mema ya maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Paskali.