Xi Jinping
JF-Expert Member
- Jun 14, 2023
- 3,651
- 11,548
Volkswagen inafikiria iwapo itafunga viwanda nchini Ujerumani kwa mara ya kwanza katika historia yake ya miaka 87 huku ikielekea kuongeza upunguzaji wa gharama huku kukiwa na ushindani unaoongezeka kutoka kwa watengenezaji magari ya umeme nchini China.
–London (CNN)
–London (CNN)
Mapema wiki hii CNN iliripoti taarifa hiyo kuhusu Volkswagen (VW) moja ya kampuni kubwa duniani ya kutengeneza magari ya nchini Ujerumani.
Tangu mwaka jana mwanzoni VW imekuwa ikipambana kupunguza gharama za uzalishaji bila mafanikio.
Wakati wakipambana na hilo imekutana tena na changamoto nyingine, inazidi kupoteza soko lake kubwa zaidi la magari la China kutokana na ushindani mkali kutoka kwa kampuni za kutengeneza magari za nchini China kama vile BYD.
Pia BYD imekuwa ikizipa ushindani mkali kampuni za Ulaya kutia ndani VW kwenye soko la dunia la magari ya umeme.
Changamoto haiko tu kwa VW bali pia sekta ya viwanda vya magari barani Ulaya kwa ujumla.

"Sekta ya utengenezaji magari barani Ulaya iko katika hali ngumu sana."
–Oliver Blume (Volkswagen C.E.O)
–Oliver Blume (Volkswagen C.E.O)
Kuna sababu gani za kudorora kwa sekta ya viwanda vya magari barani Ulaya?
"Mazingira ya kiuchumi yamekuwa magumu zaidi, na washindani wapya wanaingia kwenye soko la Ulaya. Ujerumani haswa kama eneo la utengenezaji iko nyuma zaidi katika suala la ushindani."
–Oliver Blume (Volkswagen C.E.O)
Mipango ya VW kupunguza gharama itakabiliwa na upinzani mkubwa kutoka kwa wawakilishi wa wafanyakazi na vyama vya wafanyakazi. Moja ya chama cha wafanyakazi chenye nguvu zaidi nchini Ujerumani kimeilaumu VW kwa usimamizi mbovu wa kampuni hiyo na kuapa kupigana kulinda kazi.
Tulitegemea mambo kama haya yaitokee Urusi ambayo Ujerumani na washirika wenzake wameiwekea vikwazo vya kiuchumi.
Tulitegemea mambo kama haya yaitokee Urusi ambayo Ujerumani na washirika wenzake wameiwekea vikwazo vya kiuchumi.