Voyager 1 chombo cha ajabu kinachonitisha kichwa. Aisee! hii itakushangaza

Voyager 1 chombo cha ajabu kinachonitisha kichwa. Aisee! hii itakushangaza

Salute bosses!
Hebu nikuambie story moja ambayo imenishangaza sana sana sana, mpk nimekaa nikagusa research hii wiki nzima kuhakikisha nimeelewana na hiki kitu vizuri. The research ni kuhusu chombo cha angani kinaitwa Voyager 1, na guys ukisoma hii story mpk mwisho utajiona mdogo sana mbele ya ile technology ya miaka ya 1970s.

Tuendelee
Juzi nilikuwa naenda maeneo tu kwenye makazi ya ndugu yangu, safari yangu ys usiku nilikuwa nacheki YouTube random videos, nikakutana na documentary moja kuhusu space exploration. Yani nilikuwa nawatch tu kwa ajili ya kupitisha muda mpk usingizi uniingie. Lakini kumbe nilikua sijui ninajiiingiza kwenye nini, jamaa wanazungumza kuhusu spacecraft fulani iliyotumwa mwaka 1977 bado inafanya kazi mpk sasa. Hapo akili ikagousa kitu, nikasema kwani hii ni nini sasa.

Nilivyofika makazi yao next morning sikuweza kupiga story nyingine, nilikuwa naongelea Voyager. Wadau wakanicheka sana wakaniambia mimi najifanya mjanja kumbe sijui hata basic space exploration. Lkn sikujali nikaona ni unyama tu, niliamua nitumie muda wangu kuelewa hii kitu vizuri.


Voyager 1 ni nini hasa?
Nikupe background kidogo ya hii kitu mwanetu. Mwaka 1977, wakati baba zetu walikuwa wanacheza draft na kusikilia kaset hapa Bongo, wazungu pale NASA walikuwa wanaandaa jambo kubwa. Walikuwa wameunda hizi spacecraft mbili Voyager 1 na Voyager 2. Hivi vyombo vilikuwa na mission simple lkn noma sana, mission ilikuwa kwenda kuvumbua sayari za mbali Jupiter na Saturn, kisha kuendelea safari bila kurudi tena.

Sept 5, 1977 Voyager 1 ilirushwa angani kutoka Florida. Na hapa ndio mambo yalianza, hiyo spacecraft haikuwa kama hizi satellites za leo ambazo zinaenda kwenye orbit kuzunguka Dunia tu, hapana. Hii bhan ilikuwa designed kwenda mbali kinom, na kuendelea kusafiri daima bila kusimama.

Nikakaa nikafanya hesabu, nikagundua kuwa tangu 1977 mpk 2026 sasa ni miaka 47+. Yani chombo hiki bado kinafanya kazi baada ya miaka yote hii, kinatupelekea data kutoka nje ya solar system yetu. Hiki kitu ambacho huwezi kuamini ikiwa haujaelewa vizuri.(😂 Wifi yangu huvuki mita 50 connection inapotea)

View attachment 3556220

Umbali gani tunazungumzia hapa?
Hapa ndio kiswahili kinaingia mdau. Voyager 1 sasa hivi iko umbali wa zaidi ya billion miles 15+ kutoka duniani. Yaani tukibadilisha kwenye kilomita tunasema zaidi ya kilomita billion 24. Hii ni namba ambayo akili yako haiwezi kuchakata vizuri.

Nikupe mfano rahisi uelewe. Ukituma signal kutoka Voyager 1 kuja Duniani inachukua masaa 22. Yani leo unatuma message saa 8 asubuhi, jibu linakuja kesho asubuhi saa 6. Hapo unaona umbali kiasi gani tunazungumzia.(Kunakuwa na network delay kwasababu ya huu umbali
Mwanga unasafiri kwa kasi ya kilomita 300,000 kwa sekunde, hiyo ndiyo kasi kubwa zaidi ulimwenguni. Lkn bado signal kutoka Voyager inachukua masaa 22. Fikiria hiyo umbali ni kiasi gani.

Noma sana hapa ndio niliposhangaa zaidi Technology ya 1970s(Oya ni hatari aise)
Nikisoma kuhusu computer iliyopo ndani ya Voyager 1, nilikuwa sijaamini. Jamaa hiyo spacecraft ina memory ya kilobyte 64 tu. Yani 64KB. Hata simu ya kabambe za zamani ilikuwa na memory zaidi kuliko hiyo. Smartphone yako ya sasa ina memory kubwa yaani million times zaidi kuliko Voyager 1.

Lkn voyager bado inafanya kazi perfectly!

Hii ndiyo ilinifanya nijipige maswali mengi sana. Wale engineers wa NASA walikuwa na akili ya aina gani? Yani walijenga kitu ambacho kitafanya kazi miaka 50+ bila kumgusa mtu, bila kupata update, bila kupata maintenance. Walijua kabisa hawana backup plan, hawana mbadala wa kutuma technicians kwenda kuirekebisha huko angani. Walipaswa kufanya kazi iliyonyooka sana mara ya kwanza tu.

Aise na walifanya exactly hivyo.

View attachment 3556224

Ujumbe Uliwekwa kwenye Voyager 1 kwaajili ya Aliens.
Kuna kitu kimoja ambacho kilinigusa sana ktk hii story ya Voyager. Wale wazungu walitengeneza kitu kinaitwa Golden Record. Hii ni disk ya dhahabu iliyorekodi sauti, muziki, picha na ujumbe kutoka Duniani.

Waliweka nini? Waliweka sauti za wanyama, mawimbi ya bahari, upepo, radi na sauti za asili nyingine. Waliweka muziki kutoka tamaduni mbalimbali duniani, classical music, rock and roll, na mziki wa asili wa Africa. Waliweka picha za watu, miji, wanyama, mimea na maisha yetu ya kila siku kwenye hiyo disk.

Kwanini walifanya hivi? Yani nikichukua muda kujifikiria kuhusu hii, inanigusa sana. Wale wazungu waliamini kuwa siku moja, labda baada ya miaka elfu au milioni, kiumbe kingine kikutana na Voyager huko angani na kitajua kuhusu sisi. Kitajua kuhusu binadamu, kuhusu maisha yetu duniani, kuhusu tamaduni zetu.

Haya ndio maono halisi mdau, kupanga kwa vizazi ambavyo hautaishi kuviona.

View attachment 3556221

Je Voyager inatumia nishati gani mbona ime-survive muda hivyo?
Hapa nilijifunza kitu kingine cha ajabu. Voyager 1 haitumii solar panels kama satellites za kawaida za sasa. Haitumii betr za lithium kama simu zetu. Mzigo unatumia kitu kinaitwa RTG (Radioisotope Thermoelectric Generator). Ni aina ya nuclear battery ambayo inatoa nishati polepole polepole kwa muda mrefu sana(Kama mnavyojua nishati ya nuclear ni ngumu mno kuisha).

Sasa hivi, miaka 47 baadaye, hiyo battery bado inatoa nguvu almost watts 249. Yani sawa na bulb mbili au tatu za nyumbani. Na hiyo nguvu ndogo kidogo ndiyo inayotumika kuipa nguvu component zote, kutuma data nyuma Duniani, kuendesha kila kitu.

Niliposoma hii nilijiona mdogo sana. Yani tunazungumzia betri iliyoundwa 1977 bado inafanya kazi 2026(😂). Simu yako ya sasa betri yake inadumu miaka mingapi? Mwaka mmoja? Miaka miwili? Lkn hiyo ya Voyager imefanya kazi miaka 47 bila shida.

Wanasayansi wanasema by 2025 au 2026 watahitaji kuanza kuzima baadhi ya sehemu ili kuokoa nishati ya chombo hiki. Lkn bado, tutaendelea kuzungumza na Voyager mpk karibu 2036 hivi. Yaani spacecraft itakuwa imefanya kazi miaka 59. Hii ni kitu gani sasa? 😟


Inaelekea wapi na kwa kasi gani?
Voyager 1 inasafiri kwa kasi ya kilomita 61,000 kwa saa. Kila saa inaenda mbali zaidi na zaidi kutoka kwa Jua letu. Inaelekea upande wa constellation ya Ophiuchus mbali angani.

Wanasayansi wanasema baada ya miaka 40,000 itapita karibu na nyota fulani huko mbali. Lkn hakuna mtu anajua itaishia wapi. Inaweza ikaendelea kusafiri milele, ikizunguka galaxy yetu, ikibeba ujumbe wa binadamu kwa siku zijazo.
Mwaka 2012 Voyager 1 ilifika kwenye interstellar space. Hii ni eneo gani ambalo binadamu hatujawahi kufikia. Ni nafasi kati ya nyota, nje kabisa ya solar system yetu. Ni chombo cha kwanza cha binadamu kuingia hapo.

View attachment 3556228
Picha ambayo itakushangaza kutoka Voyager 1.
Kuna kitu kimoja kingine ambacho kilinitia msisimko sana nilikuwa nafanya hii research. Mwaka 1990, mwanasayansi Carl Sagan aliomba NASA waondoe Voyager 1 igeuke nyuma ichukue picha ya Dunia. Yani spacecraft ilikuwa imekwenda mbali sana tayari, ilikuwa nje ya sayari zetu zote.

NASA wakafanya hivyo. Na picha iliyorudi ilikuwa ya kushangaza sana. Kutoka umbali wa billion miles 3.7, Dunia ilionekana kama pixel moja tu, kama vumbi kidogo kwenye ray of light. Carl Sagan aliita picha hii "Pale Blue Dot" nukta ya bluu iliyofifia.

Dah! akaandika maneno ambayo mpk leo yameniingia moyoni: "Look again at that dot. That's here. That's home. That's us. On it everyone you love, everyone you know, everyone you ever heard of, every human being who ever was, lived out their lives."

Hii picha ilibadilisha mtazamo wa watu wengi kuhusu umuhimu wetu hapa ulimwenguni. Tunadhani sisi ni wakubwa, tunajiona muhimu sana, lkn kutoka mbali kidogo tu sisi ni vumbi tu kwenye huu ulimwengu mkubwa.

View attachment 3556227
Nilichojifunza kwenye hii research.
Nilikaa nikafikiria sana kuhusu hii story ya Voyager 1, nikapata mshangao sana. Kwanza, wale wazee wa miaka ya 70s walikuwa na nidhamu na plan ambayo sisi leo hii tunaikosa kabisa. Walijenga kitu ambacho kitadumu vizazi.

Sisi leo tunajenga nini? Simu ambazo baada ya miaka miwili zinahitaji kubadilishwa. Magari ambayo baada ya miaka mitano yanakuwa outdated. Nyumba ambazo baada ya miaka kumi zinahitaji kurekebishwa. Lkn wao walijenga spacecraft ambayo bado inafanya kazi miaka 47 baadaye.

Pili, ancient technology si lazima iwe primitive. Yaani kitu cha zamani kinaweza kikawa bora kuliko cha leo kama kiliundwa vizuri. Voyager 1 ina technology ya miaka 47 iliyopita lkn bado inafanya kazi better kuliko satellites nyingi za leo ambazo zinazimika baada ya miaka michache.

Tatu, maono ni muhimu sana. Wale ma-engineer walipanga kitu ambacho kitasaidia vizazi ambavyo hawataviona. Walijua watoto wa watoto wao wataendelea kupokea data kutoka Voyager. Hiyo ndiyo maana ya kuthibitisha urithi wa kweli.

Changamoto tuliyonayo sisi
Mimi ni mpenzi sana teknojia, napenda kujua jinsi vitu vinavyofanya kazi. Lkn Aisee hii Voyager imenifundisha kitu tofauti kabisa. Hainitafundisha kuhusu ugumu, bali kuhusu uwepesi.

Dunia ya leo tunajifanya werevu sana sana. Tunaweka AI kila mahali, tunaweka features nyingi kwenye kila kitu. Tunaunda vitu vya complicated bila sababu. Lkn je tunaweza tukajenga kitu ambacho kitafanya kazi bila kusumbuliwa miaka 50? Suala kubwa sana.

Voyager 1 ilikuwa simple, ilikuwa na mission moja iliyonyooka, iliundwa kufanya kazi na kudumu. Na imefanya exactly hivyo kwa miaka 47. Hamna utani, hamna update kila wiki, hamna maintenance. Just pure performance ndio ina exist.

Hii ndiyo inanifanya nijiulize, sisi tunakwenda wapi na technology yetu ya sasa? Tunajifanya werevu lkn tunakosa basics ambazo ni muhimu. Tunajenga vitu ambavyo haviwezi kudumu. Tunakosa subira na usahihi.


Kwa wabongo wenzangu naomba msikilize
Hii story ya Voyager tuonaona kwamba tunaweza tukafanya mambo makubwa bila kuwa na teknolojia ya kisasa zaidi kama tunavyodhani. Tunaweza tukajenga, tukaunda, tukafanya kazi zenye quality bila shida.

Sio lazima mtu awe na computer ya hali ya juu. Sio lazima awe na vifaa vya kisasa sana.

Mimi nikikaa nikafikiria kuhusu hawa engineers(Wahandisi) wale wa NASA, ninawaheshimu sana sana. Hawakuwa na computer simulations nzuri kama ya leo. Hawakuwa hata na AI. Hawakuwa na GPT ya kuwaandikia code. Ilibidi kuhesabu kila kitu manually, kufanya tests nyingi, kufikiria scenarios zote zinazowezekana ili tu waje na product itakayo timiza maono yao.


Na walishinda. Waliunda kitu ambacho mpk leo kinafanya kazi perfectly bila shida yeyote, kinashinda hata technology mpya nyingi tu.

Namaliza hapa
Voyager 1 bado iko huko nje, inaendelea na safari yake ya milele. Kila siku inaenda mbali zaidi na zaidi, ikibeba ujumbe wetu, ikibeba matumaini yetu, ikibeba dhamira ya binadamu.

Na kila siku inatufundisha watu kwamba tunaweza tukafanya vitu vikubwa, vitu vya kudumu, vitu ambavyo vizazi vijavyo vitashukuru.

Mimi nimefanya research yangu, nimeelewa vizuri, na sasa nimejipa ahadi kuwa kila kitu nitakachofanya kitakuwa na quality. Sitaki tena kujenga vitu ambavyo baada ya muda mfupi ni kilio na vinahitaji kurekebishwa. Nataka kujenga vitu vya kudumu, kama Voyager.

Again I salute all you bosses, nimekaa sana kupiga huu uzi lkn naamini imekuwa worth it sana. Kama una maswali ama any additional tuwekee hapa chini, tutajadiliana.
je unajua kuna voyager 2, pioneer 1 and pioneer 2. Zote zimeshavuka solar system zipo interstellar area. Pia kuna new horizons imeshavuka pluto tiyari
 
Hiyo picha ya dunia hua inanipa mashaka kwamba hiyo tunayoiona ni dunia tuu na sio pamoja na jua na sayari zingine zinazozunguka jua.

Voyager 1 ipo umbali wa kilomita miles 3.7B, afu ipige picha ionekane Dunia tuu bila kuonyesha jua na sayari zake zingine? Sio kweli.

Hiyo picha Ilitakiwa ionyeshe sayari zote zinazozunguka jua na sio dunia pekee.

Anyway, hayo n mawazo yangu tu
 
😂😂
The farthest human made object in human history.

Kuna Voyager 2 pia ipo njiani.
Hiyo voyager 2 yenyewe imefika umbali gani kwa Sasa? Je na yenyewe namna ya kuchukua na kutuma taarifa ni Sawa na voyager 1?
 
Hiyo voyager 2 yenyewe imefika umbali gani kwa Sasa? Je na yenyewe namna ya kuchukua na kutuma taarifa ni Sawa na voyager 1?
Inasemekana mwaka Jana ilifika kilometer 20 billion. Yes Voyager zote zipo sawa ila zilikuw designed kwaajili ya mission tofauti.

Science says 1970's Kuna alignment ya sayari hutokea especially after every 127 years Sasa hiyo alignment ilitokea mwaka huo around 1977's wanatengeza hivi vivyombo voyager 1 imepita Jupiter na Saturn tu ila hii Voyager 2 ilipita sehemu ambazo voyager 1 haikupita though Voyager 2 imekuwa slow na imeweza kupita Jupiter, Saturn, Uranus na Neptune. Bado inaendelea na exploration.
 
Hiyo picha ya dunia hua inanipa mashaka kwamba hiyo tunayoiona ni dunia tuu na sio pamoja na jua na sayari zingine zinazozunguka jua.

Voyager 1 ipo umbali wa kilomita miles 3.7B, afu ipige picha ionekane Dunia tuu bila kuonyesha jua na sayari zake zingine? Sio kweli.

Hiyo picha Ilitakiwa ionyeshe sayari zote zinazozunguka jua na sio dunia pekee.

Anyway, hayo n mawazo yangu tu
Mwaka wa 1990 sidhani kama Voyager 1 ilikuwa imevuka Interstellar Region kwahiyo yeah the image is real na hiki chombo kinasafiri Ina relation to the earth orbit lengo ndio maana antenna yake inaelekea upande wetu lengo ni ili tuweze ku communicate Kuna path ambazo ni ndefu wangepitisha hiki chombo pengine delay ya signal zingekuwa kubwa.

Pia hii picha iliyoitwa Pale Blue Dot aliyeiomba alikuwa Carl Sagan haikuwa kwenye mission ya hii spacecraft. Katika kuchukua hii picha ni calculation zilifanyika sio random tu during this time Voyager ilikuwa imesha cross Neptune..
 
Yaanb kuna maswali najiuliza juu ya hawa wanasayansi na mainjinia wa nasa je,mawazo yao yanapokelewaga na ofisi gani bila kuwahisi wamechanganyikiwa(mf hawa jamaa wazo lao kupeleka icho chombo walimpelekea nani adi akawaelewa na kuwasapot maana kivyovyote kuna ukalibu wa mt aliechanganyikiwa na mwenye hayo mawazo) je walielewekaje kumbuka mwenye wazo anazungumzia kitu asichowai kukiona kwa macho yake ya nyama wala hana usibitisho na anaepewe maelekezo ya wazo kilakitu ni kigeni kwake
 
Tuje kwa mainjinia je wanawezaje kubuni vitu ambavyo dunian avipo na vifaa wanapata wapi? Maana mm kila ninachowaza na kufikili naona tayar kipo dunian yaan tayar ubongo umegota kuniletea vitu ambavyo avipo kwa macho yangu au milango ya faham
 
Yaanb kuna maswali najiuliza juu ya hawa wanasayansi na mainjinia wa nasa je,mawazo yao yanapokelewaga na ofisi gani bila kuwahisi wamechanganyikiwa(mf hawa jamaa wazo lao kupeleka icho chombo walimpelekea nani adi akawaelewa na kuwasapot maana kivyovyote kuna ukalibu wa mt aliechanganyikiwa na mwenye hayo mawazo) je walielewekaje kumbuka mwenye wazo anazungumzia kitu asichowai kukiona kwa macho yake ya nyama wala hana usibitisho na anaepewe maelekezo ya wazo kilakitu ni kigeni kwake
Curiosity na problem solving ndio inafanya watu waje na various inventions. Ukiangalia lengo la kutengeneza Voyager ilikuwa ni exploration ya sayari ya Jupiter na Saturn na lengo la wao kuweka vitu kama disks ni Imani yao. Wanaamini Kuna mahali Kuna intelligent living things kama Duniani na pengine hizo sayari zilikuwa na viumbe.

But thinking beyond our solar system wakaona Voyager 1 iwe kama utambulisho wa sisi kwenye sayari zingine.
 
Mada kama hizi wadau huwapati,wanataka mada za binti wa nini sijui

Anyways,niliwahi ona hizi documentary nadhani kuna muda huwa nahisi wazungu wamebarikiwa kwa kila kitu.
sema waafrika tumebarikiwa maana aliyekuwa komputer ya kibinamu mpaka mladi wa nasa kukamilika alikuwa mwenye asili ya afrika tena mwanamke nimemusahau jina
 
Kwa stahili hii apa duninan kuna watu vichwa vyao vina RAM 1T asee maana wanachakata vitu vizio mno visivyoonekana
 
Leo hii ikitokea any natural disaster ambayo itaua dunia nzima , kuna uwezekano baadhi ya Wazungu na waasia watafanikiwa kukimbia na kwenda sayari nyingine kuishi au wakaweza kujichimbia ndani kabisa huko ardhini na wanaweza kusurvive vizuri kabisa, ngozi nyeusi Huku Afrika labda tupewe lifti Tu ya kuokoa hii rangi Kwa maana ya watu weusi wawili watatu Tu kudandia Kwa msaada, mfano TZ Hapa hatuna maajabu, mifumo imetufunga na kutuharibu akili...

Kipindi Tuko tunapambana na Uhuru, kina Nyerere wanapiga bakuli na kina mzee sykes, USSR wanapeleka artificial satellite mwaka 1957 Sputnik 1...yaani Kipindi ambacho tunatembea peku watu tayari washaanza hizi harakati za kutembea anga za mbali kitambo.

Tukubali tukatae Sisi ngozi nyeusi hata kiakili ndio wa mwisho kabisa duniani, sasa Sisi tutaweza nini??....yaani vitu au stage ambayo wenzetu walishaipita Sisi ndo tunajiandaa kuzipita, typical primitive mindset, tuna kazi kushikana uchawi.
 
Sasa hyo picha ya hicho kifaa uko juu kapiga nani...?

Yaan 17,000 km per sec? Kivipi

Bado nasubiri hao NASA waende uko mwezini angali npo hai, na hii technology ya sasa nahisi ingekuwa rahisa sama kwao ila wanasema budget ndo kipengele ila budget ya vita kuuwa watu ipo.

Naami akuna kipya chini y jua..... ila NASA kamba nyingi sanaa
 
Back
Top Bottom