Usiwe mtu wa kuangalia makosa au madhaifu tu. Mara ngapi manula amefanya save za hatari ambazo angelikuwa kipa mwingine lingehesabika ni goli. Nakumbuka mashabiki wa Simba walipiga sana kelele za lawama kwa manula baada ya mechi ya Simba na Yanga kuisha kwa sare 2-2.
Ikapelekea kuwekwa benchi Manula na nafasi yake kuchukuliwa na Kakolanya. Kakolanya kila mechi aliyodaka kashindwa kupata clean sheet, watu watupia tu magoli lakini husikii lawama zinakwenda kwake watu wanyamaza tu kimya.
Au kuanza kulaumiwa mabeki. Anarudi Manula golini Simba wakapata clean sheet. ila mechi anazofungwa Manula hakuna anayeanza kutathmini mpira kwanzia kwa beki. Goli la leo mtu anaruka kichwa mbele ya mabeke, hawasemwi wanakuja kusemwa mtu wa mwisho ambaye ni kipa kisa tu katoka. Je mabeki walikuwa sahihi?