VPL: Yanga vs Polisi Moro,mechi ya ubingwa na kushuka daraja

VPL: Yanga vs Polisi Moro,mechi ya ubingwa na kushuka daraja

Hii sasa sifa! Thread inaanzishwa saa 36 kabla ya mechi?
 
Press release
Uongozi wa klabu Ya soka Ya Yanga unapenda kuwaalika wananchi wa Tanzania na Nchi jirani kuungana Basi kesho katika shamrashamra za ushindi wa ubingwa wa michuano Ya ligi kuu nchini.
Katika taarifa Yake kwenye vyombo vya Habari katibu Mkuu wa Yanga Dr Jonas tiboroha amesema wao Kama uongozi tayari wameanza maandalizi Ya kusherehekea ubingwa Kwa style ya tofauti Kabisa ambayo wataitumia katika mchezo wao wa kesho(jumatatu) dhidi Ya Polisi Morogoro kwenye Uwanja Mkuu wa taifa jijini Dar es salaam.
"Sisi kama Yanga tumejipanga Kwa style Ya tofauti Kabisa katika kuuchukua ubingwa wa ligi kuu na napenda kuchukua Fursa hii kuwakaribisha mamia na maelfu Ya watanzania Kutoka maeneo mbalimbali nchini kuja kuungana na sisi katika surprise Ya kuchukua ubingwa kesho"
Awali akizungumzia safari Ndefu Ya kuusaka ubingwa Dr tiboroha amesema wametoka Mbali kimafanikio Kwa kuweza kushinda Michezo Mingi na kilichobaki kesho ni kitu kitu kidogo Sana kwao kumaliza safari Ndefu Ya kuusaka ubingwa.
"Hatuwezi kula ng'ombe Mzima kisha tushindwe kumaliza mkia ambao sisi tutaula Kama supu"aliongeza tiboroha.
Kwa upande wake Mkuu wa ufarahiee ya Habari na Mawasiliano Ya Yanga,Bw jerry muro amesema tayari wanachama na viongozi wa Yanga Kutoka maeneo mbalimbali nchini wameanza kuwasili jijini Kwa ajili Ya kushuhudia mchezo wa kesho ambao kwao wameamua kuutoa Kama Zawadi Ya maadhimisho Ya Miaka 52 Ya muungano wa Tanzania na Zanzibar.
"Kwa Mara Ya kwanza Kabisa tunataka kuchukua ubingwa Kwa style ya tofauti Kabisa hivyo natoa wito Kwa wananchi na haswa mashabiki na wanachama wa Yanga popote pale walipo waungane nasi kesho kwenye shamrashamra za ubingwa"
Imetolewa na idea ya Habari na Mawasiliano Yanga-Makao Makuu
 
New updat: nimepata pesa ya kiinglio kesho uwanjani,na chenji itabaki hiyo nitkwenda kuitumia pale simba kapakatwa
 
Nataman "SAID BANUZI" aoneshe uwezo wake hapo kesho! kwa ushindi mnono na magoli ya mapema! pamoja na EDWARD CHRISTOPHER
 
Nafasi ya pili yetu

Mko nyuma ya Azam takriban pointi 7, mmejipanga vipi kuhakikisha kuwa ninyi mnashinda michezo yote na Azam anafungwa michezo 2 na kutoa sare mchezo 1? Kimahesabu ya kawaida, Simba hana chake hapo. Jichimbieni kwenye nafasi yenu ya 3!
 
Nataman "SAID BANUZI" aoneshe uwezo wake hapo kesho! kwa ushindi mnono na magoli ya mapema! pamoja na EDWARD CHRISTOPHER

Tamaa ikichukua mimba huzaa dhambi; dhambi ikikomaa huzaa mauti.

Si jambo jema kutamanitamani tu kila kitu hata kama huna issue nacho.
 
Ndoto za Alinacha, Simba akipata nafasi ya pili nitaomba mods wanipe ban ya mwez 1.........

Wanaota sana hawa Majizi FC. Simba kabakiza mechi 2 akishinda zote atakuwa na point 47. Wakati mwenzake azam kabakiza mechi 3 ana point 45. Inamaana kama azam akishinda mechi ijayo hawa mambumbumbu hawatapanda ndege kwa misimu mitatu mfululizo. Otherwise waombe azam afungwe mechi zote na wao washinde mechi zote.
 
Mechi hii ya leo uwanja wa Taifa inatarajiwa kuwa yenye mvutano mkali. Yanga inahitaji kushinda mechi hii ili kutwaa ubingwa wa soka nchini kwa mwaka 2014/2015.

Polisi Moro watataka kushinda kwa sababu mbili kuu. Mosi,kutaka kukwepa kushuka daraja. Na pili,kukwepa kuwa ngazi ya Yanga ya kutwalia ubingwa. Hakika ni mechi kali.

Wadau akina mkolaji Makoye Matale na wengineo watakuwa hapa kuwapa uhondo wa leo kutoka Uwanja wa Taifa Dar. Kama si Yanga basi ni Polisi Moro
 
Last edited by a moderator:
Tunachukua ubingwa kwa style ya aina yake leo.

Huu utakuwa ubingwa wa 25 wa ligi hii ni historia iliyotukuka.

Kwa ufupi Yanga ndio baba la Soka Tanzania.

Watani wetu njoo basi na nyie na record ya mapinduzi cup na mtani jembe.

Umefika muda sasa kila mtu nchi hii awe mshabiki wa Yanga.

Yanga Timu la Wananchi - Daima Mbele Nyuma Mwiko.
 
Mko nyuma ya Azam takriban pointi 7, mmejipanga vipi kuhakikisha kuwa ninyi mnashinda michezo yote na Azam anafungwa michezo 2 na kutoa sare mchezo 1? Kimahesabu ya kawaida, Simba hana chake hapo. Jichimbieni kwenye nafasi yenu ya 3!
Ha ha ha haaah.........mkuu Makoye Matale hata kujipa matumaini ni vizuri lolote katika soka linatokea.
 
Last edited by a moderator:
Tunachukua ubingwa kwa style ya aina yake leo.

Huu utakuwa ubingwa wa 25 wa ligi hii ni historia iliyotukuka.

Kwa ufupi Yanga ndio baba la Soka Tanzania.

Watani wetu njooni basi na nyie na record ya mapinduzi cup na mtani jembe.

Umefika muda sasa kila mtu nchi hii awe mshabiki wa Yanga.

Yanga Timu la Wananchi - Daima Mbele Nyuma Mwiko.
 
Mfungwa hachagui gereza, polisi moro leo atake na asitake kipigo kiko pale pale. Yanga kama yanga tunajua polisi Moro watajituma sana mechi ya leo ili wasifungwe na yanga ili kukwepa kushuka daraja lakin hilo halitaizuia timu bora tanzania na afrika mashariki kutoa kipigo kwa maafande hao wa Morogoro.

Kila la kheir yanga afrika.

YANGA DAIMA MBELE NYUMA MWIKO.
 
Back
Top Bottom