VPL: Yanga vs Polisi Moro,mechi ya ubingwa na kushuka daraja

VPL: Yanga vs Polisi Moro,mechi ya ubingwa na kushuka daraja

Historia inaenda kuandikwa leo uwanga wa taifa, Yanga kuchukua ubingwa na Polisi Moro kushuka daraja
 
Nikiwa Nimenyong'onyea Kwani Sina Jinsi Napenda Mchezo Wa Soka ILA Wasiojua Mpira Leo Wanatawazwa Japo Maji Hakuna Kuwa Mabingwa Wapya Wa Ligi Kuu Ya Tanzania VPL. Wanasimba Tutabaki Kuumia Shingo Tu Tukiona Wenzetu Kila Mwaka Wakipaa Angani Na Ndege.........Inauma Mno Lakini Ndiyo Hivyo Tena. Lakini PIA NAOMBA NITOE OMBI LANGU LA DHATI KWA Wana Yanga Wote Ndani Na Nje Ya Nchi Kuwa Hebu TUNAOMBA MTUSAIDIE MUWEZE KUWAFUNGA Azam FC Ktk Mtanange Wenu Wa Wiki Ijayo Mkishatoka KUPIGWA ( Kufungwa ) Magoli 11 - 0 Na Etoile Sportive Du Sahel Jumapili Ijayo. Kama MKITUFANYIA Wena Huo Basi Sisi Wana Simba Wote Tutarudisha Ule Udugu Wetu Na Nyie. Naipenda Sana Yanga ILA Nawapenda Kuliko Maelezo Etoile Sportive Du Sahel.

Hongereni Wana Yanga Kwa Kuwa MABINGWA Leo Jioni Na Tukutane Taifa!!!!!!!!
 
Historia inaenda kuandikwa leo uwanga wa taifa, Yanga kuchukua ubingwa na Polisi Moro kushuka daraja
Maskin polisi moro leo ana kibarua cha kukuta shina la mbuyu kwa kisu!!!!
Kwa heri polisi moro ligi kuu ila usijali yupo mwenzako anakuja huko si nyingi, kama si ndanda ya mtwara basi tz prisons ya mbeya.

R.I.P POLISI MOROGORO
 
Mbeya city nilijua lazima washukie mwaka huu lakini wamekomaa mpaka sasa wapo nyuma ya mikia fc nafasi ya 4. Wale jamaa wakijipanga vizuri hakika mwakani watakuwa tishio sana, mwaka huu nadhani kuna mambo hayakuwa sawa kwenye club ila sio siri wana wachezaji wazuri sana halafu vijana sana.Niliona kwenye mechi na sisi Yanga pale taifa kiukweli wako vizuri japo tuliwafunga 3
 
Manji akijiongezea muda wa uongozi,wanachama wengi walipinga,yeye aliwaahidi ubingwa kwa namna yeyote,mechi nyingi walizoshinda Manji alinunua Ili tu kuwafanya wanachama/washabiki wafurahi..mpira wa nchi hii hauwezi kusonga mbele Kama Kuna watu wanapata matokeo nje wa uwanja...
 
Kikosi cha Yanga (mabingwa watarajiwa) wa msimu wa 2014/2015 kitakachoanza leo dhidi ya Polisi Morogoro (washuka daraja watarajiwa) wa msimu wa 2014/2015.
1.Deogratius Munishi "Dida"
2.Juma Abdul Mnyamani
3.Oscar Fanuel Joshua
4.Mbuyu Junior Twite
5.Kelvin Patrick Yondan "Vidic"
6.Said Juma Makapu
7.Simon Happygod Msuva
8.Haruma Hakezimana Niyonzima "Fabregas"
9.Amiss Jocelyn Tambwe
10.Mrisho Ngassa "Anko"
11.Kpah Sean Sherman

SUBSTITUTIONS---
Alphonce Matogolo
Andrey Coutinho
Rajabu Zahir
Edward Charles Manyama
Danny Mrwanda

Kocha mkuu-
Hans van der Pluijm

Kocha msaidizi-
Charles Boniface Mkwasa

Daktari wa timu-
Juma Sufiani

Meneja wa timu-
Afidh Saleh

Kila la kheir kwa mabingwa watarajiwa dar young africans.

YANGA DAIMA MBELE NYUMA MWIKO..........
 
Wa mchangani tunawakaribisha kwenye sherehe leo uwanja wa taifA,hatiwanyanyapai
 
Manji akijiongezea muda wa uongozi,wanachama wengi walipinga,yeye aliwaahidi ubingwa kwa namna yeyote,mechi nyingi walizoshinda Manji alinunua Ili tu kuwafanya wanachama/washabiki wafurahi..mpira wa nchi hii hauwezi kusonga mbele Kama Kuna watu wanapata matokeo nje wa uwanja...
Kama Aveva alivyofanya kwa tz prisons, alinunua goli 5 ili asubuhi yake kwenye mkutano na wanachama wasimuulize chochote kuhusu mwenendo wa timu yao.
Tena usiendelee kuongea sana nitayasema mliyoyafanya juz kwa ndanda ya mtwara, ushahidi ninao wa muamala wa M-PESA.
 
GENTAMYCINE;

Mkuu unapitia moja baridi moja ya moto!!!!
Manake naona kama umeamka nazo vileeee.,
Kwa taarifa yako yanga inaenda kumtolea mwarabu kwao mbele ya mashabiki wao na wake zao.
 
Last edited by a moderator:
Jamani kama kuna link itaonyesha huu mchezo au redio tupeane. Mchezo muhimu sana
 
ulichotakiwa kufanya ni kuiombea yanga ushindi huko arabuni ili ikirudi hapa iwe na morali ya kuendeleza wimbi la ushindi dhidi ya azam!
 
Jamani kama kuna link itaonyesha huu mchezo au redio tupeane. Mchezo muhimu sana
Mchezo utatangazwa moja kwa moja kutoka uwanja wa taifa kuanzia majira ya kumi kamili jioni na TBC TAIFA.
Utaoneshwa LIVE na azam tv, wenye link watanisaidia kuiweka hapo.
 
Back
Top Bottom