Vurugu Kituo cha Mwendokasi Kimara Temboni, abiria ashambuliwa

Halafu wako bize wanajenga mfupa mwingine njia ya bagamoyo.

Hivi kwa nini wasingejenga njia sita au nane kabisa mpaka pale bunju.

Mtu kutoka bunju kuja mwenge unatumia dk 8 tu.

Nje ya mada:

Hivi mainjinia wa mwendokasi, kuna ulazima upi wa kujenga vituo vireeefu maeneo ambayo hayana historia ya kuwa na abiria wengi?

Mfano hivyo mnavyojenga lugalo.
Kwakweli hili jambo linashangaza sana
 
Vurugu zimeibuka katika Kituo cha Mabasi ya Mwendokasi cha Kimara Temboni, baada ya kile kinachodaiwa kuwa ni ukiukwaji wa utaratibu wa kupanga mstari kwa abiria.

Tukio hilo limetokea leo Februari 25,2025 majira ya saa 8:40 asubuhi ambapo lilianza pale abiria walipovunja mstari rasmi wa upanda wenye magari hayo na kuanzisha mstari mwingine baada ya basi walilokuwa wakilikimbilia kujaa. Hali hiyo ilisababisha mvutano kati ya abiria na maafisa wa usafiri wa mabasi hayo, huku baadhi ya abiria wakidai kuwa hawawezi kupangiwa namna ya kupanda kwenye basi.

Katika purukushani hizo, abiria mmoja alijeruhiwa baada ya kupigwa na maafisa wa Mwendokasi wakishirikiana na dereva wa basi hilo liifika atika kito hicho lenye namba za usajili T 544 DWR.

Mwandishi wa Nipashe Digital, alikuwa mmoja wa abiria katika kituo hicho na kushuhudia tukio hilo. Mmoja wa abiria alijaribu kutuliza hali kwa kuwaomba maafisa hao pamoja na dereva wampeleke abiria huyo waliokuwa wakimshamulia kituo cha polisi badala ya kumpiga. Dereva wa basi hilo alishuka kwenye gari na kumkaba abiria uyo aliyetoa shauri, jambo lililozua taharuki zaidi.

Tukio hilo limezua mjadala kuhusu changamoto za huduma ya Mwendokasi, ambapo abiria wengi wamekuwa wakilalamikia ucheleweshaji wa magari na msongamano mkubwa wa abiria hasa wakati wa asubuhi.

Aidha, kumekuwa na malalamiko kuhusu tabia ya baadhi ya maafisa wa taasisi za umma kujichukulia sheria mkononi na kutumia nguvu kupita kiasi, jambo ambalo linakinzana na misingi ya utoaji wa huduma kwa wananchi.View attachment 3249007View attachment 3249008View attachment 3249009
Duh!...Usafiri wa umma ndani ya hili Jiji ni changamoto kweli kweli.
 
Kujichukulia sheria mkononi ni janga.....

Tuna "STRESS" nyingi za maisha na uungwana ni kuwa na kiasi panapo changamoto....
 
Kero kubwa ni kutoleta magari kwa wakati vituoni, mtu anasimama dk 40 na gari ikija ishajaza kupita kiasi.

Wanatakiwa basi zingine zianzie katikati ya vituo kupunguza abiria sio kila basi linaanzia mwanzo.
Kweli kabisa.
Hoja yako ya gari zingine kuanzia vituo vya kati nzuri sana.
Ndugu zetu vituo vya kati wanateseka sana na kuchelewa kufika kwenye majukumu yao.
 
1740475754091.png

Top right Corner: Mchina mweusi nadhani alifuatwa kwenye eneo lake. Ukiangalia picha hizi
 
Wakati mwendokasi unaanza rasmi ,mtaani na katika viunga vya jiji la Dar es salaam zilienea habari kuwa madereva wote wa mwendokasi wametokea kwenye vikosi vyetu vinavyoanzaga na KJ .

Sasa nauliza itakuwa ni kweli wanajukwaa maana hapo juu kwenye picha nahisi huyo jamaa mwenye Shari jeupe ndiye dereva maana karuka teke matata Sana
 
Wakati mwendokasi unaanza rasmi ,mtaani na katika viunga vya jiji la Dar es salaam zilienea habari kuwa madereva wote wa mwendokasi wametokea kwenye vikosi vyetu vinavyoanzaga na K
 
CCM hao,Mwendokasi chaliii,Ndegeza ATCL chali sasa bado treni
 
Nimeshawahi kuishi kwenye nchi yenye Umafia mwingi, undava mwingi, lakini inapokuja kupanga foleni Kwa ajiri ya usafiri, basi hata Gangstas ama mshenzi na muhuni yoyote, na anaweza kuwa na Bunduki kiunoni, atapanga foleni, hata kama foleni ni ndefu kiasi Gani, ila atapanga foleni.

Gari ikija, Ataingia abiria mmoja mmoja kwenye Bus bila vurugi, Wala haraka, ni polepole
 
Kero kubwa ni kutoleta magari kwa wakati vituoni, mtu anasimama dk 40 na gari ikija ishajaza kupita kiasi.

Wanatakiwa basi zingine zianzie katikati ya vituo kupunguza abiria sio kila basi linaanzia mwanzo.
Huu ushauri ni mzuri kabisa.
 
Back
Top Bottom