Vurugu Umbwe-Lyamungo: Miaka 12 baadae

Hizi shule mbili hizi zikikuwa hatari sana,yani wale wote waliosomaga hizi shule mbili mpaka Leo no wahuni tu na uzee wao.
 
Lyamungo walishawahi kuleta noma shuleni kwao kisa wamepikiwa ugali siku ya wali viongozi wa vurugu wakafukuzwa kisa wali
Jamani Shule za Boarding za Enzi hizo ilikuwa Raha Sana. Shule zenyewe zilikamilika. Mzungu alisema na tujenge Shule na ikajengwa Shule kweli. Mabweni Safi, Dining hall yenye kila kitu, Kitchen, Classrooms, Conference room, Chapel, Laboratory, infirmary, viwanja vya Michezo, Gardens, Staff rooms, Headmistress/ headteacher room, library, store, toilets and bathrooms zenye showers na flash toilets, fire place darasani Eneo la baridi, vioo vya Lucas au vya kufunga na kufungua, Sewage System Bora kabisa. Daaah nazikumbuka hizo Shule chozi hunitoka zilivyoharibiwa na Sisi.
 
Wadau wa Sanaa ya filamu waone hii fursa watengeneze movie kali wawekeze bajeti nzuri watapiga mpunga mzuri tu
 
Lyamungo walishawahi kuleta noma shuleni kwao kisa wamepikiwa ugali siku ya wali viongozi wa vurugu wakafukuzwa kisa wali
Mkuu hapa kulikuwa na ka likikzo kama wiki 2 hivi sisi wa mbali na wengine ambao hawataki kwenda home tukabaki, sheria ikapitishwa kuwa ili ule lazima uwe umefanya kazi ya kusomba kuni na huko huko kazini mwalimu na viranja wanoko wanakupa kuponi ambayo ndo tiketi yako ya kuingia jikoni, hatujakaa sawa Headmaster Sanga akatangaza kuwa kipindi chote hicho cha likizo hamna kula wali! Vijana tukaona miyeyusho usiku mapema sana tukaenda kwa headmaster tukamsaidia kushusha vioo vya nyumba yake chini! Kesho yake defender kama 3 na FFU waliovalia zana zao wakatupa nusu saa ya kuondoka na hawakutaka hata mtu aache kivuli chake! Kwakweli mm sikwenda kwetu maana nlipiga hesabu ya 120k kwenda na kurudi nikaenda kwa mshikaji wangu kule Uchira tukapata dili la kupalilia mahindi heka moja 40k na kunyunyizia dawa, knapsack spray 1 tsh 3000, likizo ikaisha nikiwa don ila kwa sababu ya ujinga sikuchukua tahadhari wkt wa kupulizia dawa nikababuka mgongo wote! Nilirudi shule nikiwa na nido, sukari, blue band za kutosha room ilkuwa happy sana! Nilikuwa nakaa bweni la Aggrey[emoji1787][emoji1787]
 
Tuliosoma boarding school za serikali kulikuwa na raha yake sana
 
Kweli kabisa Mkuu, shule kama Umbwe, lyamungo, Galanos etc ambazo nimewahi Fika ni shule za kisasa sana, hadi swimming pool ina heater. Ukuta ukiangalia tech yake huikuti mtaani.
 
Hawa wa Tambaza na Azania tulikutana nao Old Moshi miaka hiyo (siku hizi Moshi Sec) walimu wa kike walikuwaga wanaogopa kwenda kuwakagua usafi bwenini. Walikuwa wagumu na wasioogopa kitu chochote bangi nibangue. Hapo baada ya kizazi chao kuondoka ndipo tukaanza ugomvi binafsi na Umbwe kwenye kugombania mademu wa Kibosho Girls, Weruweru na Machame Girls...Mademu walikuwa wanatupenda sisi kwasababu tulikuwa tunapiga perfume na nguo za kisasa, Jamaa wa Ubwe walikuwa wanakunywa mbege sana na kuberi na hawajui kutongoza, walikuwa wanalazimisha
 
Ni bahati pia kuwa nilisoma Lyamungo Sec A Level...ni miongoni mwa mwanafunzi aliyekuwepo kwenye form five ya kwanza mwaka 2001, July. Mwalimu Mkuu alikuwa Bureta na Nidhamu alikuwa Mwalimu Shoo.
 
Ukiweka point ya kubebana kimehesabu inawezekana; Yale mabweni ya lyamungo cabin moja watu nane ambao hawajabebana, chukua 160 Mara nane nyingine ambao wababebwa jumla 900+ kwa bweni moja Mara nne inakuja elfu tatu na ushee uko
 
Mkuu uzi wa masikitiko kweli, ungetuelezea polisi walichukua hatua gani?
 
Machame inatenganishwa na mto. Hivo kwa ninavojua mimi lyamungo ipo kibosho machame ni mpaka uvuke mto uliopo chin ya lyamungo kutoka kijiweni so sidhani kama lyamungo ipo machame
Lyamungo ni machame, umbwe ni kibosho ule mto kombo ndo unaotenganisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…