Wanabodi,
Juzi katika kikao cha bunge, Spika wa Bunge, Mhe. Anne Maklnda, alimtaja Mbunge wa Singida, Mhe. Tundu kama ndie Mbunge anayeongoza kwa kuwa chanzo cha vurugu za bungeni, kwa kuongoza kwa utovu wa nidhamu, kuleta fujo na vurugu bungeni, hali ambayo sio tuu inahatarisha hali ya utulivu, amani na usalama wa bungeni, bali pia kumevuruga ratiba za Bunge kulikopelekea Spika kufuta baadhi ya ratiba za Bunge ambazo zilikwisha ridhiwa na kuingizwa kwenye order paper ikiwemo kupokea hoja binafsi za wabunge, kwa kilichoelezwa kuepuka vurugu zaidi.
Jana kikao cha kamati ya Uongozi kimekaa kujadili hali hiyo na matokeo yake, tutayapata kesho asubuhi baada ya kipindi cha maswali na majibu ya papo kwa papo kwa PM!, ni hakika rungu la kiti, lazima litamshukia Mhe. Tundu Lissu!.
Swali la kwanza ambalo wengi mtapenda kujiuliza ni, ni jee ni kweli, Mhe. Tundu ni mtundu na ndie chanzo cha utovu wote wa nidhamu wa bunge hili la kumi kama anavyoelezwa na Madam Speaker?!, au huo utundu wa Mhe. Tundu, sio utundu bali ni uzingatiaji wa kanuni za Bunge, kufuatia Mhe. Spika, kuonyesha udhaifu mkubwa katika kuliendesha Bunge kwa kutokuzingatia, sheria, taratibu na Kanuni?!.
Kwa vile mimi ni mmoja wa watu tunaomfahamu Mhe. Tundu, Tangu toka akiwa Shuleni, Ilboru (sio darasa moja, Nikiwa A-level, yeye alikuwa O-Level) naomba kuchukua fursa hii kumshauri na kumfariji Mhe. Spika, kwa kumuomba asiumize sana kichwa chake kuendelea kubishana na Mheshimiwa Tundu Lissu kuhusu kanuni za Bunge, au kitu ambacho Lissu ana uhakika nacho, wala wasipoteze muda kumuadhibu kwa jambo ambalo liko wazi kabisa na udhaifu unajulikana ulipo tangu chanzo chake, ulipo sasa na labda utaendelea kuwepo, hata Lissu akiadhibiwa vipi, kwa sababu Mhe. huyu ni mbishi hakuna mfano!, haswa pale anapokuwa na uhakika kuwa yuko right!.
Nashauri Mhe. Spika, lazima ufike mahali, umkubali huyu jamaa kuwa lile jina lake la Tundu, sio jina tuu, huyu bwana analiishi jina lake kwa kuwa ni mtundu kikweli pale anapogundua kuwa kanuni zinakiukwa na zinapopindishwa ili kutoa mteremko kwa upande fulani!.
Nimebahatika kusoma na Mhe. Lissu shule moja kule Ilboru, (sio darasa moja) miaka hiyo enzi za Mkuu mmoja aitwae Mwalimu Mushi, kwa jina la utani, Bino!. Huyu Bino alikuwa ni mwalimu mkuu bingwa wa nidhamu, ila kwa Tundu, alinyanyua mikono juu na kishs kuishusha chini, baada ya kuthibitika kuwa japo Tundu alikuwa "toto tundu", ila pia ndie aliyekuwa kipanga wa darasa lake!, kwani pepa alikuwa akizifumua, utadhani mtihani katunga yeye!.
Tundu Lissu alijiunga shule ya vipanga ya Ilboru akitokea Singida, wakati huo shuleni akiitwa Antipasi Tundu, na alikuwa ni mtoto mtundu kweli!. Wakati huo, O-Level ya Ilboru ilichukua wanafunzi wenyeji wa Arusha, Singida na Shinyanga!. Sisi Wasukuma tukiitwa "Wasukusu", wenyeji wakiitwa "wamenye" huku jamaa wa Singida wakijiita watu wa "Singapore", uji ukiitwa "sumu", na nje kulikuwa na kaduka kwa "Akwii".
Utundu wa Tundu Lissu ulkikuwa ni kwenye mishe mishe tuu hizi za zile, haijulikani alikuwa akisoma muda gani na kwa saa ngapi, ila pepa zikija, anafumua ile mbaya kama mitihani katunga yeye!.
Moja ya maeneo ambayo Tundu Lissu alikuwa ni mtundu au tusema ni mbishi, ni kwenye school debate!. Tundu akishakuwa na uhakika yuko right and on the right track, ni mbishi hakuna mfano!.
Hata mimi nami sikuwa malaika, nilikuwa na matatizo yangu tangu shule, yale matatizo ya kawaida ya Wasukuma wa Chapa Ng'ombe, unapokutana bidhaa adimu za vibinti vya vyeupe vya Kiarusha pale Mlimani Ilboru, ukijumlisha na lile baridi kali la Ilboru , tena wakati huo, "bwawa bado halijaingia luba!'...
Tundu Lissu aliondoka Ilboru na wani kali, akaenda Galanos hatimaye UDSM. Sisi na vilaza wengine tukaishia kwenye vile vyuo vya mashenzini!. Tulipoteana kwa kipindi cha miaka 10!, tulikuja kukutana tena jijini Atlanta, nchini Marekani, yeye akiwa na yake nami nikiwa na yangu, ndipo akanieleza sasa yuko LEAT, na huko aliichachafya serikali vivyo hivyo kama anavyo mchachafya Madame Spika, kwa kumsulubu bila huruma!.
Pamoja na utundu wote huu wa Mhe. Tundu Lissu, was dam good academically. Hivyo wakati tukisubiria kusikia ni adhabu gani itamfika hapo kesho, kuna maswali matatu tujiulize!.
- Jee ni kweli Mhe. Tundu Lissu ni mtundu kihivyo na ndie mbunge anayeongoza kwa utovu wa nidhamu hadi kustahili adhabu kali?.
- Au ni Spika ndiye dhaifu hadi kushindwa kusimamia kanuni, kuliendesha Bunge kwa haki hivyo Tundu Lissu akisisitiza kufuatwa kwa kanuni, anaonekana kama analeta vurugu?.
- Baada ya kuthibitisha, Mhe. Tundu Lissu alikuwa ni mtundu toka shuleni, jee nani wa kubadilika kati ya Mhe Tundu Lissu na wabunge wa upinzani, wakae kimya wakati sheria, taratibu na kanuni, zikikiukwa, na kupindishwa?, hivyo kumpatia fursa Mhe. Spika kujiendeshea Bunge anavyotaka, ili kudumisha utii, na nidhamu ili Bunge liwe la amani?.
- Hivyo Mhe Spika kuwathibitishia Watanzania kuwa hata yeye ambaye ni Spika wa majaribio ya "jinsia" "ameweza" kuliendesha bunge vizuri tuu, ambalo ni mhimili mmoja wa dola, hivyo jee, 2015, tukamilishe majaribio ya "jinsia" kwa mihimili miwili iliyobakia?, ili nchi yetu iwe ni nchi ya usawa halisi wa kijinsia?.
Wasalaam
Paskali
(Skulu Meti wa Toto T).