Vurugu zaibuka msiba wa watoto matajiri wa Arusha, mwandishi wa Ayo TV anyang'anywa camera

Hawa waandishi wa udaku hovyo sana, watu wana majonzi wewe unakwenda kuwahoji na kuwarekodi ili upate udaku wa kupeleka kwa mange kimambi. Amekipata alichokistahili na liwe fundisho kwa wadaku wengine
 
Kuna misiba ya kitaifa na misiba private unapaswa kutofautisha
 
Kuna tofauti kati ya 'kifo' na 'msiba' - wewe ilienda kwenye 'msiba' na sio kwenye 'kifo'
 
Kila anaefariki Arusha utaskia mtoto wa tajiri ina maana mji mzima hakuna maskini. Ule mji wa kiboya Sana wanapenda kusifiana ujinga mda wote. kama kweli wanaweza waje mjini apa DSM tuoneshane umwamba
 
Acha wivu wako tajiri utajiri haufichiki mkuu!, usemalo sio kweli.
Sijajua umenisoma vipi mkuu, lakini nimewahi kutembelea na hata kukaa mikoa hiyo ya Wachaga. Ukimtendea wema hasa ukimnunulia pombe mara kwa mara atakusifu kuwa wewe ni tajiri kila sehemu. Hakuna wivu hapo na wala sijamaanisha huko hakuna matajiri.
 
Ni sawa, publicity ya nini mambo ya huzuni
 
Habari haijasema Kama mwandishi alikuwa ameanza coverage Bali alikuwa ndio anafika msibani, au Mimi ndio nimewaka ?

Kama Ni hivo nilivoelewa Basi Ni kosa kumnyang'anya vifaa vyake
Unaenda msikitini na nguruwe uachwe sababu hujaanza kujenga banda lake?
 
Taarifa za ajali zinapatikana eneo la ajali na Trafic. Sio kusumbua watu msibani ikiwa hawapo tayari.
 
Hapa ndipo mzee wetu kinana nadharia yake ina bounce, nafikir ni muhimu trafik wamepo mpaka night ...
Tatizo ni mwendo kasi. Kama abiria na madereva tukijilinda bila kusubiri serikali itulazimishe ajali zinaepukika na kupungua.
 
Bladifaken hawa waandishi wa online tv,unaenda kuhoji msibani mtu kafiwa ili upate nini?wakamhoji january makamba kwanini umeme unakatika hovyo kila siku
 
sasa huyo mwamba nae watu wako msibani anaenda na makamera yake,kama ripoti ya ajali si aende polisi au siku hizi utaratibu umebadilika.
Hawa waandishi wa online tv ni hovyo kabisa
 
Huwezi kwenda msibani hata kama ni mwandishi wa habari bila ya idhini ya wenye msiba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…