Mamlukii
JF-Expert Member
- Dec 1, 2021
- 1,063
- 2,387
kwanini mkuu?wewe ungekua south ungekufa wa kwanza
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
kwanini mkuu?wewe ungekua south ungekufa wa kwanza
Kwani kuna Mzaramo mwenye duka kariakoo?KWani wazawa hawana biashara huko mpaka nyie mkifunga mpaka wafate town bidhaa au huduma??
Ndg hakuna chenye thamani zaidi ya maisha.Kesho yake pakatulia sio wao wala sisi kuonekana kiwanja cha vitaa
PART THREE-MWISHO
Mji ulikuwa kimya sanaa hiyo kesho yake ambayo walisema ni kiwanja cha vita kitajaa damu- hakikia na yeyote mabarabarani, kulisikika milio ya magari tu na hakuna yeyte nje kila mmoja alijifungia kwake
Kesho kutwa yake tena kimya na wiki nzimaa ilikuwa kimyaa
My friend tukajadiliana hapa haina haja ya kuambiwa tufungue maduka yaani tujifungulieni tu kwani tumeshawaweza na hawawezi fanya chochote kilee
Tukafungua- wakaanza choko choko siku hiyo hiyo tukasema hatufungi ila tunawaudumia wateja wetu nje? Ya bagla yaani , wateja hawatoingia mpaka ndani dukani tutawahudumia kama maduka ya bongo, huku huwa wanaingia dukani wanachagua vitu then wanakuja tunawapigia mahesabu alaf wanalipa dzain kama ya vimin market vilee,haikuwa hivyo ikawa tunawahudumia kama bongo vilee
Ila kuna wabishi walikuwa wanawaachia waingie wajichagulie na ilikuwa fursa tena kwa vibaka katika wiki hiyo hiyo
Kuna duka wameingia vibaka na kupola pesa na kumpiga shaba mtoto wa kiarabu/kiethiopia na kumuua ila walikuwa wezi tu sio hao wenye mgomo hatimaye wakakamatwa wakaenda jela- sema inasemekana kesi ya kuua sio kesi Kwa South Africa kwamba walikuwa wawili katika upelelezi akaachiwa mmoja Kwa maana yeye siyo aliyempiga bunduki ila mwenzake amenyea ila wanasema anaweza akakaa miaka miwili tu then akatoka ila waethiopia waneapa akitoka asirudi mitaa hii kwani nayeye watampeleka alipompeleka mwenzake yaani watampiga bomba nayeye, yule mmoja tunasikia tu ametoka ila hayupo mitaa hii itakuwa amehamishwa mji
Na uwezi amini hao watoto waliomuua huyo jamaa walishawahi kuja dukani kwetu wakataka waibe tukawashitukia, tukataka tuwachape tumewakolomea tu tukawaacha maana kujenga vichuki vidogo vidogo sio inshu kabsa, maana hata ukiwakazia kuwapa sigala wakilalamika hawana kitu wanaweza wakaja kukupiga bomba yaani chuki tu mwananga sio maisha kabsa south africa hapafai kabsa yaani tupo tu Kwa ajili tumeshaanzisha maisha
KIKANUKA TENA SERIOUSLY HIYO WALIOSEMA WANAKINUKISHA
tuliambiana tufunge biashara yukafunga, wakakusanyanaa mitaani na kuanza kuchoma mapira wana mapanga na malungu na Safari hii walikuwa wengi sanaa
Sisi kama kawaida tukashituana kuwa vita imerudi tena na uzuri mahojiano ya siku ilee halifika sehemu husika so kulikuwa na asikari maalumu wapo doria
Wakawakamata ma- icon wao kama kumi , kumi na mbili hivi, yaani waliwakamata walee waanzilishi wa vurugu wakawatia ndani lakini tulikuwa tayari kwa vita , yaani tulikuwa tayari kwa chochote
Ila binafs nilishukuru kuona pambano lipo off Kwa leo nilishukuru
Walee wengine wafata mkumbo kuona wenzao wamekamatwa wakakimbia
Tukaambizana kilichoendelea tukatudisha silaha kwenye ala zake
Nna mpaka video ila sitaweza kiwawekea hapa mtandaoni
Vitaa ilisimama hivyoo- wajamaa hawajatoka mpaka leo kesi kila siku inapelekwa mbele wanaenda kama wachochezi wa vurugu
ila ninachokiona ili balaha likirudi tena itakuwa nomaa sanaa yaani watakufa watu yaani hapa nna mpango wa kujichanga kama Mil 10 , nitokomee canada/ popote pazur ila ndio nakichanga
Baada ya hili balaa- kuna baadhi ya wabongo ambao hawakuvunjiwa maduka yao, wameuza biashara zao na kwenda Tanzania kuanza maisha mengine nanasikia wengine waneshapata visa wapo zao canada huko , yaani hapa ndonga linauma nitoke hapa SA nitafute kiwanja kingine- ila ilee kutoka moyonisiogopi chochote kilee sio kuhusu tunavyopondwa watu wa SA wala hayaa maisha ya bastola kila siku sihofii chochote kilee
Ninachohofia kupoteza biashara yangu tu I wish nipate mteja niiuze nitokomee zangu makanada huko
Najifunza vingi sana na ukifikiria nna 29 yaani na naendelea kujifunza
Kuhusu kuuza biashara wasomali na waethiopia hawaogopi chochote ukitaka kuuza wao wananunua tu wao wapo tayari kwa lolote nipo kwenye mafikirio ya kuuza ila ngoja kwanza niangalie upepo
MWISHO [emoji1478]
Kuna mengi sijayaweka katika maisha ya kila sikuya South Africa
Nimeshatolewa bunduki mara mbili na kutolewa kisu mara moja ki ukweli ni maisha ya roho mkononi, karibu sanaa SA
ASANTUM- tupo sanaa maisha hayaa ila ikimpendeza M/Mungu atujaalie tutusue twende zetu CANADA HUKO-InshAAllah [emoji1431]
Simama Juu ya meza hapo sebuleni ujipige kifua nakupaza sauti kwa kusema MIMI NI KENGE.Msalimie shibekijijini
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Simama Juu ya meza hapo sebuleni ujipige kifua nakupaza sauti kwa kusema MIMI NI KENGE.
Kama unadhani ni lazima ufanye maisha yako South Africa basi hakikisha hauishi location.
Kama unaishi location IPO siku yako utazikoga risasi za kutosha tu, msidanganyane.
Mcongo hawezi kushindana na mbongo Kinondoni eti kisa Kinondoni kuna Wacongo wengi, mnadanganyana, tutaendelea kupokea maiti zenu airport.
Vingine anapanga shetani usiwe mjinga.Sitaki kudharau maneno mazuri uliyoniambia ila ukweli ni kwamba mtu anakufa popote sio sisi tu ambao tunapigwa risasi hata na wao wenyewe wasouth wanauana Kwa risasi mfano AKA.. so Mungu akikupangia kufa kwa kupigwa risasi hata hapo hapo bongo unaweza ukamiminiwa hata risasi 5 , uwa naamini sanaa kwenye M/Mungu mkuu
Atakachopanga ndicho kitakachokuwa- hivyo tu
Mangi nipe pepsi toa draft nje
Duhh mtakufwaa ila wazulu ni watu waliochanganyikiwa tangu kuzaliwa kwao
Ondokeni nchi ya watu kama ni biashara mbona hata huku bongo biashara zipo au hamieni nchi zingine kama Zambia, Zimdollar au Botswana mkafanye biashara huko.
Nasubiri muendelezo kama kawaida ya watoa episodi wa JF
Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app