Habari zenu wakuu
Moja kwa moja kwenye mada, husika na kichwa cha habari.
Sio mda mrefu sana nimekuja South Africa kutafuta maisha ni takribani miaka 5 hivi, tangu naingia hapa nilikuta zogo/vurugu Kwa kweli hawa jamaa wanaubaguzi wa kweli kabsa wao wenyewe hawajihesabu kama waafrica ukisikia wanavyotuita waafrica Na ukiangalia vizuri akili zao bado zimelala nafikiri Kwa kuchelewa kupata uhuru kunachangia ,kuhusu sisi kurudi home ni wengi wetu tumeshaanzisha maisha huku zikiwepo Biashara kubwa na familia pia ndicho kinachofanya tuone uvivu kurudi home.
Zogo nililolikuta kipindi naingia hapa kitongojini kuna msichana miaka 17/18 mzawa alipotea na wao wakawasingizia my friend yaani wageni ndio wamemficha Kwa maana wamemchukua kama mchumba au msichana wa kustareheka nae then wamemfungia na wametunyanyasa sanaa kwa kutufungia biashara zetu na kutuchomea moto kwa kisa hicho yaani tulikuwa tunaishi bila amani yapata mwaka mmoja na baadae baada ya kutulia na kufanya uchunguzi serikali yao ikagundulika kuwa huyo msichana ameuliwa na mjomba ake na baadhi ya viungo amevifukia na vingine ameviweka uvunguni kwake Kwa imani zao za kishirikina wenyewe, basi jamaa akaenda kunyea debe.
Yaani jamaa ni wapumbavu sanaa wakiamua tu wanashikana masikio na kuanza kutufukuza na hawajali chochote wakati tuna wake na watoto lukuki na tumezaa na wasouth wenzao uzuri sio wote wanaotaka tuondoke ila ni baadhi wenye nguvu ya kusikilizwa na wengi na ni watemi wa mitaa ila bado Tupo sanaa maisha hayaa.
Hiyo vurugu ya juzi sasa iliyokuwa kama vita tuliyoamua kupigana nao.
Ilianza chuki kwenye masaloon kwa kuwashutumu wanauza madawa ya kulevya, na Kweli wakatoa kauli masaloon yote yafungwe na kwa muda watakao amua wao ndio yafunguliwe na Kweli watu wa masaloon wakatii amri Na wakafunga saloon zao na ikapita kama miezi mitatu saloon hazijafunguliwa baadhi ya raia wakaanza kuwagomea wenzao kwamba tutanyoa wapi? Mbona mmewafungia mda mrefu ugomvi ukawa wenyewe kwa wenyewe watu wa saloon wakawa na maisha magumu sanaa yaani hawana pa kupata shillings mbili tatu za kukidhi haja zao, wao wakitaka kunyoa wanaenda town Na siunajua town gharama nyingi nauli na hata bei ya kunyoa pia- na mpaka mda huo na kupitia mgogoro wa wenyewe kwa wenyewe wahajaamuru saloon zifunguliwe watu njaa kalii.
Wakaanza vurugu za kwenda kusachi vyumbani kwa watu wa saloon wanapita nyumba moja moja aliyekuwepo mgeni na wanasachi na kibaya zaidi wakikukuta na pesa wanakuibia na pasport nazo wanachukua na kibaya tena wanakuja bila ruhusa yoyote ya serikali na serikali inafahamu wanachofanya na hawachukui hatua yoyote ilee uonevu tu uliyokithiri, wakawaibia sanaa watu wamasaloon baadae wakaanza kuwafukuza Kwa kuwafungishia virago na kwenda kuwahaikisha yaani kuwapandisha magari waondoke na kuwapiga, wamewaburuza sanaa mzee hawa sio watu kabsa.
Baadae wageni tukaanzisha group letu WhatsApp la kutiana hamasa kuwa haya yanayoendelea tusinyamaze sanaa inapidi tupaze sauti Na baadae itakavyokuwa tupambane nao kwani wao ni kama sisi tu, group likatamaradi tukatiana moyo sanaa na wapo wagen wenye bunduki tukasema tunapambana nao tu hakuna jins- achana na hii mda wa kama mwaka mmoja ilitokea mji wa PE-port elizabet, wasomali na waethiopia waliwapiga sanaa wazawa baada ya kuonewa Kwa kipindi kirefu wakachoka basi mpaka leo heshima Na adabu na sisi tu kaona tunaweza fanya kitu.
Tuendelee kisa
Baada ya kuona wamefanikiwa kuwafukuza na kuwavunjia wenye masaloon wakaona ngoja tuamie kwenye maduka, Na ijulikane wenye maduka ni watu wenye nguvu sanaa wana pesa na wanajiweza ukitofautisha na saloon wengi wenye masaloon hawana kitu yaani ndio wengi wanauza bangi na madawa lakini wengi wenye maduka ni waethiopia na wasomali na wachache ni watanzania ambao tuna maduka na ulinzi mkubwa tunaupata kwa hawa wenye nguvu waethiopia na wasomali, binafsi nipo dukani duka langu au sio langu tutaodiscus kipindi kijacho.
Wakaanza kutuletea home affair madukani Kwa kigezo asiyekuwa Na kibali aondoke, jalamba likapita wakatusumbua sanaa ila walikuwa wanadunda tu Coz hauwezekani una duka alaf kibali chako kiwe cha kuunga unga na walitupa wakati mgumu sanaa kipindi hicho hali ya biashara ilikuwa ngumu sanaa.
Sometimes wanakuja usiku wanakulazimisha wasach uzuri tulijua ni wezi so pesa tulitafuta jinsi ya kuficha pamoja na pasport ila wakkmaliza hapo lazima waibe vitu vya dukani wana njaa kinoma, Na wanakuwa wengi sanaa ila kusachi wanaingia kama 20 au 25 ila yaani huko nje kuna kuwa na watu kama 200 hivi yaani wakiamua kukuua wanakuua yaani mara moja.
Walitusumbua sanaa watu wamadukani na baadae wakatuambia tufunge maduka, cha ajabu tukifunga maduka hawana pa kunijua chakula mpaka waende town na town ni gharama kuanzia nauli mpaka chakula, wanaanza kugombana wenyewe kwa wenyewe na kuanza kutofautiana, wajinga kabsa hawa jamaa.
Mda ukaenda tukawa tunauza Kwa kujiiba jiiba Na wakigundua wanakuja kuchoma moto duka na ukakaa kizembe na wewe unachomwa moto Kama sio ulemavu unakufa yaani wanakuua na wapo waliouliwa.
Baadae wakatupa tarehe ya wageni wote kuondoka hiki kitongoji Na tusipofata hiyo amri kuanzia hiyo tarehe watakuja kututoa Kwa nguvu- shughuli ilianza hapo wakuu ilikuwa kama move vilee.
Tarehe ikafika wapo waliondoka Na wengi hatukuondoka kwa kuwa tuliofia kuacha mali zetu ikiwepo na familia zetu tukatiana nguvu kwenye group kuwa tunakutana sehemu flani na tunawaface na kupigana nao na atakayeshindwa vita ndio ataondoka kama sio sisi au wao baadhi yao wakasikia kwamba tumeamua kupambana wakaambiana kwenye group lao Kwa hivyo hiyo siku ilikuwa siku ya vita.
Mchana wake kulikuwa kimya sanaa kumbe walipanga waanze vurugu usiku.
To be continued...