Vurugu zisizoisha kitongoji ninachoishi Afrika Kusini

Vurugu zisizoisha kitongoji ninachoishi Afrika Kusini

Nikuhakikishie siku hizi wengi wauza madawa hawataki hata kuyasikia hao madawa yaani wanejiajir kwenye maduka na restaurant watu wanakimbia hizo biashara
Wafanyabiashara wapo ila wabongo wengi wanajihusisha na Narcotics
 
Nitarudi kujibu comments zenu nna jazba sana hapa nikijibu lazima nitapaniki nitawajibu kwa hasira na sitoendelea na hiki kibwanga

PART TWO

usiku kama wa saa saba wazee wa kazi wakaanza kazi yao wakaanza kijisehemu chenye wamalawi wengi full kuwachapa yaani wamewachakaza sanaa usiku ulee na kuwapeleka N2- yaani barabara kubwa kwa maana wapande magari waondoke kwao wengine wamekimbilia kituo cha police unaambiwa police kama hawawaoni raia vilee nomaa ilikuwa, baada ya mda watu tukashituana kwenye group kwamba wazushi wameanza mda huu saa 7 kuganya vurugu Kwa usiku ulee wenye magari ndio waliamka na kupitia baadhi ya watu /raia wageni wenye hasira zao na kuongozana mpaka kituo cha police

Walee wazushi wakawa wanawakimbiza wageni Kwa kuwapiga na magongo usiku huo na walikuwa wanakimbilia kituo cha police basi banah baada ya watu kujaa palee kituo cha police likaanza nomaa, Kwa kuwa police walijifanya kama hawahusiki raia wakigeni waliokuwepo ikabidi wakinukishe na kuungana na walee waliokimbizwa, wamama wakigeni wakaambiwa watulie wanaume wakaanza kazi binafsi usiku huo sijakuwepo mimi nilianza kazi hasubuhi ya kuwabalasa wazushi

Mziki ulikuwa mnene zilipigwa hapo mpaka polisi wakaingilia Kwa kupiga mabomu na mabunduki juu kiufupi wajinga tuliwaweza Kwa usiku ulee wakakimbia kazi ikaanza tena hasubuhi yake

Saa kumi na moja raia tumeshaamshana na kuanza kupanga tunaanzia wapi tulikuwa wengi sanaa, wazimbabwe ni nomaa aisee hawana mzaha, tulikuwepo wazimbabwe, wabongo, wagana, wanaigeria, wamalawi, waethiopia, wasomali na wamozambiki- kilinuka hiyo hasubuhi sisi tuliamka mapema kumbe na wao walishaamka kwa kutufukuza tuondoke

Tuliwaambia kuwa atayeshindwa vitaa yeye ndiye atakayeondoka, wakuu isikieni tu vitaa ni balaa lingine kabsa yaani sio ya kuiomba hata kidogo M/Mungu nijaalie niondokane na balaa hili nikiwa mzima amini

Tunapanga maandalizi mpaka saa moja, saa moja na nusutukatoka na kuwafata walipo, kuna kajisehemu kuna uwanja ndio wanaposimamaga Kwa mikutano yao na kupanga waanzie nyumba ya nani? Tukawakuta hapo sasa bwanah hawakuamini kama tupo tayari Kwa vita Na tulikuwa wengi kinomaa yaani tukiongozwa na wenye bunduki ila walizificha mpaka waone vitaa inakomaa vipi? Tulikuwa na mapanga na magofu stiki na malungu

Haina kuuliza hiyo wao walikuwa takribani kama 100 hivi wengine waliogopa fujo mziki wa jana usiku walijua hawa wapo seriously, sisi tulikuwa wengi sanaa aisee

Tukawavamia na kuanza kuwapa kichapo na fimbo na Malungu tuliongea kuwa tusiwapige mapanga maana bado tuna muendelezo katika hiki kitongoji

Walijitahidi kupambana lakini na wingi wetu tuliwaweza tuliwachakaza sanaaa baadhi yao tuliwavunja miguu na mikono, tuliwapasua pasua yaani kama lisaa Na nusu tunawapiga tu- ndipo yakaja magari ya asikari wa kawaida yaani police tukawagomea na baada ya kupiga mabomu na kuongeza vikosi vingine ndio tukawaacha walikuwa wanalia tu yaani Kwa hicho kichapo

Mda si mda waandishi ww habari wakaja sehemu ya tukio na kuanza kutuhoji

Wapo walioelezea, kuwa serikali haioni kinachoendelea mpaka mnawaachia wanatunyanyasa kama hivi kama hatutakiwi kweli watangaze na watupe utaratibu tuondoke kiharali na mali zetu kwani na sisi tuna kwetu kinachotufanya tugande hapa ni mali zetu tu na familia zetu, kama hamtuhitaji ni mseme tu na mtuandalie mazingira tuondoke kwa amani sio kutesana kama hivi- ilikuwa hivyo

Mchezo haukuishia hapo

Hapo baadhi ya wageni wengine wapo machakani wamejificha maporini huko wapo waliohama mji Kwa kukimbia vurugu na vurugu ikiisha watarudi kuendelea na maisha yao kama kawaida

Siku hiyo ikaisha tukajipongeza sanaa , huwa tuna shushuhsu kwenye group lao la whatsapp kuwa kinachoendelea atujulishe kama kawa akatuambia nini? Kinaendelea kuwa wamepanga kesho yake wakinukishe kweli na wameapa kuwa hiyo ndio vita ya bunduki kuwa lazima wafe watu

Tukapata habari , wasomali na waethiopia na wagana na wanaigeria katatutoa hofu- wakatuambia kuwa tuna bunduki tutakuja nazo wakasema Bora watu wafe ili heshima iwepo, Na baadhi ya wabongo waliokuwa Na bastora zisizo Na vibali wakasema watakuja nazo na itakuwa poa tu

Na tukasisitizana kuwa hatutakufa sisi tu kuwa sisi tutakufa na wao pia watakufa

To be continue
Man to man
 
Kkoo wale jamaa wa calculator wanasumbua sana heri vita[emoji2960]

Kariakoo sehemu nzuri sana ya biashara mkuu yaani sehemu nzuri snaa , napafikiria sanaa tatzo ni mtaji tu maana unatakiwa uwe na mtaji mzuri kidogo
 
Wafanyabiashara wapo ila wabongo wengi wanajihusisha na Narcotics

Nilikataa maisha ya kuuza dawa tangu nipo Tanzania na sijasafiri na kitu ambacho naishi mpaka sasa

Siamini et ili nifanikiwe mwenzangu aharibikiwe, siamini kabsa yaani
 
Habari zenu wakuu

Moja kwa moja kwenye mada, husika na kichwa cha habari.

Sio mda mrefu sana nimekuja South Africa kutafuta maisha ni takribani miaka 5 hivi, tangu naingia hapa nilikuta zogo/vurugu Kwa kweli hawa jamaa wanaubaguzi wa kweli kabsa wao wenyewe hawajihesabu kama waafrica ukisikia wanavyotuita waafrica Na ukiangalia vizuri akili zao bado zimelala nafikiri Kwa kuchelewa kupata uhuru kunachangia ,kuhusu sisi kurudi home ni wengi wetu tumeshaanzisha maisha huku zikiwepo Biashara kubwa na familia pia ndicho kinachofanya tuone uvivu kurudi home.

Zogo nililolikuta kipindi naingia hapa kitongojini kuna msichana miaka 17/18 mzawa alipotea na wao wakawasingizia my friend yaani wageni ndio wamemficha Kwa maana wamemchukua kama mchumba au msichana wa kustareheka nae then wamemfungia na wametunyanyasa sanaa kwa kutufungia biashara zetu na kutuchomea moto kwa kisa hicho yaani tulikuwa tunaishi bila amani yapata mwaka mmoja na baadae baada ya kutulia na kufanya uchunguzi serikali yao ikagundulika kuwa huyo msichana ameuliwa na mjomba ake na baadhi ya viungo amevifukia na vingine ameviweka uvunguni kwake Kwa imani zao za kishirikina wenyewe, basi jamaa akaenda kunyea debe.

Yaani jamaa ni wapumbavu sanaa wakiamua tu wanashikana masikio na kuanza kutufukuza na hawajali chochote wakati tuna wake na watoto lukuki na tumezaa na wasouth wenzao uzuri sio wote wanaotaka tuondoke ila ni baadhi wenye nguvu ya kusikilizwa na wengi na ni watemi wa mitaa ila bado Tupo sanaa maisha hayaa.

Hiyo vurugu ya juzi sasa iliyokuwa kama vita tuliyoamua kupigana nao.

Ilianza chuki kwenye masaloon kwa kuwashutumu wanauza madawa ya kulevya, na Kweli wakatoa kauli masaloon yote yafungwe na kwa muda watakao amua wao ndio yafunguliwe na Kweli watu wa masaloon wakatii amri Na wakafunga saloon zao na ikapita kama miezi mitatu saloon hazijafunguliwa baadhi ya raia wakaanza kuwagomea wenzao kwamba tutanyoa wapi? Mbona mmewafungia mda mrefu ugomvi ukawa wenyewe kwa wenyewe watu wa saloon wakawa na maisha magumu sanaa yaani hawana pa kupata shillings mbili tatu za kukidhi haja zao, wao wakitaka kunyoa wanaenda town Na siunajua town gharama nyingi nauli na hata bei ya kunyoa pia- na mpaka mda huo na kupitia mgogoro wa wenyewe kwa wenyewe wahajaamuru saloon zifunguliwe watu njaa kalii.

Wakaanza vurugu za kwenda kusachi vyumbani kwa watu wa saloon wanapita nyumba moja moja aliyekuwepo mgeni na wanasachi na kibaya zaidi wakikukuta na pesa wanakuibia na pasport nazo wanachukua na kibaya tena wanakuja bila ruhusa yoyote ya serikali na serikali inafahamu wanachofanya na hawachukui hatua yoyote ilee uonevu tu uliyokithiri, wakawaibia sanaa watu wamasaloon baadae wakaanza kuwafukuza Kwa kuwafungishia virago na kwenda kuwahaikisha yaani kuwapandisha magari waondoke na kuwapiga, wamewaburuza sanaa mzee hawa sio watu kabsa.

Baadae wageni tukaanzisha group letu WhatsApp la kutiana hamasa kuwa haya yanayoendelea tusinyamaze sanaa inapidi tupaze sauti Na baadae itakavyokuwa tupambane nao kwani wao ni kama sisi tu, group likatamaradi tukatiana moyo sanaa na wapo wagen wenye bunduki tukasema tunapambana nao tu hakuna jins- achana na hii mda wa kama mwaka mmoja ilitokea mji wa PE-port elizabet, wasomali na waethiopia waliwapiga sanaa wazawa baada ya kuonewa Kwa kipindi kirefu wakachoka basi mpaka leo heshima Na adabu na sisi tu kaona tunaweza fanya kitu.

Tuendelee kisa

Baada ya kuona wamefanikiwa kuwafukuza na kuwavunjia wenye masaloon wakaona ngoja tuamie kwenye maduka, Na ijulikane wenye maduka ni watu wenye nguvu sanaa wana pesa na wanajiweza ukitofautisha na saloon wengi wenye masaloon hawana kitu yaani ndio wengi wanauza bangi na madawa lakini wengi wenye maduka ni waethiopia na wasomali na wachache ni watanzania ambao tuna maduka na ulinzi mkubwa tunaupata kwa hawa wenye nguvu waethiopia na wasomali, binafsi nipo dukani duka langu au sio langu tutaodiscus kipindi kijacho.

Wakaanza kutuletea home affair madukani Kwa kigezo asiyekuwa Na kibali aondoke, jalamba likapita wakatusumbua sanaa ila walikuwa wanadunda tu Coz hauwezekani una duka alaf kibali chako kiwe cha kuunga unga na walitupa wakati mgumu sanaa kipindi hicho hali ya biashara ilikuwa ngumu sanaa.

Sometimes wanakuja usiku wanakulazimisha wasach uzuri tulijua ni wezi so pesa tulitafuta jinsi ya kuficha pamoja na pasport ila wakkmaliza hapo lazima waibe vitu vya dukani wana njaa kinoma, Na wanakuwa wengi sanaa ila kusachi wanaingia kama 20 au 25 ila yaani huko nje kuna kuwa na watu kama 200 hivi yaani wakiamua kukuua wanakuua yaani mara moja.

Walitusumbua sanaa watu wamadukani na baadae wakatuambia tufunge maduka, cha ajabu tukifunga maduka hawana pa kunijua chakula mpaka waende town na town ni gharama kuanzia nauli mpaka chakula, wanaanza kugombana wenyewe kwa wenyewe na kuanza kutofautiana, wajinga kabsa hawa jamaa.

Mda ukaenda tukawa tunauza Kwa kujiiba jiiba Na wakigundua wanakuja kuchoma moto duka na ukakaa kizembe na wewe unachomwa moto Kama sio ulemavu unakufa yaani wanakuua na wapo waliouliwa.

Baadae wakatupa tarehe ya wageni wote kuondoka hiki kitongoji Na tusipofata hiyo amri kuanzia hiyo tarehe watakuja kututoa Kwa nguvu- shughuli ilianza hapo wakuu ilikuwa kama move vilee.

Tarehe ikafika wapo waliondoka Na wengi hatukuondoka kwa kuwa tuliofia kuacha mali zetu ikiwepo na familia zetu tukatiana nguvu kwenye group kuwa tunakutana sehemu flani na tunawaface na kupigana nao na atakayeshindwa vita ndio ataondoka kama sio sisi au wao baadhi yao wakasikia kwamba tumeamua kupambana wakaambiana kwenye group lao Kwa hivyo hiyo siku ilikuwa siku ya vita.

Mchana wake kulikuwa kimya sanaa kumbe walipanga waanze vurugu usiku.

To be continued...
Huko kuna tofauti gani na Tz, hasa kwa shughuli mnazofanya?
 
Huko kuna tofauti gani na Tz, hasa kwa shughuli mnazofanya?

Tofauti ni pesa thamani ya pesa ya tanzania ni tofauti Na ya South Africa Kwa ukubwa mkubwa sana

Usi complain hakikisha unashauri au kuelekeza na kukosoa pia ruksa
 
Unaweza kupambana vipi na binadamu wasiojuwa thamani ya uhai wa binadamu?

Utaratibu wa South Africa ukiishi miaka mitano mfululizo kihalali una haki ya kuomba Uraia, au ukiowa Msouth Africa una haki hiyo.

Watanzania wanaojitambuwa watumie fursa hizo kupata ID ili wapate passport za Kisouth Africa waondoke hapo.

Passport ya South Africa inaheshimika nchi nyingi za mabeberu wanaingia bila viza na wenyewe hawana utamaduni wa kutafuta maisha nje ya nchi yao, Kwahiyo South Africa passport yao bado iko clean kwenye records za mabeberu.

Chukuweni passport muondoke hapo, ndicho walichofanya wajanja waliojitambuwa kitambo tu.

Ukiwa chini ya miaka 30 unachukuwa working holiday viza ya miaka kadhaa UK bila usumbufu wowote kwa Msouth Africa.

Pale Slough Uingereza Makaburu ni kama Nyumbani kwao wamejazana kibao kwa kutumia fursa hiyo, akirudi South Africa na Pound zake ni tajiri.
[emoji7]
 
Kwani kuna Mzaramo mwenye duka kariakoo?

Wamekuja Wakinga juzi tu wameikamata kariakoo.

Sasa Tanzania ingekuwa ni primitive country kama wale mbwa wa kizulu Kariakoo pasingekalika na Wachina wangeuwawa sana.

Shida moja wale primitive nashindwa kuwaelewa mpaka leo wao mgomvi wao ni kwa weusi wenzao, tena wanawaita jina la kibaguzi "Makwelekwele" wanawaogopa wazungu usisikie.
[emoji1787]

Jamaa ni "primitive" sana...
 
Ni vilee bint tu ila ungejua vilee mwanaume anatakiwa force mpaka afanikiwe ungenipa moyo tu

Nna vingi sanaa vya kulipa ikiwepo mahari ambayo wewe hautoisikia wala kuilipa kipindi unaolewa au ulichoolewa
[emoji1787]
 
STORY HAIENDELEI- hii ni kajikituko tu kalichotokea hasubuhi hii

Nimefungua goli saa 6:30 kwa ajili ya huduma kama kawaida, huwa hasubuhi wateja wengi ni wafanya kazi wanaoenda makazini na wanafunzi wanaoenda mashuleni

Huwa sana sana wananunua matunda na biscut kwa ajili ya break fast- kama nusu saa hivi nimefungua duka natoa huduma- kamekuja katoto kateja kinaishi hapa hapa mtaani kwetu

Kameleta baadhi ya vitu kanasema kanauza nikakaambia mimi sina kitu akanambia hautaki bastola ninayo hapa, akaitoa akafanya kama anaikoki na kujaribu kuishoot ili kunionyesha kama ipo poa huku akiwa kanielekezea mimi


Nikamwambia usiniielekezee hiyo mzee, akacheka na akanambia aina risasi akaishusha kilee kidude cha kuwekea risasi na kunihakikishia kama haina kitu

Nikamuuliza umevipata wapi? Hivi vitu; akanambia tumevunja na kuingia hapo N2 kwa mzungu tumeviiba na kwa maelezo yake kuna wenzake bado wapo kawaacha kwenye hiyo nyumba wanaendelea kuchukua vitu

Fasta tu ; nikamwambia mzee hapa fanya uende banah hapakufai kabsa akawa anacheka ka kunambia AIZN muoga sana wewe

Akaweka vitu vyake Sawa akaondoka- mtoto kavu kweli yulee
 
Kesho yake pakatulia sio wao wala sisi kuonekana kiwanja cha vitaa

PART THREE-MWISHO

Mji ulikuwa kimya sanaa hiyo kesho yake ambayo walisema ni kiwanja cha vita kitajaa damu- hakukua na yeyote mabarabarani, kulisikika milio ya magari tu na hakuna yeyte nje kila mmoja alijifungia kwake

Kesho kutwa yake tena kimya na wiki nzimaa ilikuwa kimyaa

My friend tukajadiliana hapa haina haja ya kuambiwa tufungue maduka yaani tujifungulieni tu kwani tumeshawaweza na hawawezi fanya chochote kilee

Tukafungua- wakaanza choko choko siku hiyo hiyo tukasema hatufungi ila tunawaudumia wateja wetu nje? Ya bagla yaani , wateja hawatoingia mpaka ndani dukani tutawahudumia kama maduka ya bongo, huku huwa wanaingia dukani wanachagua vitu then wanakuja tunawapigia mahesabu alaf wanalipa dzain kama ya vimin market vilee,haikuwa hivyo ikawa tunawahudumia kama bongo vilee

Ila kuna wabishi walikuwa wanawaachia waingie wajichagulie na ilikuwa fursa tena kwa vibaka katika wiki hiyo hiyo

Kuna duka wameingia vibaka na kupola pesa na kumpiga shaba mtoto wa kiarabu/kiethiopia na kumuua ila walikuwa wezi tu sio hao wenye mgomo hatimaye wakakamatwa wakaenda jela- sema inasemekana kesi ya kuua sio kesi Kwa South Africa kwamba walikuwa wawili katika upelelezi akaachiwa mmoja Kwa maana yeye siyo aliyempiga bunduki ila mwenzake amenyea ila wanasema anaweza akakaa miaka miwili tu then akatoka ila waethiopia wameapa akitoka asirudi mitaa hii kwani nayeye watampeleka alipompeleka mwenzake yaani watampiga bomba nayeye, yule mmoja tunasikia tu ametoka ila hayupo mitaa hii itakuwa amehamishwa mji

Na uwezi amini hao watoto waliomuua huyo jamaa walishawahi kuja dukani kwetu wakataka waibe tukawashitukia, tukataka tuwachape tumewakolomea tu tukawaacha maana kujenga vichuki vidogo vidogo sio inshu kabsa, maana hata ukiwakazia kuwapa sigala wakilalamika hawana kitu wanaweza wakaja kukupiga bomba yaani chuki tu mwananga sio maisha kabsa south africa hapafai kabsa yaani tupo tu Kwa ajili tumeshaanzisha maisha

KIKANUKA TENA SERIOUSLY HIYO WALIOSEMA WANAKINUKISHA

tuliambiana tufunge biashara tukafunga , wakakusanyanaa mitaani na kuanza kuchoma mapira wana mapanga na malungu na Safari hii walikuwa wengi sanaa

Sisi kama kawaida tukashituana kuwa vita imerudi tena na uzuri mahojiano ya siku ilee halifika sehemu husika so kulikuwa na asikari maalumu wapo doria

Wakawakamata ma- icon wao kama kumi , kumi na mbili hivi, yaani waliwakamata walee waanzilishi wa vurugu wakawatia ndani lakini tulikuwa tayari kwa vita , yaani tulikuwa tayari kwa chochote

Ila binafs nilishukuru kuona pambano lipo off Kwa siku hiyo-nilishukuru

Walee wengine wafata mkumbo kuona wenzao wamekamatwa wakakimbia

Tukaambizana kilichoendelea tukatudisha silaha kwenye ala zake

Nna mpaka video ila sitaweza kiwawekea hapa mtandaoni

Vitaa ilisimama hivyoo- wajamaa hawajatoka mpaka leo kesi kila siku inapelekwa mbele wanaenda kama wachochezi wa vurugu

ila ninachokiona ili balaha likirudi tena itakuwa nomaa sanaa yaani watakufa watu yaani hapa nna mpango wa kujichanga kama Mil 10 , nitokomee canada/ popote pazur ila ndio nakichanga

Baada ya hili balaa- kuna baadhi ya wabongo ambao hawakuvunjiwa maduka yao, wameuza biashara zao na kwenda Tanzania kuanza maisha mengine nanasikia wengine waneshapata visa wapo zao canada huko , yaani hapa ndonga linauma nitoke hapa SA nitafute kiwanja kingine- ila ilee kutoka moyoni siogopi chochote kilee sio kuhusu tunavyopondwa watu wa SA wala hayaa maisha ya bastola kila siku sihofii chochote kilee

Ninachohofia kupoteza biashara yangu tu I wish nipate mteja niiuze nitokomee zangu makanada huko

Najifunza vingi sana na ukifikiria nna 29 yaani na naendelea kujifunza

Kuhusu kuuza biashara wasomali na waethiopia hawaogopi chochote ukitaka kuuza wao wananunua tu wao wapo tayari kwa lolote nipo kwenye mafikirio ya kuuza ila ngoja kwanza niangalie upepo


MWISHO [emoji1478]

Kuna mengi sijayaweka katika maisha ya kila sikuya South Africa
Nimeshatolewa bunduki mara mbili na kutolewa kisu mara moja ki ukweli ni maisha ya roho mkononi, karibu sanaa SA

ASANTUM- tupo sanaa maisha hayaa ila ikimpendeza M/Mungu atujaalie tutusue twende zetu CANADA HUKO-InshAAllah [emoji1431]
Pambano linalofata wakianza kujipanga nishtue mapema nije kufanya mafunzo kwa vitendo ya Kombat kila yangu
 
Back
Top Bottom