Vurugu zisizoisha kitongoji ninachoishi Afrika Kusini

Vurugu zisizoisha kitongoji ninachoishi Afrika Kusini

Ni kweli ubaguzi hauangalii elimu ya mtu, lakini Wazungu hasa Makaburu wanapogundua kuwa wewe mtu mweusi una Elimu kubwa zaidi au ni mtaalamu zaidi kwenye eneo lako ulilosomea na watapata kitu kutoka kwako kupitia elimu yako/utaalamu wako ulionao, basi huwa wanakuwa wapole, zaidi zaidi sana watakuheshimu na kukunyenyekea. Hawawezi wakakunyanyasa, hali hii nimeshuhudia Mimi mwenyewe.

Hata ivyo heshima ambayo napewa na wazungu sijui ningekuwa na hiyo elimu unayosema sijui ingekuaje!!

By the way- mimi sio darasa la saba mkuu

Nzuri mkuu
 
Kwa nini munakomaa kwenye nchi za watu kama hamutakiwi?

Ila hilo ni fundisho kubwa maana na nyinyi watz kila siku ni lawama oooh waarabu hivi, oooh wahindi vile... kumbe ni uvivu wenu wa kufanya kazi. Sasa na nyinyi mumekwenda huko mumeona moto unaowawakia.

Poleni sana lakini rudini nyumbani.
Munakomaa~mnakomaa
Hamutakiwi~Hamtakiwi
Mumekwenda~Mmekwenda
Mumeona~Mmeona
(Toa -u-)
 
Ndugu yangu, nimeandika kwa kumaanisha kabisa tena nikiwa na ufahamu mkubwa wa kutosha kuhusu South Africa. Mara nyingi nimekuwa nikisafiri kuja SA, siyo hivyo tu lakini pia nimewahi kuishi katika miji mbalimbali ndani ya SA.
1. Jo'burg (JHB), nilikaa ktk maeneo mawili:
i) Rosebank area: along Jan Smuts Avenue, jirani kabisa na Ubalozi wa Uingereza kama unaenda Randburg.
ii) Saxonwold, Houghton Estates, jirani na Johannesburg Zoo

2. Bloemfontein (BFN), in Mangaung Municipality.
Hapo nilikaa ktk eneo linaloitwa Dan Pienaar na eneo lingine liitwalo Westdene (Brandwagg)

3. Cape Town (CPT), nilikaa ktk eneo linaloitwa Camps Bay, Hely Hutchinson Avenue, either South Beach au Eastern Beach(sina uhakika sana kuhusu hili kwani sikumbuki vizuri kama hilo eneo hasa ni beach ya upande upi, South or East?).

Wakaazi wa maeneo hayo asilimia kubwa zaidi (takribani asilimia 98+ ni weupe (wazungu), watu weusi tulikuwa tunahesabika. Naamini mpaka hata siku hizi hali hii bado inaendelea kuwa hivyo, kwanza huko hata majirani tulikuwa hatujuani, kila mtu yupo busy na mambo yake.

Muhumu kuzingatia: Tafadhali, Kamwe USIKURUPUKE kutoka ktk nchi yako na kwenda kuishi ugenini kwenye nchi za watu bila ya kujiandaa kisawasawa. Kabla ya kuondoka nchini kwako hakikisha unajianda vizuri ili usiwe mzigo au public charge ktk nchi za watu, panga mipango yako vizuri. All in all, tuzingatie sana sana suala la ELIMU, ELIMU, ELIMU, ELIMU!!
Ulikuwa unalipa kodi kama TSH kwa mwezi? Kwa nyumba ya namna gani?

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
TAARIFA

Jorberg leo kuna vurugu task lenk- sijui ya wapi? Nimepata habari

Wageni wamepigwa na kuumizwa na madereva task kwa kusemekana wanauza madawa na wanasema madawa wanataka wauze wao wenyewe madereva task so wageni waache kuuza ili wawaharibu ndugu zao wao wenyewe sio waharibiwe na wageni

Nimepata habari hiyo mchana wa leo
 
Sasa unahofia nini? Unashindwa hofia mibisu na mi AKA ya huko ila unaogopa kuweka video hapa??

Ah ah ah private za watu mkuu, binafs sipendi picha yangu iwe inatembea mtandaoni sasa vipi? Kuhusu watu wengine private zao mkuu lazima niwafikirie na wao
 
THAMANI YA PESA YA KISOUTH AFRICA- RAND

thamani ya Rand imeshuka sanaa kipindi naingia South Africa R1 ilikuwa = na 170 sasa hivi R1= 100 so zamani ulikuwa ukichange r1000 unapata tsh 170,000 sasa hivi ukichange r1000 unapata tsh 100,000-pesa yao imeshuka sanaa haina thamani kama zamani itoshe kusema tena hapa south Africa sio kiwanja cha kujichanga kidosho ni mahala pakuondoka napaona wazi wazi

AMEME- umeme umekuwa kero unakatika ovyo yaani nafikiri uchumi wao unashuka Kwa sababu ya kukatika Kwa umeme kila baada ya mda

Umeme unaweza ukakatika/ukakatwa saa 2 hasubuhi ukarudishwa saa 4 hasubuhi kwenye siku hiyo hiyo moja tena ukakatwa saa 10 jioni na ukarudishwa saa 12 jioni na mchanganyiko wa kubadilisha ratiba tena ya kukatika na kukatwa kwa umeme so kwa siku lazima umeme ukatwa masaa 4 itokee sanaa umeme ukakatwa masaa 2 tu au ukaachwa siku nzima- makampuni mengi sana yanefungwa kwa habari za chini chini nimesikia kisa Kwa kukatika na kukatwa kwa umeme

Na umeme ukikatika kuna baadhi za line yaani card za simu zinakosa network yaani hauwezi kutumia data so unabidi usubiri umeme urudi- yaani it means kuna baadhi ya network za baadhi ya mitambo hazifanyi kazi

Takribani mwaka na zaidi sasa kuna tatzo la umeme South Africa, hatufanyi kazi Kwa raha madukani mafuriji yanaharibika na nyama pia zinaharibika

Kuna tatzo kubwa sanaa la umeme South Africa na ndio sababu ya kushuka kwa uchumi wao na mpaka sasa hawana suluhisho
 
Niliwahi kukoswa kisu kika mkuta Mmalawi mmoja hapo china plaza corner. 2016
 
Back
Top Bottom