Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
uzi huu mkuu haupaswi kutolewa humu moja kwa moja.unapaswa kudondoshwa humu hata kila baada ya wiki mbili.Umetukumbusha mambo mengi saaana.Binafsi nimejihurumia na wakati mwingine comments zimenichekesha sana.Ni mizoga,Masalo na chupa za juice zilizookotwa mitaroni zikiwa na mikojo.aisee kuhusu vyakula hapa mjini ni tatizo kuu,uweza shangaaa unakula nyama ya kuku lakini husikiii ladha yoyote ya nyama,kwa ndugu zangu wapenda kachumbari na juisi ndo shida zaidi,nyanya zinazo itwa masalo ndo hutumika zaidi kutengenezea hiyo kachumbali omba tu kusikia hayo masalo kuliko uyaone.kwa wapenda juisi zinazotengenezwa mtaani na kuwekwa kwenye chupa za maji zinazo okotwa mitaani nitabu tupu,nyingi za chupa hizi huokotwa mitaroni zikiwa na mikojo ambapo siamini kama zinasafishw kwa maji ya moto,ndo hizohizo huwekewa hizo juisi
blaza nakula hapa umenikata moto aseeKwanza lazima tukubaliane kuwa hakuna mfanyabiashara anayependa hasara iwe ni hotel mgahawa au bar kubwa zikiwemo take aways. Wote hawa hutulisha ndaza na viporo.
Ni mara chache nno kuona chakula kinamwaga. Kikibaki kinahifadhiwa kwenye friji mpaka siku inayofuata. Shida inakuja kwenye umeme wetu ambao hukatika mara kwa mara ambapo husababisha chakula kuharibika.
lakini shida nyingine kubwa ni aina ya mafuta yanayotumika ,hii hasa ni kwenye hizi bar na hotel za kawaida ,kwa ajili ya kutaka faida kubwa hutumia mafuta ya bei poa ambayo yamejaa lehemu ,mbaya zaidi mafuta hayohayo hutumika kupikia chakula zaidi ya kimoja yatakaangia chips hayohayo yatakaangia mayai kuku samaki nk.
Viungo vingi ni vya kuokoteza kwenye masoko na vya bei poa ,kwa wale wapenzi wa kachumbari na salad mnalishwa minyoo mitupu kwa wale wapenzi wa tomato sauce nyingi ni feki za kutengenezwa mtaani.
Nyamachoma ,rost michemsho supu kuku na samaki vingi huwa vibudu na mizoga!!!tunalishwa vitu vya ajabu mno kuku wengi hawajachinjwa wamenyongwa nyama nyingi huwa hao wanyama wamekufa kwa ugonjwa nk samaki wengi huvuliwa kwenye mito na mabwawa ya mitaani full uchafu full sumu.
Nyama nyingine ni za mbwa paka nk.
Epuka michemsho mishkaki na roast za usiku supu za makongoro mkia ulimi nazo ndio hizohizo.
Tunakulaga vyakula ambavyo havina ladha au tunaharisha au kuumwa matumbo tujue tu kuwa siku hiyo tumelishwa ndaza vibudu au mizoga
Tuwe makini tunapoagiza hivi vyakula jamani
Nimekula ile nyama ya punda miezi mitatu mfululizo pale kiwandaniUkiacha mbwa na paka hata punda nyama yake watu wanalishwa bila kujua. Dodoma kuna kiwanda cha kuchinja nyama ya punda halafu minofu inapelekwa China lakini mabaki mengine kama makongoro, kichwa, matumbo na masalia ya nyama kama mbavu yanapikwa mitaani na watu wanakula bila kujua. Hata nyama yenyewe watu wamechanganyiwa bila kujua na kwenda kuipika nyumbani. Zamani watu wanaposafiri walikuwa na tabia ya kuandaa chakula cha safari wenyewe nyumbani ikiwa ni pamoja na kutembea na maji. Siku hizi wanajifanya wameendelea kila kitu ni kununua njiani matokeo yake tutalishwa hata nyama ya binadamu bila kujua
Siamini nikionacho naona kama maigizona wapishi wa mandazi na chapati wako ktk mashindano ya nani atauza zaidi
View attachment 365178
Sio bata tuu mkuu, hata asali ukiichunguza jinsi inavoandaliwa na nyuki ni balaa.Sa tutafanyaje wakati njaa inauma..... ukimchunguza sana bata huumli
Hapo kwenye supu ya mkia umenipata kuna bar moja maeneo ya ubungo kila jiioni nikirudi kutoka kwenye mishe zangu lazima nipitie hapo kupiga hiyo supu ya mkia ila hii habari yako imenishtua sana
Nimekula ile nyama ya punda miezi mitatu mfululizo pale kiwandani
Sent from my SM-N910X using JamiiForums mobile app