Vyakula tunavyolishwa kwenye Baa, Hotelini, Migahawa nk

kuna siku calabash nimekaa karibu na jikoni, mhudumu kaja kuchukua chakula kwa bahati mbaya akadondosha paja ya kuku kwenye sahani hadi chini, ile kiroho safi kabisa kamwambia mwenzie embu niokotee. kashika na mikono toka kwenye sakafu moja kwa moja kwenye sahani.. inaenda kwenye meza! nilisikitika sana..
 
uzi huu mkuu haupaswi kutolewa humu moja kwa moja.unapaswa kudondoshwa humu hata kila baada ya wiki mbili.Umetukumbusha mambo mengi saaana.Binafsi nimejihurumia na wakati mwingine comments zimenichekesha sana.Ni mizoga,Masalo na chupa za juice zilizookotwa mitaroni zikiwa na mikojo.
Aiseee hii ni hatari saaaana
 
na wapishi wa mandazi na chapati wako ktk mashindano ya nani atauza zaidi
 

Attachments

  • Uchawi wa mapishi.jpg
    36.6 KB · Views: 107
blaza nakula hapa umenikata moto asee
 
Kuna baa moja Kaloleni Arusha wanauza firigisi za kusaga na mayai
Hakuna firigisi pale ni nyama za miguu ya kuku na utumbo wake
 
Ukiacha mbwa na paka hata punda nyama yake watu wanalishwa bila kujua. Dodoma kuna kiwanda cha kuchinja nyama ya punda halafu minofu inapelekwa China lakini mabaki mengine kama makongoro, kichwa, matumbo na masalia ya nyama kama mbavu yanapikwa mitaani na watu wanakula bila kujua. Hata nyama yenyewe watu wamechanganyiwa bila kujua na kwenda kuipika nyumbani. Zamani watu wanaposafiri walikuwa na tabia ya kuandaa chakula cha safari wenyewe nyumbani ikiwa ni pamoja na kutembea na maji. Siku hizi wanajifanya wameendelea kila kitu ni kununua njiani matokeo yake tutalishwa hata nyama ya binadamu bila kujua
 
point yako ni nn watu wasiende baa na hotel au? tukale wap sasa kwa mfano hata kama unakula home je mchana ukiwa ktk mishe zako usile kisa utalishwa ndaza! cha msingi ni kula sehem makin tu si vinginevyo
 
Nimekula ile nyama ya punda miezi mitatu mfululizo pale kiwandani

Sent from my SM-N910X using JamiiForums mobile app
 
point yako ni nn watu wasiende baa na hotel au? tukale wap sasa kwa mfano hata kama unakula home je mchana ukiwa ktk mishe zako usile kisa utalishwa ndaza! cha msingi ni kula sehem makin tu si vinginevyo
bona naona umeanza kwa kuniuliza lakini ukaishia kujijibu
 
Kwa kweli ni shida, mama nitilie wengi wali ukabaki kesha anapika mwingine kidogo. Ukiisha iva anaupakua nusu ya sufuria halafu anauweka ule wa jana katikatoti kisha ule wa leo alioupkua anauweka juu ili ule wa jana pale kati upate joto. Ndio maana wakati wa kupakua anachanganya changanya wa chini na wa juu. Unapewa mixa yako maisha yanaenda.
 
Hii ni kazi ya maPublic health inspector.

sema mabwana afya wetu Waendekeza njaa tu.

hili jipu nalo rais alitumbue. wafutiwe leseni kabisa, watu wakapike nyumbani.

hivi kati ya uchafu barabarani na hii migahawa/mama ntilie/wauza matunda ni wapi hasa watu wanapata kipindupindu na typhoid!
 
Hapo kwenye supu ya mkia umenipata kuna bar moja maeneo ya ubungo kila jiioni nikirudi kutoka kwenye mishe zangu lazima nipitie hapo kupiga hiyo supu ya mkia ila hii habari yako imenishtua sana

yenu bar hiyo bila shaka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…