Vyama vya Siasa 8 nchini China

Niambie ilikuaje wanachama wa chama Cha demokrsia walifungwa? Kwa Nini lazima Politburo ipitishe jina l mgombea?
Vurugu za 2019 ulifuatilia ?
 
Ok
 
Rushwa na ufisadi ni adui wa haki

Asante nawe pia kwa mchango wako hapa
 
What is dictatorship ?
Dictatorship can be defined as the form of government in which one person or a small group possesses absolute power without effective constitutional limitations.

The countries that suit this example are China, Russia, North Korea, Cuba, Iran, Syria, Saudi Arabia, Bahrain etc.
 
Ok
 
Uimara wa kusabotage nchi zingine, hivi unajua walichokifanya wachina kwenye jengo la AU kuhusu kuiba taarifa?

Unaujua mpango wa China kwa Africa?

Au ww unaona wanakuchekea tu.
Afrika itapata ukombozi wa kweli pale tu tutakapo amua kufuata sera zetu kuendana na historia,jamii,jiografia na utamaduni wetu kitendo Cha kuona kwamba Afrika itajikomboa kiuchumi,kisiasa,kijamii kwa kuegemea Ulaya,Asia au America ni kujidanganya wazi wazi sio Ulaya, America na Asia watakuja kulijenga bara la Afrika na nchi zake bali wapo kwa ajili ya maslahi ya nchi zao.

Ujinga wa viongozi wa bara la Afrika ndio umefanya bara hili kuonekana la ajabu na ujinga mwingi hivyo kuchezewa na mataifa makubwa ya Ulaya, America na Asia
 
Reactions: TPP
Nimekuuliza unaujua mpango wa China kwa Afrika?

Kuna kitu kinaitwa "Dept trap diplomacy" unakijua?

Xi anatumia msemo aliouacha Mao na anauzingartia kwelikweli unaosema "there is two ways to conquer a man, one is by sword another is by Dept"

Xi ni mkomunost na ni Mao mtupu, fatilia vizuri na ujue madhara yake ni yapi kwa Africa,

Leo hii wachina wamejazana Zambia wapo kila Kona hawaheshimu sheria za nchi, wanawabagua na kuwadhalilisha wa Zambia kwenye nchi yao, Leo hii wazambia wanakwambia ni Bora kuwa mchina Zambia kuliko kuwa Mzambia Zambia. Mchezo huu walitaka kuupeleka Kenya na Uganda na kwa kiasi fulani wamefanikiwa. Pia na Tanzania walitaka kuuingiza kupitia mkopo wa kujenga Bandari ya Bagamoyo.., ya Bagamoyo yalikuwa yaje kuwa kama ya Sri Lanka.

Magufuli aliposoma yale masharti ya mkataba wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo alisema "hata mlevi hawezi kukubaliana na masharti yale ya kinyonyaji" fatilia.

Hawapendi uwazi na wanapenda rushwa na mambo ya kupindapinda,

Hawa jamaa we waone hivyohivyo jaribu kukaa nao karibu ndio utawajua vizuri. They don't respect local countries laws kabisa.

Nikikuwekalea list ya nchi ambazo ameziingiza kwenye Dept trap utashika kichwa kwa mshangao na masikitiko
 
Hakuna taifa lenye kulitakia bara la Afrika kheri zaidi ni unyonyaji tu sio kutoka Ulaya, America na Asia wanacho tofautiana ni njia tu za unyonyaji.

Kuhusu Zambia na ambayo umesema naweza sema kwamba hapa ndipo ujinga wa mwafrika ulipo kumthamini mgeni na kumdharau mwenyeji shida hapo sio wachina bali waafrika wenyewe.

Afrika itajikomboa yenyewe bila kuegemea sera za ulaya, America na Asia
 
Reactions: TPP
Hivyo siyo vyama, ni jumuia tu ambayo haishiriki katika mambo ya SIasa. Uliwahi kusikia China kuna uchaguzi wowote? Mzee Deng alijaribu kujenga jamii ya kidemokrasia mpaka akaweka ukomo wa uongozi, na kujaribu kuwa na uchaguzi lakini alipokufa tu, mambo ya uchaguzi yakatupiliwa mbali, na alipoingia jamaa Xi yeye akafuta hata ukomo wa uongozi akawa frais wa maisha. Nchi yenye rais wa maisha unaitegemea kuwa na uchaguzi wowote kweli?
 
Mchina akija kuharibu mazingira kwetu hapo kosa sio mchina kosa lipo kwetu sisi wasimamizi wa Sheria na sera zetu juu ya mazingira wachina wanapaswa kufuata Sheria zetu sio kuacha wafanye wanavyo taka katika nchi yetu.

Suala la wachina kuharibu mazingira kwao hilo linawahusu wao na sera zao na Sheria zao maana hatufanani nao katika nyanja zote mkuu
 
Reactions: TPP
Unazijua sheria za kimataifa za kulinda mazingira? Au "international environmental laws" wewe..?

Sheria za mazingira za kimataifa zinalenga vitu vikuu vinne.

(1) protecting the global atmosphere, including preventing climate change and ozone depletion;

(2) conserving wildlife and biological diversity;

(3) managing the oceans and marine environment; and

(4) regulating global movement of chemicals, wastes and other hazardous ...

Unaposema swala la uharibifu wa mazingira kwakuwa limefanyika China basi tuachane nalo hapo nakuvua vyeo na utafanya nikuone hauna upeo wa kutosha kuleta hoja hapa.

Unajua ni madhara kiasi gani China inachangia kwenye uharibifu wa anga hewa au hewa ukaa,.?
Unajua ni madhara gani China inachangia kwenye kuharibu wildlife kwa kuua kuharibu na kula viumbe pori?
Unajua ni kwa kiasi gani China inavuruga uzalianaji wa samaki kwa kufanya overfishing?
Taka sumu zinazoachiliwa kwenye mito na bahari unajua zina madhara kiasi gani kwa taifa la kesho?

Twende kisomi..!!

Leo hii oil spills ikitokea China usitegemee kwamba madhara yatabakia China pekee Bali yatasambaa na kuleta madhara kulekote ambapo hayo mafuta yatasambaa kulingana na mzunguko wa ocean currents na kwa taka sumu ndio hivyohivyo, Tambua hili!
 
Ni swali gani sijajibu naomba unioneshe.

Je, na maswali yangu unaya jibu ?
Why China Kuna Tabia za kibaguzi na selikari wala CCP hawakemei?

Kwanini mwafrica aanapokuwa China haruhusiwi kukanyaga hospitali za wachina na pia baadhi ya restaurant na sehemu zingine zenye huduma muhimu mnamdiscriminate mtu mweusi?

Utatuaminisha VP kwamba nyinyi wachina hamna Nia binafsi ambayo ni ovu kwetu kwa kutuenezea propaganda ilhali kwenu mnatubagua, kutudharau na kutunyanyapaaa.?
 
Suala la uchafuzi wa mazingira ni global problem hasa kwa mataifa yaliyo endelea kiviwanda kote dunia Asia,Ulaya na marekani sioni mantiki ya wewe ya Kila Jambo kutupa lawama kwa China as if China ndio chanzo Cha uchafuzi wa mazingira pekee duniani.

Kuhusu international laws za kulinda mazingira zipo wazi mbona na licha ya uwepo wa Sheria hizo pia Kila nchi ina Sheria zake na sera zake za kulinda mazingira hivyo Kila mmoja kwa nafasi yake anatimiza wajibu.

NB: Mimi nipo hapa kujifunza sio kubishana ,naomba takwimu za data juu ya madai uliyo weka kuhusu uvuvi nk asante
 
Reactions: TPP
Wacha nikujibu for last. moja(1) ubaguzi upo duniani kote pili(2) serikali haihusiki na aina yoyote ile ya ubaguzi tatu(3) kubaguliwa na mchina moja, wawili au watu haimaanishi hiyo ndiyo mentality ya raia na viongozi wote wa China
 
Hivyo siyo vyama, ni jumuia tu ambayo haishiriki katika mambo ya SIasa.
Hivyo ni vyama vya siasa vya China vina viti vyake katika bunge la watu wa China
 
Mzee Deng alijaribu kujenga jamii ya kidemokrasia mpaka akaweka ukomo wa uongozi, na kujaribu kuwa na uchaguzi lakini alipokufa tu, mambo ya uchaguzi yakatupiliwa mbali,
Demokrasia ya kichina ipo toka utawala wa Mao alicho fanya Deng ni marekebisho machache yenye manufaa katika demokrasia ndani ya chama, serikali na nchi na mpaka sasa ipo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…