Vyama vya siasa mkikutana na Rais Samia mtamwambia nini?

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
18,154
Reaction score
17,491
Sio vema mkazungumze hoja zenu binafsi kama vile nilipigwa, nilivunjwa mkono, biashara yangu ilifungwa, na mambo kama hayo kwa Rais ambae ni mpya na ambae yuko serious kutaka kujaribu kunza ukurasa wake mpya.

Kunzia sasa kila chama kirudi kwa wanachama wake wakusanye maoni yao juu ni mambo gani ya kumwambia Rais. Baada ya hapo vyama vya siasa vikutane ili kupata mambo watakayomwambia Rais kwa pamoja kama agenda zao.

Jitahidini msiwe na mambo mengi ya kuomba kwa Mh. Rais. Machache yanaeleweka zaidi kuliko mengi.

Baada ya hapo wateue msemaji wao wa kuyasema hayo walioamua kumwambia mh. Rais wakati wa kikao. Wachague msemaji anaejua namna ya kuwakilisha, kuomba na kushawishi (lobby), maana, how you say it matters much than what you say, hasa hapa kwetu Afrika.
Lugha ya kufoka, command, na kejeli inaweza kupata tafsiri totauti kwa Mh. Rais inayoweza kutoa matokeo hasi.

Hata hivyo nadhani mambo yenu muhimu ni umaliziaji wa katiba mpya, tume huru ya uchaguzi na kuruhusiwa kufanya siasa za kuvijenga vyama vyenu kabla ya 2025.
 
Kuna haya mambo matano muhimu wasiyasahau;
1.) Rasimu ya Katiba Mpya kujadiliwa upya kwenye Bunge la Katiba
2.) Tume Huru ya uchaguzi
3.) Kuruhusiwa mikutano ya kisiasa
4) Polisi kutoingilia shughuli za kisiasa (mfano yule OCD wa Hai, yule Kamanda Shana, nk)
5.) Uhuru wa vyombo vya habari na pia vyombo hivyo vya habari kufanya shughuli zao kwa usawa na pasipo kupendelea upande wowote ule (TBC, Habari Leo na Daily News inawahusu hii)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…