Vyama vya siasa vianze kujitofautisha kwa mirengo

Vyama vya siasa vianze kujitofautisha kwa mirengo

econonist

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
20,189
Reaction score
29,663
Vyama vyetu vya siasa nchini vianze kujitofautisha kwenye mirengo ya kushoto au kulia. Hii itasaidia wananchi na wanachama kuvijua vyama hivyo vinasimamia Nini. Pia itasaidia vyama kujua vijikite kwenye maeneo gani na sera zipi.

Mrengo wa kulia unategemea zaidi kwenye ubepari na kuangalia maendeleo ya mtu mmoja mmoja. Ila mrengo wa kushoto unaegemea kwenye ujamaa na maendeleo ya pamoja. Kwa mfano nikipitia katiba ya CHADEMA naweza kukiri CHADEMA inafuata mrengo wa kulia Yani ubepari na nikiangalia katiba ya CCM naweza kukiri ya kwamba inafuata mrengo wa kushoto. Swali ni je, wanachama wa CCM wanajua kuwa chama chao ni Cha mrengo wa kushoto ? na je wanachama wa CHADEMA wanajua ya kwamba chama chao ni Cha mrengo wa kulia?

Nadhani ni muhimu vyama vikajiweka wazi kuhusu mirengo yao na sio kujificha kwenye uwingi wa uanachama, ushabiki na uchawa. Ni vizuri kuweka mirengo ya vyama wazi ili wanachama wawe huru kujiunga na chama kinachosimamia maslahi yao.
 
Hakuna mwanachama wa CCM asiyefahamu Falsafa na Itikadi ya chama kuwa ni Ujamaa na Kujitegemea.

Tangu enzi za mwalimu, ulikuwa husajili kuwa mwanachama wa CCM ispokuwa umehitimu darasa la Falsafa na Itikadi.

Hadi sasa CCM inaendelea kutoa elimu hiyo kwa wanachama wapya.

Hoja yako ni halisi kwa vyama vya upinzani. Vijengo hoja zao kutoka katika misingi ya Falsafa na Itikadi zao. Viache kukosoa sera za serikali ya CCM bila mpangilio wa kifalsafa. Watu wanaojielewa, wanaviona bado havina uwezo wa kuongoza nchi, kuanzia katika uwanda wa hoja yako.
 
Back
Top Bottom