mwanamwana
JF-Expert Member
- Aug 1, 2011
- 1,309
- 4,798
Salaam wakuu,
Miaka ya hivi karibuni kumeibuka tabia hii mbaya ya kutumia wananchi wanaokumbwa na matatizo mbalimbali hasa wanaokumbana na mkono wa sheria.
Imefika wakati hadi wanamgombania kama mpira wa kona raia aliye kwenye matatizo husika ili kila mmoja basi aonekane akijali tatizo lake.
Baadhi ya wanasiasa wanaweza kutoa msaada wa kifedha au rasilimali kwa familia za raia waliohukumiwa ili kujenga picha ya ukarimu na kujali, hivyo kujinufaisha kisiasa.
Wanasiasa wanaweza kutumia kesi za uhalifu za watu maarufu au zinazovutia hisia za umma kama njia ya kujipatia umaarufu na kuonekana kama watetezi wa haki.
Mfano hivi karibuni tumeona kijana akiingia kwenye matatizo ikidaiwa kuwa alitekwa na kutaka kuuawa lakini Mungu alikuwa na makusudi naye akaepuka kifo, baada ya taarifa zake kusambaa wakajitokeza wanasiasa, wanaharakati, vyama vya siasa wote wakiwa na lengo la kumjali. Inafika hadi muda wengine wanashawishi mchango wa chama, au mtu fulani familia iukatae au kuurudisha. Haya yote hayafanyiki gizani, bali kwenye mitandao ya kijamii ili kujiuza.
Pia tumeona Vijana wawili Yusuph Chaula na Mhandisi Matarra waliohukumiwa kwa makosa ya kimtandao wakigombewa na wanasiasa na kuwachangia ili kuwa huru.
Lengo linaweza kuwa zuri lakini linapoingizwa mambo ya siasa linaharibu mantiki nzima ya kumsaidia mhitaji badala yake kuwanufaisha wanasiasa kukamata nyoyo za watu.
Huko mbeleni tutakuwa na Taifa la ajabu linaloshabikia uvunjaji wa sheria za nchi. Imefikia hadi muda kuna wanasiasa wanajiteka makusudi ili kuingia vinywani mwa watu na kujinufaisha kisiasa.
Matumizi ya raia waliohukumiwa kwa manufaa ya kisiasa ni kinyume na maadili ya nchi. Ni muhimu kwa jamii kuwa na ufahamu na uangalifu juu ya vitendo hivi na kuhakikisha kuwa haki inatendeka kwa njia inayofaa.
Pia soma