Fumadilu Kalimanzila
JF-Expert Member
- Dec 10, 2016
- 1,770
- 5,423
Vyama vya upinzani karibia vyote na hasa CHADEMA havina mikakati na watu makini wanaoweza kuendesha siasa ya kuing'oa CCM madarakani.
Ni vyama ambavyo vimejaa mamluki na wachumia tumbo wanaotafuta umaarufu na kuendesha siasa za mihemuko.
Vyama havina organization na vinaendeshwa siyo kitaasisi na vimetawaliwa na mediocres ambao hawana vision yoyote zaidi ya kulalamika na kutafuta huruma ya jamii ndani na nje ya Nchi.
Vyama hivi havina ubunifu,hata miradi midogo midogo hawana ambayo ingewasaidia kuendesha vyama na kuwafikia wananchi wengi mno hasa wa ngazi ya chini.
Vyama ambavyo havijui vina wanachama wangapi, wako wapi, wanafikiria nini na wanafanya nini haviwezi kupambana na CCM hata kidogo.
Hivi vyama viache kuwapotezea watu muda kwani nje ya mikutano ya hadhara na maandamano havina lolote kabisa.
Vyama hivi sasa vimebaki kuendeshwa kishabiki na kwa hisia kwa kuzingatia jamii iliyoko kwenye mitandao ya kijamii kama Twitter, Instagram, Facebook n.k.
Vimebaki kutegemea mawazo ya akina kigogo2014 kuendesha siasa zao.
Vimeshindwa kutambua kuwa jamii ya wanamitandao hapa Tanzania hawazidi laki 6 kati ya Wapiga kura takribani milioni 20.
Na hawa wanamitandao wengi wao ni wasomi uchwara ambao hawajui umuhimu wa siasa na ndio walio- create hii mentality ya kususia chaguzi na hata ku-discourage watu kujiandikisha kushiriki michakato ya kisiasa!