Vyama vya upinzani Tanzania vinajihujumu na kuhujumiana badala ya kushindana CCM

Dr Adam Francis

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2011
Posts
790
Reaction score
1,316
Ni dhana inayoaminika kuwa, kama ukitaka suluhu ya kweli na ya kudumu kwa matatizo yako basi ujiepushe na kutafuta majubu rahisi kwa maswali magumu.

Kuelekea Oktoba 29, kundi linalohamasisha maandamano linauza hoja kuwa mtesi wa wapinzani tangu 1992 tuingie kwenye vyama vingi ni CCM. Wakati huo huo hawatuambii kwanini wao wameruhusu CCM ifanikiwe kuvihujumu vyama 18 kwa zaidi ya miaka 33?

Hebu tutafakari kidogo, ni nani kaifungulia CHADEMA kesi ya mgawanyo wa mali? Ni nani kaishtaki CHADEMA kwa msajili? Ni nani aliyekuwa wa kwanza kumuwekea mgombea urais wa ACT pingamizi? Nani alikivuruga chama cha CUF? Nani walioivuruga NCCR? Kisha zitazame kauli na mienendo ya wapinzani mara tu wanapohamia CCM.

Kwa tafakari hizi ni jambo lililo wazi kuwa; kama ni kweli CCM inahujumu vyama vya upinzani, basi watekelezaji wa hujuma hizo ni vyama vya upinzani vyenyewe pamoja na wafuasi wao kwa maslahi binafsi, chuki na wivu.

Tuwe wa kweli kwa nafsi zetu, kwa chama kama CHAUMA, unadhani kati ya CHADEMA kuchukua nchi na CCM kuendelea kubakia madarakani, wangechagua jambo gani? Ni imani yangu jawabu ulilolipata, ndio hali halisi kwa ACT na vyama vingine vya upinzani vilivyobaki.

Leo hii tunashawishiwa kuandamana sababu kubwa ni vyama vya upinzani kushindwa kutekeleza majukumu yao kwa umoja na mshikamano. Kama hivi vyama vinavyodai vinahujumiwa kwa umoja wao vingekuwa na msimamo thabiti kuwa havitashiriki uchaguzi mpaka mabadiliko yafanyike; Je, CCM wangefanya uchaguzi wa chama kimoja? Lakini wao wanasalitiana, wanahujumiana, wanalamba asali harafu wanataka sisi ndio tuwe chambo yao kudai madai yao, serious?

CCM shabaha yake ni kuendelea kushika dola. Ni wazi kuwa haiwezi kukataa kuwatumia wapinzani ndumila kuwili kufikia malengo yake. Ni jukumu la vyama vya upinzani kuvijenga vyama vyao kuwa taasisi imara na kuwajenga wanachama wao kuwa makada waaminifu kwa itikadi zao badala ya kufanya siasa za udalali huku wakiwabebesha wananchi zigo la kudai reforms kwa faida yao.
 
Tatizo la nchi yetu ni njaa na umasikini. MCC wameweza kutumia fursa na kujitwalia resources muhimu kama fedha, properties na magari kwa njia halali na zisizo halali kupitia umiliki wa dola.

Ukiwa na fedha unaweza nunua uhuru wa mtu yeyote ambaye ni masikini. Ukishalielewa hilo utajua kwa nini ni rahisi kufanya dividing and rulling provided hakuna mtu ambaye hapendi fedha.

Ukiweka hela CHADEMA unawavuna wenye njaa wote na watasaliti chama. Same way CHAUMMA, ACT, CUF and the rest.
 
Umezunguka tu umeshindwa kusema CCM ina mapandikizi vyama feki vya upinzani.

Mfano project CHAUMMA choka mbaya eti mwaka huu mwezi mmoja tu watu wanahamia na kufanya press na kupata nafasi za uongozi wa juu , mara wakapata chopa , magari , mkutano mkuu katika kumbi kubwa tu na ziara za ghafla nchi nzima.

Hayo yote ni kodi za wananchi zinazotumika kuhadaa umma pia kuna upinzani na eti kutakuwepo uchaguzi kumbe anashindana mtu mmoja na kivuli chake.
 
Ni dhana inayoaminika kuwa, kama ukitaka suluhu ya kweli na ya kudumu kwa matatizo yako basi ujiepushe na kutafuta majubu rahisi kwa maswali magumu.

Kuelekea Oktoba 29, kundi linalohamasisha maandamano linauza hoja kuwa mtesi wa wapinzani tangu 1992 tuingie kwenye vyama vingi ni CCM. Wakati huo huo hawatuambii kwanini wao wameruhusu CCM ifanikiwe kuvihujumu vyama 18 kwa zaidi ya miaka 33?

Hebu tutafakari kidogo, ni nani kaifungulia CHADEMA kesi ya mgawanyo wa mali? Ni nani kaishtaki CHADEMA kwa msajili? Ni nani aliyekuwa wa kwanza kumuwekea mgombea urais wa ACT pingamizi? Nani alikivuruga chama cha CUF? Nani walioivuruga NCCR? Kisha zitazame kauli na mienendo ya wapinzani mara tu wanapohamia CCM.

Kwa tafakari hizi ni jambo lililo wazi kuwa; kama ni kweli CCM inahujumu vyama vya upinzani, basi watekelezaji wa hujuma hizo ni vyama vya upinzani vyenyewe pamoja na wafuasi wao kwa maslahi binafsi, chuki na wivu.

Tuwe wa kweli kwa nafsi zetu, kwa chama kama CHAUMA, unadhani kati ya CHADEMA kuchukua nchi na CCM kuendelea kubakia madarakani, wangechagua jambo gani? Ni imani yangu ulilolipata, ndio hali halisi kwa ACT na vyama vingine vilivyobaki.

Leo hii tunashawishiwa kuandamana sababu kubwa ni vyama vya upinzani kushindwa kutekeleza majukumu yao kwa umoja na mshikamano. Kama hivi vyama vinavyodai vinahujumiwa kwa umoja wao vingekuwa na msimamo thabiti kuwa havitashiriki uchaguzi mpaka mabadiliko yafanyike, CCM wangefanya uchaguzi wa chama kimoja? Lakini wao wanasalitiana, wanahujumiana, wanalamba asali harafu wanataka sisi ndio tuwe chambo kudai madai yao, serious?

CCM shabaha yake ni kuendelea kushika dola. Ni wazi kuwa haiwezi kukataa kuwatumia wapinzani ndumila kuwili kufikia malengo yake. Ni jukumu la vyama vya upinzani kuvijenga vyama vyao kuwa taasisi imara na kuwajenga wanachama wao kuwa makada waaminifu kwa itikadi zao badala ya kufanya siasa za udalali huku wakiwabebesha wananchi zigo la kudai reforms kwa kauli moja kwa faida yao.
Vyama vya upinzani vipi? List them here
 
Nadharia kuwa FAM ni pandikizi yaweza kuwa propagadna yenye mafanikio makubwa ktk siasa za hivi karibuni
 
Why wafuasi wake wote wahamie CHAUMMA!! why akiue chama alichokijenga mwenyewe? imagine wenje ndio angekua makamu mwenyekiti ingekuaje leo? Si angemsaliti Lissu hadi anyongwe
Propaganda ya FAM kuwa pandikizi ndio iliyotumika kumtoa ktk kiti pamoja na mengine, hivyo haikuanza baada ya kukosa uenyekiti. Baada ya hilo kutokea FAM na TAL isingeliwezekana wafanye kazi pamoja tena, na silioni hilo likitokea katika hali ya kawaida. Namuona FAM kwenda CHAUMMA, binafsi niliona muda sahihi wa kwenda huko ni baada ya uchaguzi, tetesis za kuwa ingelikuwa ni kabla ya uchaguzi ni hazikupaswa kupuuzwa ila niliona ingelikuwa na doa kwake. CHAUMMA wantoa wapi pesa? Nadhani FAM ana uwezo na mtaji rasimali fedha na watu za kufanya yale CHAUMMA waliyo fanya. Mimi sijaona dalili ya maana ya kuwa FAM ni pandikizi, bali naona hali za siasa za uhasama na chuki kati yao.
 
Nadharia kuwa FAM ni pandikizi yaweza kuwa propagadna yenye mafanikio makubwa ktk siasa za hivi karibuni
Ok, huyu mtu tangu ametoka kwenye nafasi ya mwenyekiti January 21 kahudhuria matukio mangapi ya chama?

Mbowe ni mjumbe wa mkutano mkuu, mwenyekiti mstaafu, mshauri wa chama .

Ila ajabu alipoulizwa msimamo wa no reforms no election anauzungumziaje yeye kama mwanachama akadai yeye sio msemaji ! WTH.

Mbowe anahudhuria dira ya Samia Dodoma anapiga na picha juu high table halafu hajahudhuria court proceeding hata moja ya Lissu hapo Kisutu ???
 
Ni dhana inayoaminika kuwa, kama ukitaka suluhu ya kweli na ya kudumu kwa matatizo yako basi ujiepushe na kutafuta majubu rahisi kwa maswali magumu.

Kuelekea Oktoba 29, kundi linalohamasisha maandamano linauza hoja kuwa mtesi wa wapinzani tangu 1992 tuingie kwenye vyama vingi ni CCM. Wakati huo huo hawatuambii kwanini wao wameruhusu CCM ifanikiwe kuvihujumu vyama 18 kwa zaidi ya miaka 33?

Hebu tutafakari kidogo, ni nani kaifungulia CHADEMA kesi ya mgawanyo wa mali? Ni nani kaishtaki CHADEMA kwa msajili? Ni nani aliyekuwa wa kwanza kumuwekea mgombea urais wa ACT pingamizi? Nani alikivuruga chama cha CUF? Nani walioivuruga NCCR? Kisha zitazame kauli na mienendo ya wapinzani mara tu wanapohamia CCM.

Kwa tafakari hizi ni jambo lililo wazi kuwa; kama ni kweli CCM inahujumu vyama vya upinzani, basi watekelezaji wa hujuma hizo ni vyama vya upinzani vyenyewe pamoja na wafuasi wao kwa maslahi binafsi, chuki na wivu.

Tuwe wa kweli kwa nafsi zetu, kwa chama kama CHAUMA, unadhani kati ya CHADEMA kuchukua nchi na CCM kuendelea kubakia madarakani, wangechagua jambo gani? Ni imani yangu ulilolipata, ndio hali halisi kwa ACT na vyama vingine vilivyobaki.

Leo hii tunashawishiwa kuandamana sababu kubwa ni vyama vya upinzani kushindwa kutekeleza majukumu yao kwa umoja na mshikamano. Kama hivi vyama vinavyodai vinahujumiwa kwa umoja wao vingekuwa na msimamo thabiti kuwa havitashiriki uchaguzi mpaka mabadiliko yafanyike, CCM wangefanya uchaguzi wa chama kimoja? Lakini wao wanasalitiana, wanahujumiana, wanalamba asali harafu wanataka sisi ndio tuwe chambo kudai madai yao, serious?

CCM shabaha yake ni kuendelea kushika dola. Ni wazi kuwa haiwezi kukataa kuwatumia wapinzani ndumila kuwili kufikia malengo yake. Ni jukumu la vyama vya upinzani kuvijenga vyama vyao kuwa taasisi imara na kuwajenga wanachama wao kuwa makada waaminifu kwa itikadi zao badala ya kufanya siasa za udalali huku wakiwabebesha wananchi zigo la kudai reforms kwa kauli moja kwa faida yao.
Vyama vingi ni mamluki
 
Ok, huyu mtu tangu ametoka kwenye nafasi ya mwenyekiti January 21 kahudhuria matukio mangapi ya chama?

Mbowe ni mjumbe wa mkutano mkuu, mwenyekiti mstaafu, mshauri wa chama .

Ila ajabu alipoulizwa msimamo wa no reforms no election anauzungumziaje yeye kama mwanachama akadai yeye sio msemaji ! WTH.

Mbowe anahudhuria dira ya Samia Dodoma anapiga na picha juu high table halafu hajahudhuria court proceeding hata moja ya Lissu hapo Kisutu ???
Kwa kumbukumbu zangupande zote mbili zilitaka FAM afanye hilo, yaani FAM alisema akishindwa uchaguzi ataenda pumzika na kufanya biashara zake, na kina TAL walisema FAM amefika kilele cha siasa zake aachie damu mpya abaki kushauri pale itakapo hitajika. Ongeza ba hili, kwa siasa zile za uchaguzi wa CDM zilivyo kwenda ingelikuwa ni wewe ungeweza fanya hilo unalo sema?

Kuhusu jibu lake kunako no reform no election, naona ni jibu la kiungwana kwasababu nia wazi FAM hakuafiki maamuzi hayo, sasa njia sahihi ni yeye kukaa kimya kuwaacha wenzake walio kubali hilo watekeleze jambo lao kuliko kuwapinga au kusema jambo asilo amini.

Kuhudhuria dira sioni shida, labda useme shida iko wapi? ni jambo la kitaifa. Mbona TAL kaongoza vikao vya vya vyama siasa kama mwenyekiti, walikutana na JK msibani wakapeana salamu kwa vicheko na kukumbatiana. Kutofika mahakamani kwa kesi ya TAL, sina majibu yeye ndio anaweza eleza zaidi, je ni indicator ya uhasama baina yao?
 
Kwahiyo kitendo cha kuambiwa aachie damu mpya ziingie na yeye kusema anaenda mapumzikoni ndio inampa nafasi kutosimama na mwenyekiti wako katika madhila?

Nikuulize tu swali la msingi wewe ukiwa likizo mfano ya kikazi mwanao au mtu wa karibu akipata tatizo hutokatisha likizo?

Una uhakika FAM hakuafiki NRNE??

Una habari FAM ndio mwanzilishi wa NRNE 2024?

Nitakupa hapa ushahidi wa video.

View: https://www.instagram.com/reel/DIEf1F4pTiF/

Umeelewa "context" yangu ya swali?

Yaani kukutana msibani ni sawa na kukacha kuhudhuria court proceedings Dar Es Salaam halafu ukasafiri kwenda Dodoma kuhudhuria hafla huku ukimuacha mwenyekiti wako?

Maana ya "stronger together " baada ya uchaguzi kuisha ilikua na maana gani?
 
Hii timu:

IMG_20251026_103208.jpg

Imeuza wengi na bado masalia yaliyopo yanaendea na biashara hiyo.

Ukweli mchungu, kulihitajika purge ya maana!

Wapumzike kwa amani akina Kibao.
 
Kuhusu clip ya FAM au Kigaila kuhusu no reform no election, najua zipo na niliandika nikijua zipo. Lakini ni wazi upande wa TAL na FAM wametofautina ktk tafsir na utekelezaji wa no reform no election wamesha jieleza sana wenyewe.

Kuhusu kukatisha likizo kwasababu ya matatizo ya chama, hujanipata hoja yangu, upande wa TAL ulishajipanga kuhama chama kama wangeshindwa, walikiri wakati wa uchaguzi kuwa wasingekaa chama kimoja tena kwa hali ilivyokuwa. FAM alichofanya kwa maoni yangu ni kuwageuzia mchezo tu, kuwa na yeye akajipanga akishindwa ahame chama na watu wake, kinacho subiriwa ni mazingira na wakati sahihi wa hilo kufanyika hasa kutokana na aina ya siasa za kina TAL. Hata ule wito wa upatanishi nadhani alisema kama mtego pengine kwa kuwajua walio shika chama
 
Kwahiyo kitendo cha kuambiwa aachie damu mpya ziingie na yeye kusema anaenda mapumzikoni ndio inampa nafasi kutosimama na mwenyekiti wako katika madhila?

Nikuulize tu swali la msingi wewe ukiwa likizo mfano ya kikazi mwanao au mtu wa karibu akipata tatizo hutokatisha likizo?

Una uhakika FAM hakuafiki NRNE??

Una habari FAM ndio mwanzilishi wa NRNE 2024?

Nitakupa hapa ushahidi wa video.

View: https://www.instagram.com/reel/DIEf1F4pTiF/

Umeelewa "context" yangu ya swali?

Yaani kukutana msibani ni sawa na kukacha kuhudhuria court proceedings Dar Es Salaam halafu ukasafiri kwenda Dodoma kuhudhuria hafla huku ukimuacha mwenyekiti wako?

Maana ya "stronger together " baada ya uchaguzi kuisha ilikua na maana gani?

Hilo la msiba nilitajia pia ungeweza react namna hio, lakini nilicho lenga hasa ni kukutana kwa kicheko, kuna mambo hayana uadui licha ya toafuti zetu za kisiasa au nyingine zozote zile
 
Hii timu:

View attachment 3493826

Imeuza wengi na bado masalia yaliyopo yanaendea na biashara hiyo.

Ukweli mchungu, kulihitajika purge ya maana!

Wapumzike kwa amani akina Kibao.
Siasa ni ngumu, FAM kuwa pandikizi bado kwangu ni premature scenario. Kama si shambulizi la majaribio ya kumtoa uhai TAL, basi sioni mwanasiasa alie pata madhara mengi kuliko FAM.

Kinacho mponza ni aina ya siasa zake zinaruhusu kubebeshwa tuhuma, lakini hata jirani zetu hapo walimtuhumu Baba kabla ya umauti wake, sina hakika kama bado wanamsimamo uleule baada ya kifo chake? Ni wazi hapana ! Je baba alikosea kufanya engagement na Ruto? kwangu hapana!
 
FAM kuwa pandikizi ndio iliyotumika kumtoa ktk kiti pamoja na mengine,
Mbona kaitwa pandikizi miaks yote tokea anamtimua zitto!!

Hata mimi binafsi nimemtetea sana Mbowe humu miaka yote Ilatuwe wakweli tu Mbowe overstayed na watu wakamchoka so hata asingeitwa pandikizi bado angeangushwa na Lissu!!

People wanted change and that person wasn't Mbowe.
 
Hii timu:

View attachment 3493826

Imeuza wengi na bado masalia yaliyopo yanaendea na biashara hiyo.
Hii timu kabaki Sugu, Boniface, na Martin Masese, ambao kwa maoni yangu walisoma upepo wakabaki ila njia ilikuwa ni moja Chaumma.

Sugu na Boniface walijipanga sana kugombea ubunge lazima walikuwa disappointed na maamuzi ya chama.

Kwasasa ili kuwa relevant ni kufanya appearance za hapa na pale na kuandika mtandaoni ila mda utasema.
 
Tatizo la nchi yetu ni njaa na umasikini. MCC wameweza kutumia fursa na kujitwalia resources muhimu kama fedha, properties na magari kwa njia halali na zisizo halali kupitia umiliki wa dola.

Ukiwa na fedha unaweza nunua uhuru wa mtu yeyote ambaye ni masikini. Ukishalielewa hilo utajua kwa nini ni rahisi kufanya dividing and rulling provided hakuna mtu ambaye hapendi fedha.

Ukiweka hela CHADEMA unawavuna wenye njaa wote na watasaliti chama. Same way CHAUMMA, ACT, CUF and the rest.
Nakubaliana na hoja yako. Lakini bado ninaswali; Je, nijukumu la nani kuvijenga vyama vya upinzani kuwa taasisi imara zenye makada wasionunulika?
 
Back
Top Bottom