Vyama vya upinzani Tanzania vinajihujumu na kuhujumiana badala ya kushindana CCM

Vyama vya upinzani Tanzania vinajihujumu na kuhujumiana badala ya kushindana CCM

Kuhusu clip ya FAM au Kigaila kuhusu no reform no election, najua zipo na niliandika nikijua zipo. Lakini ni wazi upande wa TAL na FAM wametofautina ktk tafsir na utekelezaji wa no reform no election wamesha jieleza sana wenyewe.
Sawa hapo hukuwa na ujanja.
Kuhusu kukatisha likizo kwasababu ya matatizo ya chama, hujanipata hoja yangu, upande wa TAL ulishajipanga kuhama chama kama wangeshindwa, walikiri wakati wa uchaguzi kuwa wasingekaa chama kimoja tena kwa hali ilivyokuwa.
Walijijipanga kwenda chama gani?

Unaweza kuweka uthibitisho hapa?
FAM alichofanya kwa maoni yangu ni kuwageuzia mchezo tu, kuwa na yeye akajipanga akishindwa ahame chama na watu wake, kinacho subiriwa ni mazingira na wakati sahihi wa hilo kufanyika hasa kutokana na aina ya siasa za kina TAL. Hata ule wito wa upatanishi nadhani alisema kama mtego pengine kwa kuwajua walio shika chama
Mkuu, mbona unazunguka na hujibu maswali yangu ya msingi?

Unajua kusoma kwa ufahamu?
 
Siasa ni ngumu, FAM kuwa pandikizi bado kwangu ni premature scenario. Kama si shambulizi la majaribio ya kumtoa uhai TAL, basi sioni mwanasiasa alie pata madhara mengi kuliko FAM.

Kinacho mponza ni aina ya siasa zake zinaruhusu kubebeshwa tuhuma, lakini hata jirani zetu hapo walimtuhumu Baba kabla ya umauti wake, sina hakika kama bado wanamsimamo uleule baada ya kifo chake? Ni wazi hapana ! Je baba alikosea kufanya engagement na Ruto? kwangu hapana!

Kumfananisha huyo mwamba na baba ni way too much. Raila hakuwa mlamba asali na kwa ndogo ndogo zilizopo, alikuwa Moi kamhasi gerezani.

Siyo siri kuwa mwamba katugharimu sana ukombozi wa nchi hii.

Huyo na vibaraka wake walipanga kumfukuza TAL chamani:

PreGE2025 - Mbowe: Lissu kuhutubia Taifa ni kukosa nidhamu na kufanya kazi isiyo yake

Unaiona post hiyo wakimwita TAL takataka?

imhotep, binti kiziwi au nasema uongo?

Kwamba wewe, hii timu tuseme tayari umeisahau?

IMG_20251026_140140.jpg
 
Ni dhana inayoaminika kuwa, kama ukitaka suluhu ya kweli na ya kudumu kwa matatizo yako basi ujiepushe na kutafuta majubu rahisi kwa maswali magumu.

Kuelekea Oktoba 29, kundi linalohamasisha maandamano linauza hoja kuwa mtesi wa wapinzani tangu 1992 tuingie kwenye vyama vingi ni CCM. Wakati huo huo hawatuambii kwanini wao wameruhusu CCM ifanikiwe kuvihujumu vyama 18 kwa zaidi ya miaka 33?

Hebu tutafakari kidogo, ni nani kaifungulia CHADEMA kesi ya mgawanyo wa mali? Ni nani kaishtaki CHADEMA kwa msajili? Ni nani aliyekuwa wa kwanza kumuwekea mgombea urais wa ACT pingamizi? Nani alikivuruga chama cha CUF? Nani walioivuruga NCCR? Kisha zitazame kauli na mienendo ya wapinzani mara tu wanapohamia CCM.

Kwa tafakari hizi ni jambo lililo wazi kuwa; kama ni kweli CCM inahujumu vyama vya upinzani, basi watekelezaji wa hujuma hizo ni vyama vya upinzani vyenyewe pamoja na wafuasi wao kwa maslahi binafsi, chuki na wivu.

Tuwe wa kweli kwa nafsi zetu, kwa chama kama CHAUMA, unadhani kati ya CHADEMA kuchukua nchi na CCM kuendelea kubakia madarakani, wangechagua jambo gani? Ni imani yangu jawabu ulilolipata, ndio hali halisi kwa ACT na vyama vingine vya upinzani vilivyobaki.

Leo hii tunashawishiwa kuandamana sababu kubwa ni vyama vya upinzani kushindwa kutekeleza majukumu yao kwa umoja na mshikamano. Kama hivi vyama vinavyodai vinahujumiwa kwa umoja wao vingekuwa na msimamo thabiti kuwa havitashiriki uchaguzi mpaka mabadiliko yafanyike; Je, CCM wangefanya uchaguzi wa chama kimoja? Lakini wao wanasalitiana, wanahujumiana, wanalamba asali harafu wanataka sisi ndio tuwe chambo yao kudai madai yao, serious?

CCM shabaha yake ni kuendelea kushika dola. Ni wazi kuwa haiwezi kukataa kuwatumia wapinzani ndumila kuwili kufikia malengo yake. Ni jukumu la vyama vya upinzani kuvijenga vyama vyao kuwa taasisi imara na kuwajenga wanachama wao kuwa makada waaminifu kwa itikadi zao badala ya kufanya siasa za udalali huku wakiwabebesha wananchi zigo la kudai reforms kwa faida yao.
Mwamba hoja yako ni nzuri sana na inahitajika akili kubwa ikujibu badala ya kuendekeza ushabiki wa vyama
 
Hakuna upinzani bali kuna upinzani kivuli...upinzani kuungana haitoweza tokea hata kidogo kutokana na migongano ya kimaslahi..kiufupi wanasiasa wote ni wachumia tumbo..KATAA SIASA,KWASASA NI UTAPELI WA KIFIKRA.
 
It is so sad, wapinzani wanahubiri mabadiliko kwa maneno yao lakini matendo yao yanayakana. Upinzani wa Tanzania ni udalali na undumila kuwili, wanajivunjia heshima sana hawa jamaa.
 
Umezunguka tu umeshindwa kusema CCM ina mapandikizi vyama feki vya upinzani.

Mfano project CHAUMMA choka mbaya eti mwaka huu mwezi mmoja tu watu wanahamia na kufanya press na kupata nafasi za uongozi wa juu , mara wakapata chopa , magari , mkutano mkuu katika kumbi kubwa tu na ziara za ghafla nchi nzima.

Hayo yote ni kodi za wananchi zinazotumika kuhadaa umma pia kuna upinzani na eti kutakuwepo uchaguzi kumbe anashindana mtu mmoja na kivuli chake.
Je, ni wajibu wa CCM kuvijenga vyama vya upinzani imara vyenye makada waaminifu kwa itikadi zao?
Nani anayepaswa kuwatambua na kuwashughulikia mamluki ndani ya vyama vya upinzani?
Upinzani wanapaswa kujua CCM sio mjomba wao, na kamwe CCM haitatoka madarakani kama tendo la huruma kwa wapinzani.
Hakuna kisingizio chochote kutoka kwa upinzani kitakachokubalika kama justification ya kushindwa kwao. They are fully responsible for their demise.
 
Je, ni wajibu wa CCM kuvijenga vyama vya upinzani imara vyenye makada waaminifu kwa itikadi zao?
CCM yenyewe imeshaanguka ndio inatakiwa ijijienge.

CCM bila polisi na vyombo vingine vya dola na mafisadi ni sawa na TLP.
Nani anayepaswa kuwatambua na kuwashughulikia mamluki ndani ya vyama vya upinzani?
Mamluki wanachukua pesa za mafisadi kutoka CCM ambao wanaamini wakififisha wapinzani wa kweli ndio wataendelea kuwepo.
Upinzani wanapaswa kujua CCM sio mjomba wao, na kamwe CCM haitatoka madarakani kama tendo la huruma kwa wapinzani.
Hakuna kisingizio chochote kutoka kwa upinzani kitakachokubalika kama justification ya kushindwa kwao. They are fully responsible for their demise.
Hii kauli umesoma vizuri mara mbili kabla ya kupost??

Unaweza kujua kiini cha kesi ya mgawanyo wa mali za CHADEMA Tanganyika na Zanzibar kiini chake ni kipi??
 
Sawa hapo hukuwa na ujanja.

Walijijipanga kwenda chama gani?

Unaweza kuweka uthibitisho hapa?

Mkuu, mbona unazunguka na hujibu maswali yangu ya msingi?

Unajua kusoma kwa ufahamu?
Tafuta interview za clouds tv (kina Masoud wakiwahaoji kina Lyemba/kampeni manager wa TAL), waliulizwa kama wanaona wanaweza baki ktk chama kimoja wakasema hapana si rahisi. Pili hata TAL mwenyewe baada y kushinda alisema kama si kushinda basi angeshughulikiwa kama wengine ambao waliwahu gombea uenyekiti, mwisho FAM alikuwa akisema baada ya uchaguzi chama lazima kichukie hatua za kinidhamu kwa yalitokea ktk uchaguzi.

Kuhusu chama, kina TAL hawajawahi sema chama waziwazi au angalau sijawahi sikia, lakini upande wa FAM waliwahi vumisha kina TAL kuhamia CHAUMMA/ACT sina kumbukumbu wakati wa uchaguzi wa CDM
 
CCM yenyewe imeshaanguka ndio inatakiwa ijijienge.p

CCM bila polisi na vyombo vingine vya dolw na mafisadi ni sawa na TLP??.

Mamluki wanachukua pesa za mafisadi kutoka CCM ambao wanaamini wakififisha wapinzani wa kweli ndio wataendelea kuwepo.

Hii kauli umesoma vizuri mara mbili kabla ya kupost??

Unaweza kujua kiini cha kesi ya mgawanyo wa mali za CHADEMA Tanganyika na Zanzibar kiini chake ni kipi??
Hatua ya kwanza ya kujinasua kutoka kwenye matatizo ni kutambua kuwa upo kwenye matatizo, kutathmini ukubwa wa matatizo yako ndipo utaweza kuanzisha mchakato wa kujinasua kwa mafanikio.
Unapokuwa mwanamageuzi halafu unaamini CCM ni kama TLP ni wazi bado hujajua ukubwa wa changamoto uliyonayo.
Kwavyovyote vile utavyozielezea nafuu za kuwa na dola zinavyoisaidia CCM, bado CCM litabaki kuwa dude kubwa, linalohitaji upinzani ujipange kwelikweli kukabiliana nalo.
 
Tafuta interview za clouds tv (kina Masoud wakiwahaoji kina Lyemba/kampeni manager wa TAL), waliulizwa kama wanaona wanaweza baki ktk chama kimoja wakasema hapana si rahisi. Pili hata TAL mwenyewe baada y kushinda alisema kama si kushinda basi angeshughulikiwa kama wengine ambao waliwahu gombea uenyekiti, mwisho FAM alikuwa akisema baada ya uchaguzi chama lazima kichukie hatua za kinidhamu kwa yalitokea ktk uchaguzi.
Unasema nitafute wakati mimi nilichokileta hapa nimeleta hadi video za ushahidi kuwa FAM ndio aliasisi NRNE baada ya kushindwa timu yake wakaanza michakato ya chini chini kuhama chama wakiulizwa NRNE ni nini wanajikanyaga na interview hizo wamefanyiwa Kigaila na Joh Mrema.

Mimi nakuwekea hapa video sitaki hababri za nenda katafute maana wewe unatete uongo kama mwanzo ulisema FAM hakuasisi NRNE

Huyu ni Kigaila

View: https://youtube.com/shorts/MD9OSzuQ9TE?si=Adytcnft8HQnTAdG

View: https://youtu.be/ZEDXk6rb64g?si=iKC418npSA3bDvBG

Huyu ni Mrema

View: https://youtube.com/shorts/6XjKQjqXRTU?si=E5G1OOTzIE8TDNQ3

Kuhusu chama, kina TAL hawajawahi sema chama waziwazi au angalau sijawahi sikia, lakini upande wa FAM waliwahi vumisha kina TAL kuhamia CHAUMMA/ACT sina kumbukumbu wakati wa uchaguzi wa CDM
Waliosema hakuna kuhama chama ni team ya Mbowe, na hao ndio focus yao kubwa ilikuwa waliamini wangeshinda maana hadi dola iliwasidia kuwajaza mapesa haramu aliyosema Lissu ndio maana walijua watashinda na kuwatimua akina Lissu waliokuwa wanakataa siasa za udalali.

Mfano ni huyu kibaka Yericko Nyerere

Aliyesema hakuna kuhama chama ukishindwa maana walijua watashinda hata kwa njia haramu

View: https://youtu.be/SMRnMEu2eSY?si=T-DlUrPOt0Nnumro
 
Nakubaliana na hoja yako. Lakini bado ninaswali; Je, nijukumu la nani kuvijenga vyama vya upinzani kuwa taasisi imara zenye makada wasionunulika?
Jukumu la kuvijenga vyama ni la wanachama ila pia serikali lazma ijenge mazingira wezeshi kwa kuvipa haki zao kama ruzuku ili viweze kustawi. Let each opposition party strive to the apex without nullifying its movements.

Tatizo mfumo wa serikali ni wa kuzalisha machawa or dividing and rulling. Imetengenezwa kuwa walio karibu na tawala wanakuwa na extra privilleges au wanaosaidia tawala kufanikisha mipango yao which is not a sole purpose ya chama cha upinzani. Imefikia stage wapinzani wana collude na chama tawala ili kufanikisha ufisadi flani in exchange of mkwanja.

Chama pinzani kinatumika kupumbaza raia kupitia kwa wale key politicians wa chama kufanya maigizo ambayo yanaratibiwa na chama tawala. At the end of the day the public trust is gone na chama kinakuwa hakina tofauti na chama kilichopo kwenye dola.
 
Back
Top Bottom