Mbuyu ulianza kama mchicha. Chadema ni kama wanaunda Jeshi lao kimyakimya kwa kutumia maafisa waliokuwa jeshini. Wanawatumia hawa kwa kuwarubuni na fedha, na wanawapa maelekezo watafute maafisa wenzao ili liwe kundi kubwa, naipongeza serikali kwa kuwabaini mapema.
Ila napendekeza, uchunguzi mkali uanzishwe kujua kina hasa Cha nia ya Chadema, labda wanataka kuunda Jeshi la uasi, kitu ambacho ni hatari sana.
Sheria ya vyama vya siasa iangalie namna ya kufuta vyama vya aina hii vinavyohatarisha amani ya nchi. Vyombo vya dola visilale, vifuatilie maafisa wa aina hii, na wachukuliwe hatua kali sana.
Kama nia hivyo ipo, Chadema ivunjwe kwa mujibu wa Sheria, na maafisa wake wote washtakiwe kwa kesi ya uhaini