chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 20,711
- 31,331
Ukweli usemwe, watanzania wanapenda umbea na habari nyepesi, kuwa cut off watu wanaokata kiu hiyo ni kujifanya hatuijui jamii yetu, na pia habari hizo nyepesi (umbeya) zimesaidia ku-de-fuse jamii na pia kunyonya negative issues katika jamii kama godoro linavyonyonya maji. Pia sidhani kama jamii inahitaji watu wenye hard news tu kutokana na usomi wao na ithibati zao.
Kwa ambao hawajui, mainstream media kwa sasa ni kama inatembea juu ya uzi mwembamba kwa kuwa kifo chake ni social media. Kimsingi wako kwenye struggle ya ku survive. Wanaisoma jamii inataka ni ni, wanapita humohumo.
Pia hao wa ithibati wakijaa sana sijui kama serikali itakubaliana na vipindi vyao ambavyo vinaweza kuwa kiithibati vyenye critical observation ya mambo ambayo serikali ilitaka pengine yawe pending. Kama taifa, tumejipangaje kudhibiti mawimbi mapya ya jamii iliyoondolewa kwenye umbeya/soft news yasiangushe chombo?
Nadhani sheria haizuii chombo cha habari kuwa na analyst wa mambo mbalimbali wanaokuwa kwenye kipindi. Nashauri wawepo, lakini wawe chini ya mkuu wa kipindi ambaye ndiye atakuwa ana ithibati ya uandishi wa habari. Sheria iweke wazi jambo lipi lazima lisimamiwe na mwenye ithibati, na lipi linaweza kuwa huria, mfano mhariri mkuu, msaidiI, mkuu wa kipindi/Maud Hui, hao wanabeba professional accountability. Na wana majukumu ya udhibiti. Lazima wawe na ithibati. Hawa wapiga maneno wadhibitiwe na mabosi wao wenye ithibati na wapate vi-training hata vya wiki mbili kuwapa ABC, zifanywe na bodi ya ithibati.
Mwandishi mwenye ithibati ndiye atakuwa anasimamia mjadala. Kwa msingi huo, Bodi ya Ithibati isi-assume kila ambaye anaonekana studio ni mwandishi au anajifanya mwandishi. Vyombo via habari vipewe muongozo wa namna ya kywatambulisha hao analyst kwa bodi ya ithibati.
Mfano, mwenye ithibati ni Sam Sasali au Oscar, yeye ndio awe mkuu wa kipindi, Masudi na genge lake wanaokuwa analyst au contributors... Vile vile Oscar, anakuwa mkuu wa kipindi, Zembwela anakuja kama analyst au contributor.
Hao ambao hawana ithibati, wamekuwa breathing point ya jamii, wanafanya mjadala ya saiti, na ndiko saiti palivyo. Hata usalama wa nchi pia unaimarika pale watu wanapokuwa bize na mambo yao, kivyao, kwa kuwa kila ambaye hakuwa na ithibati alisepa na kijiji chake wakakaa mahala kujadiliana mada zao za kitaa zisizo na ithibati, na serikali ikapata muda wa kusaka fedha kujenga barabara, maji na mambo mengine