Vyombo vya Habari vya Kimataifa vinapata faida gani kuzusha uongo kuihusu Tanzania na Rais Magufuli ?!. Angalia uongo/uzushi wa The Guardian la UK!

Vyombo vya Habari vya Kimataifa vinapata faida gani kuzusha uongo kuihusu Tanzania na Rais Magufuli ?!. Angalia uongo/uzushi wa The Guardian la UK!

We jamaa Ungetunza heshima yako maana kama umezeeka then bado akili zinabaki zakitoto , Sasa umeandika nini?
 
Sasa kama hiyo taarifa ni ya uongo na iliyojaa uzushi, ni kwa nini usiipuuze? Kwa nini mkuu Pascal Mayalla taarifa za aina hii huwa zinataka kukutoa roho? Au kwa sababu nyinyi ndiyo watawala wetu sasa hivyo hamtaki kitumbua chenu kiingie mchanga?

Umeshasahau ulianza hivi hivi kuja na mada kulihusu Gazeti la The Economist la huko juko Uingereza, na mwisho wa siku Swahiba wako Eric Kabendera akakamatwa na kushtakiwa kwa makosa chungu nzima! Awamu hii unamlenga Mwandishi gani mwingine ili atiwe matatani maana kuna kuna wakati baadhi ya wadau humu jukwaani hawakuamini.

Kaa tu utambue kuna Watanzania wengi tu nikiwemo mimi, si wafuasi wa sera nyingi za Rais Magufuli, hasa zile zihusuzo ustawi wa maisha bora kwa Watanzania walio wengi!

Hivyo tunafarijika walau kuona anapata upinzani kutoka nje ya mipaka yetu! Maana huu wa ndani ameshatumia silaha za aina zote kuusambaratisha tangu alipoingia madarakani! Na amefanikiwa kwa asilimia nyingi tu.
 
Hilo gazeti lifungiwe mara moja na kupigwa faini
Wanabodi,

Wanabodi, kila nipatapo fursa huwa ninawaletea makala ndefu za Kwa Maslahi ya Taifa, hivyo leo nimepata fursa tena naendelea na zile makala zangu za kuhamasisha uzalendo kwa jina la "Kwa Maslahi ya Taifa" ambazo zinaendeshwa kwa mfumo wa maswali, leo nazungumzia media za kimataifa zinafaidika nini kwa kuzusha uongo kuihusu Tanzania?, na hawa sources wao ambao ni Watanzania wenzetu, wanafaidika na nini kwa kuwa feed info za uongo, uzushi au kubuni?, what do they stand to gain?. Kuzusha uongo dhidi ya taifa lako na viongozi wake kwenye media za mabeberu ni uzalendo?!.

Ni muda mrefu baadhi ya vyombo vya habari vya kimataifa zikiwemo TV, Majarida na Online contents zao kutunga maurongo kuihusu Tanzania kumkashifu au kukashifu hatua mbalimbali zinazochukuliwa na rais Magufuli, katika maendeleo ya Taifa letu Tanzania, wao watabeza, watakashifu na sometimes hata kumtukana rais wetu, swali la kujiuliza ni vyombo hivi, vinapata faida gani kwa kututungia uongo au kutuzushia na kumzushia rais wetu Magufuli tuhuma za uongo?. What do they get or what do they wish to achieve?.

Katika janga hili la Corona, rais wetu Magufuli anasifiwa duniani kote kwa hatua alizochukua kupambana na Corona, ikiwemo kugomea lockdown, sasa hebu soma makala hii ya gazeti la The Guardian la Uingereza, jinsi ilivyo shehenezwa mauongo na mauzushi kuihusu Tanzania na rais wetu Magufuli!.
Tanzanian president accused of covering up Covid-19 outbreak

Wakati serikali yetu imetoa idadi ya vifo ni 16, na walioambukizwa ni watu 489, hawa jamaa kupitia source wao, wanadai eti Tanzania inaficha idadi ya vifo na maambukizi ya Corona, watu waliokufa kwa ugonjwa wa Corona kwa Dar es Salaam tuu pekee ni zaidi ya watu 400!, huku watu zaidi ya 20,000 wameambukizwa nchi nzima!.

Uongo kama huu una malengo gani?, wanapata faida gani kwa kuzusha uongo mkubwa kama huu?.

Kwa faida ya wale wavivu kufuata links, nakuwekea makala yote, nikiainisha nini ni kweli, nini ni uongo na nini ni uzushi,
Coronavirus outbreak
Tanzanian president accused of covering up Covid-19 outbreak
John Magufuli has repeatedly played down the threat from the pandemic
Jason Burke Africa correspondent
Wed 27 May 2020 17.43 BSTLast modified on Wed 27 May 2020 19.45 BST
President John Magufuli

My Take
Hawa jamaa wanapata nini kwa kutuzushia uongo?. What do they stand to gain?. Na nyinyi Watanzania wenzetu mmafaidika na nini kwa kuwa vibaraka wa mabeberu na kutunga uongo kuhusu nchi yenu?!.
Uzalendo wenu uko wapi?.

Nawatakia Alhamisi Njema

Paskali.
 
K
Kweli Paskali jamaa ni waongo sana yaani sisi kwetu corona imeisha kabisa takwimu zipo vile vile hawazioni? Huko mpakani mwa kenya na uganda madereva wanapatikana na corona wengi ni "WA NCHI NYINGINE".
Kuna raia wa Kenya walipima positive wakiwa Uganda. Waliporudi Mombasa wakapima ikawa negative.
Mtu anaeugua Covid -19 anaweza endesha gari km 200? Mambo mengine tuwe tunajiuliza.
 
Hueleweki. Hao wanasema wanachoweza kusema nyinyi wabongo mnasema anachota kusikia Magu. Huna uwezo wa kuwakosoa maana mpo Dunia mbili tofauti kwa Uhuru wa binadamu. Wewe ni mpiga mtumwa mwema wa jiwe wakati yeye ni mtu huru. Acha kujifananisha kenge we
Ujumbe umemfikia
 
Mkuu Pascal, wewe ni mtu uliyeheshimika sana humu Jf. Na mimi nimesoma makala zako nyingi. Ulisimama katikati katika issues kubwa. Now you are becoming too subjective kwa kigezo cha uzalendo. Wengi humu ni wazalendo na wengine ni washabiki tu.
Kinachotakiwa ni kuzikataa hizo tuhuma kwa facts and figures na sio kwa mihemko.
Mfano, tunasema tulipima watu 1000 na watu 20 wakakutwa positive. Tukapima tena watu 5000 watu 10 wakapatikana positive nk. Therefore hali ya korona inapungua.
Bora mamlaka ilitoa facts kupitia wagonjwa waliopo hospitali.
Figures ni nzuri na zinatafsiri nyingi na muhimu.
Mfano tukipima watu 1000 tukakuta 200 ni positive na wagonjwa ni 10, na 9 wakapona 1 akafa. Lakini nchi x ikapima watu 1000 na 100 wakakutwa positive na 50 wagonjwa na vifo 15 tutapata taarfa gani muhimu hapa? Tukifanya comparison tuta come out na nini?
Je, tukilinganisha Afrika na ulaya tutajifunza nini kuhusu hii pandemic?
Ndio maana watu wanatakiwa kupimwa tujue idadi ya maambukizi, wanaougua, wanaopona na wanaokufa na tuchukue hatua sahihi. Tunaweza kujua mwishoni kuwa huu ni kama mafua tu makali na watu wakaishi kwa amani nao kwa tahadhari za kawaida
So, Pascal facts and figures please na prpaganda hazisadii kamweeee!

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Halafu mkuu siku mojamoja fupisha haya maandishi yako maana unaandika bonge la mgaazeti, Neno moja unatudiarudia unatuchosha wasomaji wako
 
Uzuri dunia inayashuhudia
awamu yenu ikipita itabidi tuwajengee masanamu.
Worst term ever, mnajaribu kupambana n hao mnaowakopa daily.
Ni kama kutukana wakunga.
Nchi zinazoendekea kiuhalisia kuna mikomo kwenye baadhi ya vitu, hasa kwenye afya za watu, anachokifanya meko ni kucheza na afya ya wananchi wake
 
Huyu jamaa tufike mahali tususue post zake tusiwe tunachangia Kwa sababu anasumbuliwa na vitu viwili
1.uccm(tabia za kishetani)
2.ukabila(ubinafsi Wa kujiona mjuaji)

Swelana.
Mkuu Swelana, moja ya faida kubwa ya jf ni kuelimishana na kusaidiana, hivyo sasa nakusaidia.

JF ni user generated Forum, members wako huru kuanzisha mada yoyote, na members wako huru kuchangia, hivyo hakuna anayelazimishwa kusoma bandiko lolote au kuchangia bandiko lolote.

Unapokereka na mabandiko ya mtu yoyote, hatua ya kwanza ni ukikutana nayo, you just ignore na kusoma ile kitu roho inapenda.

Na kwa vile tuko members wa jinsia tofauti, kuna wenzetu wakiwa katika hali fulani, wanachefukwa, hivyo ikitokea na wewe ni mmoja wa kundi hili la kuchefukwa una kereka sana hadi kuharibu siku yako kila ukikuna na threads zangu, then jf imekuwekea utaratibu wa kukuzuia kukereka.

Kama ni hali tuu ya mapito, then, then bonyeza hapo kwenye avatar yangu, kisha bonyeza ignore, hutakaa uone tena thread yangu au post yangu yoyote, kipindi chote cha mpito.

Nakutakia kumaliza salama, tena mkimchukia mtu katika hali hiyo, utapata kinachomfanana!, hivyo utajaaliwa kidume!.

Wish you all the best.
P
 
Wanabodi,

Wanabodi, kila nipatapo fursa huwa ninawaletea makala ndefu za Kwa Maslahi ya Taifa, hivyo leo nimepata fursa tena naendelea na zile makala zangu za kuhamasisha uzalendo kwa jina la "Kwa Maslahi ya Taifa" ambazo zinaendeshwa kwa mfumo wa maswali, leo nazungumzia media za kimataifa zinafaidika nini kwa kuzusha uongo kuihusu Tanzania?, na hawa sources wao ambao ni Watanzania wenzetu, wanafaidika na nini kwa kuwa feed info za uongo, uzushi au kubuni?, what do they stand to gain?. Kuzusha uongo dhidi ya taifa lako na viongozi wake kwenye media za mabeberu ni uzalendo?!.

Ni muda mrefu baadhi ya vyombo vya habari vya kimataifa zikiwemo TV, Majarida na Online contents zao kutunga maurongo kuihusu Tanzania kumkashifu au kukashifu hatua mbalimbali zinazochukuliwa na rais Magufuli, katika maendeleo ya Taifa letu Tanzania, wao watabeza, watakashifu na sometimes hata kumtukana rais wetu, swali la kujiuliza ni vyombo hivi, vinapata faida gani kwa kututungia uongo au kutuzushia na kumzushia rais wetu Magufuli tuhuma za uongo?. What do they get or what do they wish to achieve?.

Katika janga hili la Corona, rais wetu Magufuli anasifiwa duniani kote kwa hatua alizochukua kupambana na Corona, ikiwemo kugomea lockdown, sasa hebu soma makala hii ya gazeti la The Guardian la Uingereza, jinsi ilivyo shehenezwa mauongo na mauzushi kuihusu Tanzania na rais wetu Magufuli!.
Tanzanian president accused of covering up Covid-19 outbreak

Wakati serikali yetu imetoa idadi ya vifo ni 16, na walioambukizwa ni watu 489, hawa jamaa kupitia source wao, wanadai eti Tanzania inaficha idadi ya vifo na maambukizi ya Corona, watu waliokufa kwa ugonjwa wa Corona kwa Dar es Salaam tuu pekee ni zaidi ya watu 400!, huku watu zaidi ya 20,000 wameambukizwa nchi nzima!.

Uongo kama huu una malengo gani?, wanapata faida gani kwa kuzusha uongo mkubwa kama huu?.

Kwa faida ya wale wavivu kufuata links, nakuwekea makala yote, nikiainisha nini ni kweli, nini ni uongo na nini ni uzushi,
Coronavirus outbreak
Tanzanian president accused of covering up Covid-19 outbreak
John Magufuli has repeatedly played down the threat from the pandemic
Jason Burke Africa correspondent
Wed 27 May 2020 17.43 BSTLast modified on Wed 27 May 2020 19.45 BST
President John Magufuli

My Take
Hawa jamaa wanapata nini kwa kutuzushia uongo?. What do they stand to gain?. Na nyinyi Watanzania wenzetu mmafaidika na nini kwa kuwa vibaraka wa mabeberu na kutunga uongo kuhusu nchi yenu?!.
Uzalendo wenu uko wapi?.

Nawatakia Alhamisi Njema

Paskali.
Kujaribu kuuficha ukweli ni sawa na kujaribu kuzuia mwanga wa jua kwa kiganja
 
Back
Top Bottom