DOKEZO Vyombo vya ulinzi na Usalama taarifa hii naomba muichukulie kwa uzito mkubwa

DOKEZO Vyombo vya ulinzi na Usalama taarifa hii naomba muichukulie kwa uzito mkubwa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Ninaandika haya kwa sababu nakupenda nchi yangu Tanzania kwa sababu na wewe unanipenda pia. Ninaandika haya kwa sababu sitamani hata siku moja kuona machafuko ndani ya nchi yetu nzuri ya kupendeza inayotamaniwa na kila nchi/kila mtu.

Japo nimeingilia kazi ya vyombo vya ulinzi na usalama vya nchi yetu naimani wenye kazi yenu mpo humu na kama yatakua na tija mnaweza kuyachukua na kama hayana tija mnaweza kuachana nayo japo naimani yatakua na tija kama sio kesho hata vizazi vijavyo.

Kazi ya ulinzi ya usalama wa nchi yetu ni jukumu la kila raia mwema mwenye mapenzi mema na nchi hii bahati nzuri sana mimi ni kati ya raia wema ninayeipenda nchi yangu Tanzania, binafsi kuna taarifa humu JF wakati mwingine ninazisoma kama story na zingine ninazichukulia kwa uzito mkubwa kati ya taarifa ambayo leo hii nimeichukulia kwa uzito mkubwa ni Ndugu "Vicent Karega Mnyarwanda kudai kuwa Waha ni wenyeji wa Rwanda".

Naanzia hapa hii taarifa ingekua imesemwa na mtu kama mimi pale Rwanda wala nisingejisumbua kuja na hili bandiko ila kwa sababu imesemwa na Vicent Karega basi imebidi nije na kuwapa vyombo vya ulinzi na usalama la kufikiri kidogo.

Who is Vicent Karega?

Baada ya kupitia vyanzo anuwai nimegundua huyu mtu ni mtu muhimu sana kwenye Serikali ya Rwanda chini ya Rais Kagame.

Vicent Karega alishawahi kuwa balozi wa Rwanda Nchini South Afrika, wote tunaelewa nini kilichowapata waliokua wanajeshi wa vyeo vya juu waliokua kinyume na Sera za Kagame na kuishia kwenda kuishi South Afrika wengi wao walikula vyuma waliuliwa kipindi wanakula vyuma huyu jamaa ndio alikua balozi kule.

isitoshe Vicent Karega alishawahi kuwa Balozi wa Rwanda nchi Democratic Republic of Congo wote tunaelewa kinachoendelea pale Drc chini ya M23 rais wa Congo amekua akitoa shutuma kila kukicha Rwanda ipo nyuma ya M23 sio ajabu hata Tp mazembe waliwekewa ngumu kuvaa yale maandishi.

Pia Vicent Karega Ubelgiji walimkataa kama Balozi wa Rwanda nchini mwao, tunafahamu kati ya nchi za Ulaya Ubelgiji ndio nchi yenye Intelijensia kali sasa kama wao walimkataa hatuwezi kujua sababu ila ajabu anaweza kuteuliwa kuwa Balozi Tanzania akapokelewa vizuri tu.

Baada ya kusoma ile taarifa humu Jf kuna maswali mawili matatu nimejiuliza

Vicent Karega anasema waha wapo karibia milioni 2 hebu tujiulize hizi takwimu kazitoa wapi na watu milioni 2 ni wengi sana jeshi zima la Urusi hata milioni 2 hawafiki je mpaka ametaka kufahamu idadi ana malengo gani ?

Akazidi kusema ni Kabila la tatu kwa ukubwa nchi Tanzania mimi binafsi sifahamu hizo takwimu ila Vicent Karega anazifahamu. Plse vyombo vya ulinzi na usalama najua mpo makini sana ndio maana tunalala usingizi mtamu ila naomba muongeze umakini zaidi hasa ujajusi.

Kwanini nimetoa angalizo nlishawahi kuja na uzi humu kuonyesha jinsi Urusi anavyopandikiza raia wake nchi za jirani na mwisho wake kudai raia wake wanaonewa na kuishia kuanzisha vita kafanya hayo Georgia, Ukraine, Finland, Chechnyia...nk sio ajabu leo nchi kama Finland inataka kujenga uzio kwenye mpaka wake na Urusi ili kuzuia warusi wasiingie Finland.

Je mpaka Vicent Karega ameamua kusema haya anataka kupima Tanzania itareact vipi binafsi ningependa sana nchi kama nchi itulie isijibu kitu, Je wameshamaliza kuipeleleza nchi yetu na kufahamu ubora wetu na udhaifu wetu sitaki kuamini katika hilo.

Ni kweli Watanzania tunapenda sana wageni ila kwa dunia ya sasa ni vyema tukaanza kuangalia maslahi ya nchi kwanza turudi kwenye lile Somo letu la Uraia Ulinzi na Usalama ni Jukumu la Kila Mtanzania.

Vvyanzo vya habari.

View attachment 2810918
View attachment 2810919
Wanyarwanda RPF wanaamini watanzania ni wapumbavu na hawana uwezo wa kijeshi kupambana nao .Na wana mpango wa kuchukua maeneo ya Karagwe na Ngara kwa nguvu,,sema tu uwepo wa JWTZ hasa wale makomandoo wa mipakani unawatatiza na wanajua 1994 bila usaidizi wa JWTZ special forces wasingeweza kuwashinda RDF.Na RPF wanaamini kua Waha na Wahangaza na Wanyambo ni sehemu ya wanyarandwa.

Vicent Karega namjua na ndio anataka kumrithi Kagame afu siku awapime watanzania kijeshi na yamkute yale yaliyomkuta Iddi Amini.

EVERYBODY KNOWS KAREGA ALICHOKIFANYA KWA WAKIMBIZI WA KIHUTU NCHINI RWANDA NA ZAIRE 1994 UP TO 1999
 
Rwanda ipo siku tutaitawala EA yote na hakuna atakayekohoa.
Thubutu...
Mjomba mwenyewe mara kibao tu amekataa kuizungumzia Tanzania
Sababu anajua outcome ya ukabila kwenye siasa za kinyarwanda.
Bahima (Makabila ya Mtemi Kintu) wenyewe hatupendani,,sasa tutaitawala vipi afrika mashariki yenye makabila 3000 na nchi pekee zenye ukabila ni Rwanda na Burundi na DRC na South Sudan.
 
Haha jidanganye labda Paul Kagame nife kesho
 
Tukiacha jokes za jf,ila pk kajipenyeza seemu zote nyeti,ule mpango wa bahima empire kuitawala Kanda yote ipo siku itatimia

Bila wazee kumaliza mission flan huenda Leo mpango ungeshakamilika
Hakuna kitu mkuu.

Tuulize sisi tunaojua kabila la kinyarwanda.

Wanyarwanda wanashindwa kuelewa kitu kimoja, watanzania tuna msingi yetu japo kuna makabila 400 hivi na hatuna ukabila wala udini linapokuja suala la kitaifa.

Bahima ni makabila yote yanayotokana na ukoo wa Kintu.

Koo pekee za kitusi na kihutu zinazozungumza kinyarwanda ndio zenye roho mbaya ya ubaguzi
 
Bora tu huyo Kalega aje kutukomboa kutoka makuchani mwa mkoloni mweusi (CCM). Nchi ikiwa na amani sisi tunanufaikaje wakati mifisadi tu ndiyo inafaidi rasilimali za nchi hii
Mkuu bila CCM hakuna Tanzania.
Na CCM sio watu ni taasisi
 
Umefanya vizuri kutoa la moyoni. Ila ukweli ni kwamba kwa kazi za wana usalama, hilo ni jambo dogo. Kwamba fulani kasema? Ana haki ya kuongea anachokitaka. Kwani ni wapi kadai waha warudi Rwanda? Unadhani Rwanda hakuna waha? Watu weusi walifikaje Marekani? Au wazungu walifikaje South Africa?

Kwa umri wako, ni utoto unaokusumbua. Hata kila mhamiaji aliyepo nchini unadhani hajulikani? Siku ajitose kuleta vurugu, ndo utajua hivyo vyombo vinafanya kazi.

Ushabiki wa kinafiki hauna maana. Kwani akidai waha ni wa Rwanda, akaomba hao waha warudi kwao, unapungukiwa nini? Hao waha, leo hii ukiwambia rudini kwenu, wataenda?

Hata yeye ni binadamu, kuongea tofauti na uhalisia ni jambo la kawaida. Kama lina uzito, ulisikia serikali inatoa jibu lake kuhusu hilo? Acha utoto.
 
Mkuu hujamuelewa mtoa mada
 
Hakuna kitu mkuu.
Tuulize sisi tunaojua kabila la kinyarwanda.
Wanyarwanda wanashindwa kuelewa kitu kimoja,,,watanzania tuna msingi yetu japo kuna makabila 400 hv na hatuna ukabila wala udini linapokuja suala la kitaifa.
Bahima ni makabila yote yanayotokana na ukoo wa Kintu.
Koo pekee za kitusi na kihutu zinazozungumza kinyarwana ndio zenye roho mbaya ya ubaguzi

Wabongo tunapenda Sana kujifariji laiti tungejua,hao miamb wanawatu wao Hadi wa kufoji vyeti na kuingizwa jeshini rasmi

Siibez nchi yangu,ila hakuna muda wa kua makini hivi sasa na baadae
 
Wabongo tunapenda Sana kujifariji laiti tungejua,hao miamb wanawatu wao Hadi wa kufoji vyeti na kuingizwa jeshini rasmi

Siibez nchi yangu,ila hakuna muda wa kua makini hivi sasa na baadae
Kua na majasusi ni kitu kimoja.
Na kua royal ni kitu kingine.
You cant buy royalty
 
ndio wanasemaga tusome vitabu vingi. Alafu tuwaze nini, kuna kuwaza upuuzi usio na mbele wala nyuma😂😂😂😂.
Simsemi mtoa mada, wala sisemi amekosea.
Ila live huu ni upuuzi.
 
Back
Top Bottom