Wewe ni mwandishi wa habari? Kabisaaaa? Kama wa FDRL sawa. Si kwamba nakupinga au nakutukana, hapana. Na si kwamba nalazimisha uandike navyotaka mimi, la hasha. Ila kama kweli umedhamilia kusimamia taaluma yako, naomba wakati unaandaa makala, usiegemee upande wowote. Kama kweli wewe ni mwandishi professional, jiulize mada yako wanasoma wangapi, wanakuelewaje, upindishapo ukweli unaelewekaje! Mimi si mwanasiasa wala sipendi hayo mambo, lakini, mambo mengine usikurupuke, fanya utafiti wa kina, na wa kina zaidi.
Ntapenda nikuulize kitu. Kuhusu M23. Unafurahia watu wanavyochinjwa? Kwa nini wachinjwe? Wenyeji hawajali, majirani hawajali, lile genge linalojiita UN halijali, lakini ukiangalia taarifa zinazoandikwa, kana kwamba kuna kundi linalofagilia unyama unaoendelea, na lingine linakemea.