Vyuo Vikuu Binafsi vinalipa mishahara midogo sana

Vyuo Vikuu Binafsi vinalipa mishahara midogo sana

Vitabu
Vitini
Course outline
Mitihani
Nk....

Jumlishia kwenye mshahara apo....
So hela ya mshahara plus hela ya hayo mazagazaga hapo juu inatosha kbs
Hata mie nashangaa hapa.
 
Kuna hicho kinaitwa MTO JORDAN kipo pale Morogoro kama unaenda Dsm aisee kinaajiri kila siku hakilipi watumishi wake.

Ukipata ajira pale hata usisumbuke kwenda
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Naona wengi tunaongea kama waajiriwa, jaribu kuwaza kama mwajiri. Idadi ya wanachuo haiongezeki, ada haiongezeki hapo mshahara utaongezekaje? Ukiwaza hivyo hutalaumu mtu. Kama ni mwajiriwa Utavumilia au utaondoka kwenda kwenye nyasi za kijani
 
Magufuli alikomesha uhuni uliokuwa unaendeshwa na vyuo binafsi. Akuvifunga ila vilijifunga vyenyewe kwa kutotimiza vigezo.

Mfano, Vyuo vilikuwa vinaokoteza ma lecturer! Mtu mwenye degree moja, tena grade ya chini anaajiriwa kufundisha wanafunzi wa degree. Mishahara hawalipwi wengine wakawa wanaongeka ovyo ili kufaulisha wanachuo!
Kwa upande huo upo sahihi. Lakini hata sehemu chache waliko fanya vizuri hakupenda hata kidogo. Angeweza kuwabana waliofanya uhuni wakabaki wachache wazuri tungekuwa na private universities chache zenye quality nzuri sana.
 
Sasa kama hakuna wateja wa kutosha (wanafunzi) unafkri watatoa wapi pesa za kukulipa 3 million?...

Usisahau pia chuo kina husika katika kulipa kodi kila mwezi, na gharama zote ambazo ni maji,umeme, ulinzi, N.K

Swala la msingi hapo ni kwamba hawana pesa za kutosha kulingana na hali ya wanafunzi kuwa ni chache.
 
Tanzania nadhani tumerogwa, yaani msomi wa level ya kuitwa lecturer na ambaye tunakutegemea uzalishe wataalam wengine unakuja huku jamiiforums kulia kulia kuhusu mshahara? Kwamba hata haki zako huzijui? kwamba hutambui kuwa ajira siyo jela usubiri msamaha wa Rais?
Ukienda CMA unakuwa umewapelekea ulaji wasuluhishi, chuo kinawapa mtonyo kesi inapigwa chini, unakuwa umefanywa daraja😀
 
Noma sana..mbona darasani wanaonekana wanaoesa mingi!!
 
Kichwa cha habari chahusika.

Vyuo vikuu binafsi nchi hii ambavyo vingi vinamilikiwa na taasisi za dini wanalipa wahadhiri wao mishahara midogo sana. Huwezi amini mishahara ni midogo kuliko hata walimu wa shule za sekondari. Kwa mfano Mhadhiri msaidizi analipwa Tsh Milioni moja kabla ya makato.

Mbaya zaidi wengine wamekaa na mishahara hii kwa miaka zaidi ya 20, wengine 15 na wengine 10. Waajiri wa hivi vyuo hawajui kitu kinaitwa nyogeza ya mshahara.Hata hii nyogeza ya mama Samia hawataongeza maana nyogeza nyingi zilishapita hasa kipindi cha JK lakini wao haikuwahusu.

Kiukweli wafanyakazi wanaishi kama watoto yatima hakuna wa kuwasemea, Siyo idara ya kazi wala Wizara yenyewe. Wafanyakazi wa umma wao wana wazazi hawa hawana. Lakini tukumbuke wanaofanya kazi kule ni watanzania na wanafunzi wanosoma vile vyuo ni watoto wetu wa kitanzania. Kwanini Serikali kupitia vyombo vyake haifuatilii hivi vyuo?

Naomba serikali itembele hivi vyuo ikaone hali halisi na iwasaidie wahadhiri wale ktk unyanyasaji huu mkubwa. Ifuatilie ipate ukweli wahadhiri wamekaa miaka zaidi ya 20 bila nyongeza yoyote.

Hata THTU haina habari maana haina matawi ktk vyuo vingi. Jamani wahusika timizeni wajibu wenu kuwasaidia watanzania wenzenu.
Pesa zinazolipwa na wanafunzi zinaishia wapi
 
Labda wanaofundisha mikoa yenye vyuo vichache eti mwalimu kwa wiki anakipindi kimoja muda unaobaki ni kufanya utafiti na mwisho wa mwezi analamba 2.5 huyo wa masters na anapiga part time vyuo hata viwili tena na wengi bado wana mishe zao binafsi kwa wanaofundisha sheria wana law firms zao sasa kulia njaa ni uvivu wake tu.
 
Elewaga dhana ya mshahara usitaje vitu vya ajabu. Na ambao siyo wanasheria? Hizo law firms walio nazo ni wachache.
 
Elewaga dhana ya mshahara usitaje vitu vya ajabu. Na ambao siyo wanasheria? Hizo law firms walio nazo ni wachache.
Sasa uzi ulianzisha wa nini kumbe umeshapanga majibu unayotaka,na kwanza nani aliyekuambia ukiwa mwalimu wa chuo umetusua maisha au ulijua utafundisha tuition huko walimu sijui mkoje yaani mmekuwa watu wa kulialia tu na kuendekeza vimikopo njaa na hapo unakuta unafundisha kachuo ka ufundi mi nikajua naongea na DR. kumbe kajamba nani tu mwalimu wa chuo wa mchongo.
 
we hujitamabui, nenda kakojoe, ngedere mkubwa. Nania kakuambia mi mwalimu. Akili yako ina kwashiakor
 
Back
Top Bottom