Vyuo vya private na migpa mikubwa kwa nini?

Vyuo vya private na migpa mikubwa kwa nini?

ngoja nikuambie kitu, private universities hata waalimu wao hawana vigezo vya kufundisha university! Nimemaliza chuo cha serikali, kuna jamaa zangu wa3 wote wana gpa za 3.1. Mmoja anafundisha saut, mwingine mwenge, mwingine ruco.. Unategemea nini kuajiri wasiojua...obvious hata mwanafunzi akiandika pumba atampatia marks tu.

Naomba management za vyuo private waangalie kuanzia kwenye kuajiri, wazingatie 3.5 and above!

ni kweli kabisa. Wote wanaomshambulia mtoa mada ndo walewale wanaolinganisha matokeo ya kidato cha nne na chuo kikuu. Hii nchi bado ina wajinga wengi sana.
 
special schools zimekumbwa na competition kutoka kwa private schools,lakini kwa upande wa vyuo govt schools zina competitive advantage kubwa. Vyuo vya private havijajega competitive advantage kubwa ndio maana watu wengi hawaendi kwa moyo wote.kama unabisha ntakupa ukweli zaidi
KWA KIASI FULANI.
lakini ukweli ni kwamba, kwa hali ilivyo sasa uwezo wa kuchukua wanafunzi kwa vyuo vya serikali umezidiwa kabisa na idadi ya wanafunzi na huwezi kunishawishi kuwa eti wote wasioenda vyuo vya serikali si bora. wapo wengi sana walio bora na hata wenye matokeo mazuri, maana kuna tofauti kati ya ubora wa mwanafunzi na ubora wa matokeo. UBORA WA MWANAFUNZI NI NATURAL IQ LAKINI UBORA WA MATOKEO NI MATOKEO YA MAZINGIRA MAALUMU, ambapo mtu anaweza kuwa bora akawa na matokeo ya kawaida kulingana na mazingira mabovu and the like.

lakini kubwa kwa hoja yako ni kwamba, competeive advantage kwa sasa ni kubwa hata vyuo vya private kulingana na kozi. mathalani kuna vyuo vitatu tu vya engineering Tanzania, COET ,UDOM AND coet ya SJUIT na ukiangalia uwezo wa vyuo hivi bado haviwezi kuhudumia wanafunzi wote waliopo na waliofaulu na hapa wengi wanaachwa japo wamefaulu
 
Wakuu nimefanya utafiti kwenye vyuo vya PRIVATE kama SAUT,RUCo(Ruaha university college),MWENGE UNIVERSITY,JORDAN UNIVERSITY,ARUSHA UNIVERSITY,ST.JOSEPH UNIVERSRTY,TUMAINI DAR,TUMAINI IRING,TUMAINI MAKUMIRA,ST.JOHN,TEKU,SEKOMU,EUKENFORD,nikagundua kwamba wanagraduate na G.P.A kubwa sana yaani unakuta G.P.A za 4 zimejaa hadi unashangaa ! na tunajua kabisa asilimia kubwa ya wanafunzi wanaochukuliwa kwenye hivi vyuo vya PRIVATE wamepata division three zile mbaya mfano,15,16,17,! Hebu tujadili wakuu kwa nini hivi vyuo vya PRIVATE wanapewa G.P.A kubwa sana je ni sababu za kibiashara

Nakushangaa kwa nguvu zote. Mi nimesoma saut na sijawahi pata division 3 sio o level wala a level. Nimepata one kali o level na two ya mwanzo a level. Na sijawah shika nafasi chini ya tatu toka nimeanza primary. I went to saut by choice and not forced by points. Nimesoma na watu flani masters udsm na walikua wanaonekana wakali cha kushangaza walikua wanajiandika kwenye pindo za mashati sie ndo tunawaona. Hiki unachosema hapa ni ujinga mtupu
 
I dont care umetoka chuo gani au una Gpa ya namna gani. Ninachojali unauwezo gani wa kuonesha ulichojifunza kwa vitendo na ubora zaidi? HILO NDILO SWALI KWENYE SOKO LA AJIRA SIKU HIZI, VINGINEVYO JE UNA CONNECTION?
 
Mkuu kuna mwalimu mmoja anatoka chuo cha TUMAINI alikuja kufundisha partime taboraboys yaani hajui kitu linakazi ya kujisifia eti ana G.P.A kubwa

Kufundisha nacho ni kipaji m2 anaweza akawa na material ama akawa na.GPA nzuri bt hawezi kupresent material kwa wanafunzi,
 
Eti unakuta chuo miG.P.A ni mikubwa hadi unashangaa! cha kushangaza ni kwamba wanachukua vilaza sugu! ni bora wangekuwa wanachukua CREAM nisingeshangaa kuona miG.P.A mikubwa

Basi kinakuuma kama wameleta div v unashangaa hilo tu na bora hizi product zinazomaliza miaka hii ambao unawadharau kuliko hicho kizazi cha div v kinachokuja
 
KWA KIASI FULANI.
lakini ukweli ni kwamba, kwa hali ilivyo sasa uwezo wa kuchukua wanafunzi kwa vyuo vya serikali umezidiwa kabisa na idadi ya wanafunzi na huwezi kunishawishi kuwa eti wote wasioenda vyuo vya serikali si bora. wapo wengi sana walio bora na hata wenye matokeo mazuri, maana kuna tofauti kati ya ubora wa mwanafunzi na ubora wa matokeo. UBORA WA MWANAFUNZI NI NATURAL IQ LAKINI UBORA WA MATOKEO NI MATOKEO YA MAZINGIRA MAALUMU, ambapo mtu anaweza kuwa bora akawa na matokeo ya kawaida kulingana na mazingira mabovu and the like.

lakini kubwa kwa hoja yako ni kwamba, competeive advantage kwa sasa ni kubwa hata vyuo vya private kulingana na kozi. mathalani kuna vyuo vitatu tu vya engineering Tanzania, COET ,UDOM AND coet ya SJUIT na ukiangalia uwezo wa vyuo hivi bado haviwezi kuhudumia wanafunzi wote waliopo na waliofaulu na hapa wengi wanaachwa japo wamefaulu
ardhi wanatoa engeneering mkuu vitatu?udom wanatoa,dit wanatoa,must wanatoa arusha tech wanatoa ,mandela,.umechapia hapo mkuu
 
kumekuwepo na wimbi kubwa la watu na hata mada zikibeza na kutilia shaka uwezo na ubora wa vyuo vya binafisi kiasi cha wengine kuviita majina ya ajabu ajabu.

kwa mkutadha huo nimeona bora niwaeleweshe wote wanaojigamba kwa majina ya vyuo vyao na si ubora wao kuwa elimu waliyoipata bado haijawasaidia na hawajakombolewa na kuwajengewa uwezo wa kufikiria,kung'amua na kutambua ukweli halisi ulivyo na nitawashauri warudi darasani wakasome upya ili wapate uwezo wa kuona mambo kwa usahihi wake.

BACK TO TOPIC.
napenda kuweka wazi ukweli huu na watu waniambie kama ni sahihi kwa wanavyofikiria.

1.mfumo wa elimu ya tanzania kuanzia form one mpaka form six unazipendelea shule za serikali kwa kuzipa nafasi ya kuchagua wanafunzi waliofaulu tu na makapi wanaachiwa ndugu zangu wa private.


-shule za serikali form one zinachukua wanafunzi walio na ufaulu wa juu na kwa kiasi kikubwa wanafunzi wanaokosa kuchaguliwa kwa sababu ya marks zao kuwa za chini wanaenda kujaribu bahati yao private.

-matokeo ya form two necta yakitoka shule za private pamoja na kwamba ziliachiwa wanafunzi wengi wenye marks za kawaida zinaibuka kidedea dhidi ya shule za serikali ambazo zilichagua wanafunzi wazuri tu

-matokeo ya kidato cha nne yakitoka shule za private zinafanya vizuri tena kuliko za serikali pamoja na kwamba shule za serikali zilichagua wanafunzi wazuri tu.


MAELEZO HAYA YANATOA FUNDISHO KUWA ELIMU YA SERIKALI SI BORA KULIKO YA PRIVATE NA SERIKALI KAZI YAO NI KUHARIBU FUTURE ZA WATOTO ALAFU WANAWAACHA ILI TENA WAOKOLEWE NA PRIVATE SCHOOLS KIDATO CHA TANO NA SITA BAADA YA KUACHWA.

mimi mwenyewe ni mwathirika maana darasa zima tulikula za uso kwenda form one hakuna hata mmoja aliyepenya,ndipo wanafunzi watano tukaokolewa na private ya huko home na kati ya hao ni mmoja tu ndio alishia form four ila wengine walichanja mbuga mpaka vyuoni.


SABABU ZA UBOVU WA ELIMU SERIKALINI ZINAJULIKANA NA SITAZITAJA ILA ITOSHE TU KUSEMA KUWA SABABU NYINGI ZINAZOATHIRI ELIMU SEKONANDARI HATA KWENYE VYUO VIKUU VYA SERIKALI SABABU HIZO ZIPO NA ZINAFANYA KAZI YA KUPUNGUZA UFAULU WA WANAFUNZI HUKO ALAFU WENYE KUKOSA MAARIFA YA KUFIKIRI WANASEMA WAKIPATA GPA NDOGO NDO ELIMU ILIKUWA NZURI KUMBE WAMEATHIRIKA NA MAZINGIRA MABOVU ZIKIWEMO TARATIBU.

-wanafunzi wanaofeli form four kwa kupata angalau three ya mwisho na four za mwanzo serikali inawaacha ambao wengi wao ni wa shule za serikali na ndio hao serikali ilituambia ndio waliostahili kusoma ilipowachagua form one,hawa wanafunzi inabidi waende private kutafuta bahati yao huko, wengi wao kati ya hawa huwa wanafaulu tena na kuthibitisha kumbe wanaweza kufaulu ila walifeli kulingana na kusoma serikalini na si ajabu tena hawa serikali ikawataka.


KIFUPI NI KWAMBA PRIVATE SECTORS WAMEONYESHA UWEZO MZURI WA KUWAFUNDISHA WATOTO NA KUFAULU NA HAPA HAKUNA ANAEBISHA KWA SABABU WANAFUNZI WOTE WANASOMA KWA SYLLABUS MOJA NA MITIHANI NI ILE ILE ILA TATIZO LINAKUJA VYUONI AMBAPO WATU HAWANA SAME SYLLABUS NA MITIHANI YAO NI TOFAUTI NA NDIPO UNAANZA KUSIKIA MAJINA YA AJABU AJABU KWA HIVI VYUO KISA WANAFUNZI WAKE WANA GPA KUBWA.

mfano wanafunzi wanalundikwa lecture hall ukute wapo 400,humo wapo hawasikii kabisa najua maana wanafunzi wengi wanakimbilia mbele ili angalau wasikie na wakichelewa wanakaa nyuma na kusikia ndo inakuwa utata,wengine hawaelewi lakini hawawezi kusema hawaelewi na inabidi wakaushe tu nk nk alafu wakipata GPA ndogo wanalalamika wanapoona wale wa vyuo vya vitongoji wamepata GPA kubwa wakati wenzao walifundishwa darasani wanafunzi 40 tu,wasipoelewa wanauliza na wote wanasikia,lecturer akizingua ama haeleweki analipotiwa na kubadilishwa ama kutimulimuliwa.


mbona hamsemi mashule ya private yanavyofanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa ambapo kuna mtihani mmoja?


ama huko hamuoni kama wanapata one na two wengi na hata one kali kali kiasi hata cha tanzania one wengi kutokea huko?

nini tofauti ya mifumo ya shule za private na vyuo vya private katika ufanisi?nini tofauti ya shule za serikali na vyuo vya serikali katika ufanisi?

mbona pia hamuulizi kwa nini shule za serikali pamoja na kujichagulia wanafunzi wazuri lakini bado zinafelisha badala ya kufaulisha?

ingekuwaje kama siku moja shule za private zichague wanafunzi waliofaulu alafu makapi yaende serikalini?watu wangetoka kweli?haki ya nani itakuwa kiama,naamini hata division four zinaweza kukosa kabisa kwenye necta na wanafunzi wote kubaki na zero.


ingekuwaje kama mfumo wa elimu ungetaka kuwa wanafunzi wa shule za binafisi waendelee kuwa wa binafisi mpaka vyuoni?kwa kuwa wanafunzi wa shule za serikali ndio wanaongoza kufeli je mpaka kufikia form six kuingia chuoni serikali ingebaki na asilimia ngapi ya wanafunzi ilioanza nao na je ingeonekanaje kama ubora ungeangaliwa kwa ufaulu tu kama wanavyofanya watu wetu wenye uwezo mdogo wa kufikiri?hizo one nyingi leo sizingekuwa private universities?



2.udahili wa vyuoni na hoja za wanaosema vyuo vya watu binafisi havina ubora.

-kwanza vyuo hivi vinadahili wanafunzi wenye marks za chini sana mpaka hata three za 17 lakini mwisho wanapata GPA kubwa za 4 na kuendelea(si maneno yangu bali ni hoja ya watu hao)

MAJIBU KWA HOJA HII.

kabla hujafikiri chochote kuhusu majibu kwa hili unapaswa kujua pia kwa nini shule za private zinachukua wanafunzi hata waliofeli la saba lakini wanaibuka na one?

unapaswa pia kujua kwa nini shule za private zinachukua wanafunzi wenye three za mwisho na div four kusoma advance alafu wanaibuka na division one na two na hata three kwa combination zote hata za sayansi?


HAPA SITAKI KUPIGIA DEBE SHULE NINAYOIJUA ILA NAJUA KAMA WATU NI WAJASIRI WATAKUJA HAPA KUTOA USHAHIDI KUWA WAO WALIPATA FOUR O LEVEL SHULE ZA SERIKALI ILA WAKAENDA PRIVATE NA KUIBUKA NA ONE AMA TWO YA FORM SIX NECTA NA WALIENDA UDSM AMA UDOM AMA MZUMBE AMA SUA.

UKISHAPATA MAJIBU HAYO NI VYEMA UKAJARIBU KUYAUNGANISHA TENA KWA MATOKEO YA GPA KUBWA ZA VYUO VYA BINAFISI.

JE UMEWAHI KUJIULIZA INGEKUWAJE KAMA VYUONI KUNGEKUWA NA PAPER MOJA KWA VYUO VYOTE?JE PRIVATE WANGEONEKANA MABOYA AMA WANAWEZA?hayo majibu kila mtu anayo yake.

-UBORA WA WANAFUNZI WA CHUONI UNAPATIKANA KWA VIGEZO VIPI HASA?

nimefatilia kwa kiasi kikubwa kwa wenye hoja hizi nikabaini wanaangalia matokeo ya wanafunzi ya kidato cha sita tu huku mengine wakiyaacha kabisa kuyaangalia.

NASEMA KUNA MAKOSA MAKUBWA SANA HAPA NA WATU HAWATAACHA KULALAMIKIA VYUO VYA BINAFISI KWA SABABU YA UFINYU WAO WA KUFIKIRI NA NDIO MAANA NIMESHAURI HAWA WARUDISHWE TENA SHULE UPYA WAKAJENGEWE UWEZO WA KUFIKIRIA.

MAPUNGUFU KATIKA HOJA YA MATOKEO KAMA KIPIMO CHA UBORA WA MWANAFUNZI.
-kwanza matokeo yanayotazamwa na wengi ni ya form six pekee,hawajui kuna wanafunzi wana one na two za form six na wapo udsm ama udom ama mzumbe ama sua ila form four walikuwa na four ama three za kuchechemea na waliokolewa na private, ama hawajui kuna wanafunzi wana three za 17 form six ila wana wana one za single digit O level ila kisa wapo vyu vya kitongoji ni tatizo.

SASA JE TUTUMIE MATOKEO YAPI KUSEMA HUYU MWANAFUNZI NI BORA?TUKITUMIA YA SIX NI MWAKE ATAONEKANA ALIFAULU VIZURI LAKINI TUKITUMIA YA O LEVEL NANI ATASEMA HUYU NI MWANAFUNZI BORA?
swali kwa nini mnatumia hasa matokeo ya kidato cha sita tu na mnasahau kuchukua historia ya matokeo yote mpaka ya form four?

mbona udsm ina watu walikuwa na four O Level ama nacho ni chuo cha kitongoji? NAJUA WATU WATASHANGAA HAPA LAKINI NDIO UKWELI WENYEWE.

KIDOGO NINGEPENDA KUELEZA KWA NINI UDSM INACHUKUA WANAFUNZI WENGI WENYE MATOKEO MAZURI YA FORM SIX.

kwanza udsm ni chaguo na ndoto za wanafunzi wengi kusoma hapo(ila haikuwa mimi) na sababu ni za kihistoria,mpaka leo ndicho chuo kinachojulikana na wengi hasa watu wa zamani ambao ni wazazi wetu kwa hiyo wengi tumejengwa tokea mwanzo kuwa hicho ndio chuo kikuu,ukisema kwingine wazee wanakushangaa sawa na watakavyomshangaa mtu atakaekuja hapa aseme yeye ni engineer wa kemikali mana wao wanajua injia ni yule wa civili engineering tu.

kwa hiyo udsm inapata request nyingi sana na wote tunajua utaratibu wa kuchagua ni kuanza na aliye bora zaidi kushuka chini,japo nao udsm wanaangalia sana matokeo ya six na ndio mana hawajali sana kama o level uligonga four ama three ya mwisho.

na sababu nyingine ni kwamba udsm ina uwezo mdogo wa kuchukua wanafunzi wanaostahili kusoma degree,na ninawahakikishia kuwa hata wanafunzi wenye div three za 17 wapo eligible kusoma udsm kama tu wana C tatu O level na principle mbili Advance ila kutokana na uwezo mdogo wa udsm ku accomodate wanafunzi ndio inawaacha.



-sababu zilizopelekea hawa wanafunzi waliofeli kufeli hazizingatiwi katika kuangalia ubora wa wanafunzi,mtu katoka shule ya serikali haina hata walimu amekomaa mwenyewe akapata three yake ya 17 alafu unasema hana uwezo wa kupata GPA ya 4.5 kumbe anao uwezo kama akifundishwa na kupewa kila kinachostahili. na wanapofika vyuo vya private elimu inaonekana kumbe ni nyepesi maana wanafundishwa vizuri,sasa kwa ni nini wasifaulu na kupata GPA ya 4?

ngoja nitoe mfano mmoja,kuna shule moja kali ya private arusha nilimtembelea rafiki yangu ambaye ni sister(katoliki) na yeye ndo alikuwa mkuu wa shule ile,ilikuwa kipindi cha kuchagua wanafunzi wa kuingia kidato cha kwanza.
kwa kuwa ananiamini sana akaniambia nisahishe mitihani ya kiingereza nikakataa,baadae akaniambia nisahishe ya hesabu nikakataa ila akanilazimisha,ikabidi nikubali,nikasahisha na marks za wanafunzi wote zikawa tayari.

sasa vigezo vya shule ile kuchagua wanafunzi ndio vilinishangaza ila nikajifunza kitu baada ya kuelekezwa.

-kwanza wanaangalia mwanafunzi katoka wapi?na shule ipi?na kukoje huko?hapa wanaweza kumchukua mwanafunzi hata mwenye marks ndogo kabisa ila ameonyesha uwezo fulani baada ya kuangalia alikotoka na kubaini kuwa huyu katoka eneo ambalo elimu iko chini sana na hivyo atakuwa mzuri ila mazingira ndio yanamfanya asijue. ama wanaweza kumuacha mwanafunzi mwenye ufaulu wa wastani aliyetoka shule bora kabisa japo amefikisha marks kwa kuangalia kuwa amepata marks za kawaida sana pamoja na kuwa katika mazingira bora zaidi na shule bora zaidi.

sister akanipa mfano wa mwanafunzi aliyekuwa form three wakati ule 2012 ambaye ndio alikuwa akiongoza darasani,akaniambia yule mwanafunzi alipata marks ndogo sana ila walilazimika kumchukua kwa kuwa waliona katokea ndani kabisa maporini huko arusha kwa wamasai ambako elimu ni kitendawili na walihisi atakuwa mzuri sema tu huko elimu ni mbovu kupindukia,alipoanza form one wakadili nae kumfundisha english kwa ukaribu zaidi na baada ya mwezi wa sita tu akaanza kuongoza mitihani ya shuleni licha ya mwanzo kuanza na namba za mwishomwisho,aliongoza necta ya form two na hata form three bado alikuwa moto.


NADHANI PIA MMEJIFUNZA KITU HAPA JUU YA UBORA WA MWANAFUNZI KUWA UNATEGEMEA MAMBO MENGI SANA NA HATA UFAULU WA MWANAFUNZI UNATEGEMEA MAMBO MENGI SANA IKIWEMO YEYE MWENYEWE NA MAZINGIRA YA SHULE AMA CHUO

MWISHO NINGESHAURI WATU MJIPAMBANUE KWA MAFANIKIO YENU BAADA YA KUMALIZA VYUO KAMA UBORA WA ELUMU YENU NA SI KULAZIMISHA KUPATA SIFA KISA UMESOMA CHUO FULANI AMA KUMUBEZA MWINGINE KISA KASOMA CHUO FULANI.

tunataka akina Stive Jobs hapa,tunataka kina Newton hapa,tunataka kina Eisten hapa,tunataka kina GALILEO GALILEI hapa na wengine wengi,hatutaki majina ya vyuo ama shule. show your quality of education to innovations and is when we shall appriciate your quality,UNLESS YOU ARE A NORMAL PERSON WITH A NORMAL QUALITY.



Mkuu asante kwa uchambuzi wako, we acha waendelee kulilia GPA wakati vichwani watupu, Nawahakikishia leo hii hata tukikupa GPA ya tano, kama wewe ni mburula ni mburula tu na kama wewe una uwezo unao tu, haijalishi ulijificha kichaka gani (Chuo cha Private or Government). Ndio utaona sasa kwanini maofisini kuna watu waliotoka huko private, Nashauri interview za kazi ziendelee kua tight ili taka zote toka vyuo vya serikali na Private ziishie mtaani tu.
 
Jamani,penye ukweli tuseme ukweli,kuna kipindi nlikua nafanya kazi bank flan hapa tanzania,wakawa wanaajiri wanafunzi kulingana na Gpa zao,mwisho wa siku wakajikuta wameajiri watu wengi kutoka vyuo vya private ambao walikua na ma GPA makubwaa..mbona walijuta kuwaajiri,mtu akiwekwa hata teller anashndwa kurudisha chenji kwa wateja.ikafikia hatua MD wa hyo bank akasema ni bora kumuajiri mtu mwenye matokeo ya kawaida kutoka vyuo kama udsm au mzumbe kuliko kuajiri wale wenye gpa kubwa kutoka vyuo vya private.
 
Private Uni hyo ni strategy ya kuwapromote wanafunzi wao kwenye soko la ajira,baas...wasipowabeba hela watatoa wapy jina lachuo likichuja?
 
Mkuu kuna mwalimu mmoja anatoka chuo cha TUMAINI alikuja kufundisha partime taboraboys yaani hajui kitu linakazi ya kujisifia eti ana G.P.A kubwa


kumbe uko form 6
 
Chenga tu huko private wanatafuta wateja tu ukitaka shule vyo vya serikali hata kufika gpa ya 2.5 shughuli reference: kasome udsm(national university)
 
yan mi sijaona kitu cha kubishana khs private and govt university. la muhimu ni kujadiliana na kusaidiana namna gani tufanye ili tuibadili nchi yetu hii iliyo na majanga kibao.By the way uwe umesoma private au govt, je unaweza kuendesha maisha yako? na taifa kwa ujumla, mengine hayana maana hata tukibishana mpk kesho mshindi hawez patikana
 
Wewe halafu MANAGEMENT nyingi za vyuo vya private wanawakomand WAHADHIRI wawape G.P.A kubwa

jamaa wanalalamika et GPA kubwa vyuo vya private.
Mbona watu walio serious gvt tunapiga GPA kubwa kishenzi tuacha mambo ya ajabu tatzo walioko vyuo vya gvt wanajarbu kuja na historia za 4m6 et div 1,2. ukwel ni kwamba wanajisahau na kula bata mm shaidi nipo ud tena COET lkn GPA kama 4,zipo sasa kaa unalalamika utakoma kwenye soko LA ajira achane urmbuken na mademu someni .name matokeo ya div hayana msaada.kumbuka % kumbwa wenye div 3 na 4. adv wanakuwa na juhud za kusoma wafikapo chuo zaid ya wajihita wana matokeo mazur adv.Hinawezekana kupata GPA kubwa hata ukiwa vyuo vya gvt issue KUJiTAMBuA
 
jamaa wanalalamika et GPA kubwa vyuo vya private.
Mbona watu walio serious gvt tunapiga GPA kubwa kishenzi tuacha mambo ya ajabu tatzo walioko vyuo vya gvt wanajarbu kuja na historia za 4m6 et div 1,2. ukwel ni kwamba wanajisahau na kula bata mm shaidi nipo ud tena COET lkn GPA kama 4,zipo sasa kaa unalalamika utakoma kwenye soko LA ajira achane urmbuken na mademu someni .name matokeo ya div hayana msaada.kumbuka % kumbwa wenye div 3 na 4. adv wanakuwa na juhud za kusoma wafikapo chuo zaid ya wajihita wana matokeo mazur adv.Hinawezekana kupata GPA kubwa hata ukiwa vyuo vya gvt issue KUJiTAMBuA

upo coet mwaka wa ngapi?
hebu niambie na upo group namba ngapi plz
 
jamaa wanalalamika et GPA kubwa vyuo vya private.
Mbona watu walio serious gvt tunapiga GPA kubwa kishenzi tuacha mambo ya ajabu tatzo walioko vyuo vya gvt wanajarbu kuja na historia za 4m6 et div 1,2. ukwel ni kwamba wanajisahau na kula bata mm shaidi nipo ud tena COET lkn GPA kama 4,zipo sasa kaa unalalamika utakoma kwenye soko LA ajira achane urmbuken na mademu someni .name matokeo ya div hayana msaada.kumbuka % kumbwa wenye div 3 na 4. adv wanakuwa na juhud za kusoma wafikapo chuo zaid ya wajihita wana matokeo mazur adv.Hinawezekana kupata GPA kubwa hata ukiwa vyuo vya gvt issue KUJiTAMBuA

Mwanafunzi wa CoET ,?. kwa uandishi huu sidhani hata form4 ushamaliza
 
Back
Top Bottom