Wa kuabudiwa, kutukuzwa na kusujudiwa ni Mungu pekee!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,

Leo kuna SMS nimetumiwa, niliposema humu kuhusu hiyo SMS imeleta kizaazaa na kutoleana maneno mabaya
hadi baadhi ya watu humu kutoleana maneno ya kufuru Mungu. Kuwa kitendo cha kumkubali, kumsifu na kumpongeza mtu fulani kunahesabiwa, ni kumuabudu, kumtukuza na kumsujudia, kitu ambacho si kweli!.
Pongezi hizo ni za kumkubali kutokana na utendaji kazi wake uliotukuka wenye kuleta matokeo chanya. Hivyo pongezi ni za kumpa moyo aendelee kufanya makubwa na sio kumuabudu, kumtukuza au kumsujudu.

Naendelea kusisitiza wa kuabudiwa, kutukuzwa na kusujudiwa ni mmoja tuu, "The One and Only God - Mungu Baba Pekee"

Hivyo nawaomba please
please, please, tusitake kumponza na huyu kama tulivyomponza yule kwa hizi lugha za machukizo.

Nawatakia sensa njemau tujitokeze kwa wingi kuhesabiwa!

Paskali.
 
Ninajaribu kukutetea lakini wapi naona unaendelea kujichafua mwenyewe khaaa...umekuwaje lakini?

Hizi nyuzi za kitoto waaachie akina johnthebaptist na uvccm washamba.

Pascal punguza hizi mada nyepesi sio size yako.
Kama uliteoeza kwa uzi ule ukashambuliwa busara ni kunyamaza tu
 
Hahaha.......pole sana bwashee!
 
Hilo na kumheshimu halina ubishi kwani lipo tu automatically.

Lakini kumkubali, kumsifu na kumpongeza yategemea na "output" ya uongozi wake na nini ameweka humo katika "input".

Utaeleweka ikiwa utaongelea kwa uzito wake hayo mambo matatu ukichambua lipi ni la kumkubali, kumsifu na kumpongeza huku pia ukitanabaisha ni yepi huwezi kumsifu, kumkubali na kumpongeza.

Hapo utakuwa umeipaisha sifa yako kubwa na uchambuzi makini.

Tuache unafiki tuwe wakweli tuwe wawazi.
 
Paskali unajua mitandao na teknolojia Ina tabia ya kuweka kumbukumbu muda mrefu sana, unataka kuja kuwaonesha watoto wako na wajukuu zako kitu gani aisee. Kwanini unachagua cheap popularity Paskali?

Achana na ujinga huu kaka. Utawapa wakati mgumu watoto wako mbele ya jamiii iliyostaarabika

Usiponzwe na machawa mengi yasiyotumia majina Yao kamili kwenye mitandao
 
Ye mwenyewe unayemsifia anajua amechemka ndio maana inafikia hatua analalamikia wapiga picha wanaficha raia kwenye mikutano yake.
 
Hahah kachafuka kisha anajisafisha kwa kutumia oil chafu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…