Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
- Thread starter
- #41
Baada ya Dr. Bashiru kufanya ukosoaji, wale waabudu watu wamekuja juu kama moto wa kifuu na kumshukia kama mwewe anayesarandia kifaranga cha kuku!, utadhani Dr. Bashiru amemkufuru Mungu!. Aliyekosolewa ni binadamu!, tuendelee kumsifu kwa kuupiga mwingi, ila hala hala, tusipitilize, tukajikuta ni kama kumuabudu fulani au kumtukuza fulani hivyo tukajikuta tunamponza bila kujijua!. Kusifu, sifuni kwa kiasi, tusipitilize badala ya kusifu ikageuka machukizo!.Wanabodi,.
Naendelea kusisitiza wa kuabudiwa, kutukuzwa na kusujudiwa ni mmoja tuu, "The One and Only God - Mungu Baba Pekee"
Hivyo nawaomba please
please, please, tusitake kumponza na huyu kama tulivyomponza yule kwa hizi lugha za machukizo.
Paskali.
P