Ndugu zangu macho yetu watanzania ndani na nje ya mipaka yetu yakaelekezwa kwa Mama huyu shupavu, mwenye moyo wa huruma upendo na unyenyekevu ulio jaa hekima busara Subira na Aliyejaa hofu ya Mungu, mwenye upendo wa kweli kwa watu na mzalendo wa dhati kwa nchi yetu, msikivu na mwenye kumaanisha kile akitamkacho, mwenye kuchuja maneno na kuchunga ulimi wake
Mh Rais wetu mpendwa Taratibu akaanza kufufua na kuinua matumaini ya watanzania ambayo wakati huo Tulikuwa Tumetoka kwenye majonzi na mshituko, akaanza kuwa mfariji wetu, Akaanza kutufuta machozi, Akaanza kutushika mikono kutunyanyua tulipo kaa ili tuanze safari ya Kuendelea kazi ya kuijenga nchi yetu kwa kauli yake ya kazi iendelee, Akaanza kutuunganisha watanzania kukabili maadui wetu wa ujinga umasikini maradhi Rushwa na ufisadi
Kuna watu walikuwa wamekata Tamaa, Kuna watu walikuwa wanatamani hata kuona kila baya linaipata Tanzania, lakini mama huyu Hodari akazizima roho hizo chafu na kupanda mbegu za upendo na uzalendo katika mioyo watanzania, Ndio maana unaona Leo hii Taifa Ni moja likisonga kwa pamoja,