Naomba ieleweke na iendelee kueleweka. Kanisa la Roman Catholic linasherehekea KUMBUKUMBU YA KUZALIWA YESU KRISTU, na linatambua wazi kwamba tarehe halisi ya kuzaliwa Yesu haipo katika kumbukumbu. Kwa hiyo mtu yeyote wa imani yoyote anayedhani kwamba ANALETA HOJA MPYA KWA kusema kuwa tarehe 25 Disemba sio tarehe halisi ya kuzaliwa Kristu, basi ajue kuwa HIYO SIO HOJA MPYA, HATA RC WANAJUA SIO TAREHE HALISI. Kwa mantiki hiyo, uzi wowote au post yoyote inayohoji, haitakuwa na majibu zaidi ya kwamba HIYO NI KUMBUKUMBU YA KUZALIWA KRISTU.
Iwapo wewe unasherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwamko (ni kumbukumbu maana katika uchanga ule, haukuwa na akili ya kujua tarehe halisi zaidi ya kusimuliwa), iweje uzuie wengine wasisherehekee KUMBUKUMBU YA KUZALIWA KRISTU? Wewe ni zaidi ya Kristu? Sikukuu njema!