Wa-Tanganyika tuamke, tulinde haki zetu

Wa-Tanganyika tuamke, tulinde haki zetu

JERUSALEM 2006

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2012
Posts
527
Reaction score
596
Wasalaam wana Jamvi!

Moja kwa moja kwenye mada.

1. Hakuna watu wenye raha katika nchi hii kama Wazanzibari. Wao wana privillages nyingi sana katika taifa kuliko mwananchi wa sehemu yoyote. Wao ni kama wana wa Mfamle na Watanganyika ni vijakazi wao.

Wana Uhuru wa kuishi upande wowote wa muungano na kupata haki zote bila shida yoyote, kitu ambacho ni ndoto kwa Watanganyika wakienda Zanzibar. Hawapewi haki yoyote ile katika visiwa hivyo. Sina haja ya kuelezea kila kitu kwa kuwa kuna nyuzi nyingi humu zimeeleza kwa upana sana.

2. Sasa limekuja swala la mikopo ya nje na ajira. Zanzibar wanatunyonya sana waTanganyika kama vile hamnazo hivi.
Kweli inaingia akilini kwa nchi yenye idadi ya watu 2M kupata Mkopo kwa 25% na ajira 21% dhidi ya nchi yenye watu 58 M?

3. Yote tisa, kumi mimi ninawataka Watanganyika ambao ni Pro-Muungano wa aina hii wanipe faida zinazotokana na Muungano huu kwa watu wa Upande wa Bara? Kwa Lugha nyepesi, mimi mtu wa Morogoreo nina faidika vipi na uwepo wa Muungano huu zaidi ya hasara.?

MWISHO! Jamani tuamke tulisemee taifa letu, tunataka usawa katika nchi yetu na sio vinginevyo
 
Mkuu, wamepewa fedha kwa ajili ya miradi ya maji tu. Ni maji tu ya kuoga, kufulia, kupikia na kunywa.
Wala hata sio hela ya bia na bata.

Au kuna ubaya mkuu ?
Maana naona msingi wa hoja yako umeanzia kwenye mgawo wa huo mkopo wa "mabeberu".
 
Wale chama dola wakikusikia watadai wewe sio mzalendo, mara unahatarisha amani iliyopo, ila upande wa pili hakuna chamaana zaidi ya ukoloni mambo leo
 
Embu twende na uhalisia:

Taifa la Tanganyika, eneo lake ni eneo lote la Tanzania Bara ya sasa.

Kwa hiyo waliokuwa Watanganyika, ndiyo wanaitwa Watanzania kwa sasa.

Kisheria, Watanganyika hawapo na hata ardhi yao haipo. Ila, Watanzania wapo na ardhi yao ipo.

Zanzibar wana eneo lao kisheria. Wana watu, Serikali n.k. Watanzania, ambao Watanganyika wa zamani, nao wana serikali yao na taasisi zake.

Kwa hiyo, Watanganyika unaowataka wapiganie haki zao hawapo kwa sababu sasahivi Wanaitwa Watanzania kuanzia April, 26 1964.

Ila Wazanzibari wapo kisheria na haohao Wanzanzibari wanatambulika kisheria kama Watanzania.

So kuna Watanzania Wanzanzibari na kuna Watanzania ambao siyo Wazanzibari. Yaani, ni sawasawa kusema, kuna Watanzania Wasukuma na kuna Watanzania amabo siyo Wasukuma, maana wengine ni Wachagga, n.k.

Lakini, wewe unayejiita Mtanganyika, kwa mfano, ukienda Zanzibar au kupewa unachokitaka huko, kitabadilishaje maisha yako?

Lakini pia, ukibadilishwa jina ukaitwa Mtanganyika, kimsingi haitabadili kitu. Yaani haina tofauti na Mpare atake aitwe Mchagga.

Kimsingi, iliyokuwa Tanganyika ndiyo sasa Tanzania, ikiwemo Zanzibar.

Na huwezi ukawaita Watanganyika na kuwahimiza maana hawa watu wenye jina hilo la Watanganyika hawapo.
 
nafikiri kuna mambo mengi ya kujadili ya muungano ili tukubaliane, na kama kunatakiwa kufanyika amendments yafanyike, kwasababu bado tunahitaji kuishi kwenye muungano. ila viongozi wetu wakifeli au kutotumia busara kwenye hili, watanganyika wakaamka na kuwa na mawazo mengine, nakuhakikishia utavunjika kwasababu watanganyika ni wengi hata kiiidadi, italeta mgawanyiko mkubwa sana. pia, hatutakiwi kuishi kana kwamba tatizo hili halipo, tutakuwa tunafuga jipu, tukubali kuna mambo yanatakiwa kuwekwa sawa, na tutafute suluhisho haraka nakuendelea na maisha. masuala ya kujifanya kama hakuna tatizo huwa yanaisha vibaya. zaidi ya yote, nafikiri katiba ya warioba hata ikiwa adopted leo, itatufaa kuliko hata kuanza kutafuta mpya nyingine. ili adress hayo mambo yote.
 
Wasalaam wana Jamvi!

Moja kwa moja kwenye mada.

1. Hakuna watu wenye raha katika nchi hii kama Wazanzibari. Wao wana privillages nyingi sana katika taifa kuliko mwananchi wa sehemu yoyote. Wao ni kama wana wa Mfamle na Watanganyika ni vijakazi wao.

Wana Uhuru wa kuishi upande wowote wa muungano na kupata haki zote bila shida yoyote, kitu ambacho ni ndoto kwa Watanganyika wakienda Zanzibar. Hawapewi haki yoyote ile katika visiwa hivyo. Sina haja ya kuelezea kila kitu kwa kuwa kuna nyuzi nyingi humu zimeeleza kwa upana sana.

2. Sasa limekuja swala la mikopo ya nje na ajira. Zanzibar wanatunyonya sana waTanganyika kama vile hamnazo hivi.
Kweli inaingia akilini kwa nchi yenye idadi ya watu 2M kupata Mkopo kwa 25% na ajira 21% dhidi ya nchi yenye watu 58 M?

3. Yote tisa, kumi mimi ninawataka Watanganyika ambao ni Pro-Muungano wa aina hii wanipe faida zinazotokana na Muungano huu kwa watu wa Upande wa Bara? Kwa Lugha nyepesi, mimi mtu wa Morogoreo nina faidika vipi na uwepo wa Muungano huu zaidi ya hasara.?

MWISHO! Jamani tuamke tulisemee taifa letu, tunataka usawa katika nchi yetu na sio vinginevyo
Watanganyika tumelala usingizi wa pono tuamke!
 
Embu twende na uhalisia:

Taifa la Tanganyika, eneo lake ni eneo lote la Tanzania Bara ya sasa.

Kwa hiyo waliokuwa Watanganyika, ndiyo wanaitwa Watanzania kwa sasa.

Kisheria, Watanganyika hawapo na hata ardhi yao haipo. Ila, Watanzania wapo na ardhi yao ipo.

Zanzibar wana eneo lao kisheria. Wana watu, Serikali n.k. Watanzania, ambao Watanganyika wa zamani, nao wana serikali yao na taasisi zake.

Kwa hiyo, Watanganyika unaowataka wapiganie haki zao hawapo kwa sababu sasahivi Wanaitwa Watanzania kuanzia April, 26 1964.

Ila Wazanzibari wapo kisheria na haohao Wanzanzibari wanatambulika kisheria kama Watanzania.

So kuna Watanzania Wanzanzibari na kuna Watanzania ambao siyo Wazanzibari. Yaani, ni sawasawa kusema, kuna Watanzania Wasukuma na kuna Watanzania amabo siyo Wasukuma, maana wengine ni Wachagga, n.k.

Lakini, wewe unayejiita Mtanganyika, kwa mfano, ukienda Zanzibar au kupewa unachokitaka huko, kitabadilishaje maisha yako?

Lakini pia, ukibadilishwa jina ukaitwa Mtanganyika, kimsingi haitabadili kitu. Yaani haina tofauti na Mpare atake aitwe Mchagga.

Kimsingi, iliyokuwa Tanganyika ndiyo sasa Tanzania, ikiwemo Zanzibar.

Na huwezi ukawaita Watanganyika na kuwahimiza maana hawa watu wenye jina hilo la Watanganyika hawapo.
Una uhakika Watanganyika hatupo kweli? Ccm acheni kucheza na akili zetu bhana! Sasa huo Muungano wa 26/04/1964 ulikuwa ni kati ya nani na nani?

Siyo kati ya Tanganyika na Zanzibar! Sasa kwa nini leo mtuite watu wa Tanzania Bara? Nakuhakikishia Tanganyika itadumu milele. Na binafsi naamini ipo siku tu Tangaanyika itamuondoa huyu kupe anayeitwa Zanzibar kwenye ngozi yake.
 
Sera za muungano zipitiwe upya, iweje taifa moja ila wengine wanapata nafuu kwenye kodi na huduma zinginezo za msingi.
 
makubaliano mapya yawepo, kwenye matumizi ya umeme, mikopo, nk. kwani, kama zanzibar ina faida kwao kukopa wenyewe, kwanini tusiwaruhusu wakope kizanzibar kuliko kukopa kwa muungano, hela za muungano huwa ni zipi na ndio hizo huwa zinatumika kulipa huo mkopo?
 
Embu twende na uhalisia:

Taifa la Tanganyika, eneo lake ni eneo lote la Tanzania Bara ya sasa.

Kwa hiyo waliokuwa Watanganyika, ndiyo wanaitwa Watanzania kwa sasa.

Kisheria, Watanganyika hawapo na hata ardhi yao haipo. Ila, Watanzania wapo na ardhi yao ipo.

Zanzibar wana eneo lao kisheria. Wana watu, Serikali n.k. Watanzania, ambao Watanganyika wa zamani, nao wana serikali yao na taasisi zake.

Kwa hiyo, Watanganyika unaowataka wapiganie haki zao hawapo kwa sababu sasahivi Wanaitwa Watanzania kuanzia April, 26 1964.

Ila Wazanzibari wapo kisheria na haohao Wanzanzibari wanatambulika kisheria kama Watanzania.

So kuna Watanzania Wanzanzibari na kuna Watanzania ambao siyo Wazanzibari. Yaani, ni sawasawa kusema, kuna Watanzania Wasukuma na kuna Watanzania amabo siyo Wasukuma, maana wengine ni Wachagga, n.k.

Lakini, wewe unayejiita Mtanganyika, kwa mfano, ukienda Zanzibar au kupewa unachokitaka huko, kitabadilishaje maisha yako?

Lakini pia, ukibadilishwa jina ukaitwa Mtanganyika, kimsingi haitabadili kitu. Yaani haina tofauti na Mpare atake aitwe Mchagga.

Kimsingi, iliyokuwa Tanganyika ndiyo sasa Tanzania, ikiwemo Zanzibar.

Na huwezi ukawaita Watanganyika na kuwahimiza maana hawa watu wenye jina hilo la Watanganyika hawapo.

Ok twende na Logic yako.

Mtanzania mwenye asili ya upande wa bara anafaidika vipi na huu muungano?

Kipi hasa anakipa akienda Zanzibar ambacho waZanzibari wakija bara wanapata??

Tusaidie hapo Mtaalam
 
hivi wabunge wa bara huwa hawalioni hili, au ni mwiko kuliongelea? hakuna hata mmoja anajilipua kutoa hoja hii ijadiliwe? ndio ataona watu wengi mtaani watakavyomsapoti. au wanatetea ugali wao tu.
 
Hakuna wabunge mule, wanaangalia matumbo yao na teuzi tu, wapo wapo tu!
 
Back
Top Bottom